Dr.Dennis S Wamalwa

Dr.Dennis S Wamalwa

Share

Am An Entreprenuer At Webuye

12/05/2021

.... LIPO TUMAINI, THERE'S HOPE! Ayubu 14:7-8,

Kwa maana lipo tumaini kwa mti, k**a ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini
na kisiki chake kufa udongoni, lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi k**a mche...at least there is hope for a tree if it is cut down, it will sprout again, and it's new shoots will not fail.....mti unaweza ukakatwa na habari njema ni kwamba huo mti utachipuka tena, kwa harufu ya maji huu mti utapata uhai na utasimama tena nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Unaweza kuwa umekatwa na hauna nguvu ya kusimama tena, lakini kwa kusikia neno hili utasimama tena. Kuna machipukizi mapya yanayochipuka katika maisha yako, haya machipukizi hayatakoma, yatachipuka na kufanya usimame tena. Be encouraged kwamba hapo ulipo si mwisho wako, biashara kuanguka, ndoa kuharibika, kupoteza kazi na mengi sio mwisho, utasimama tena! Barikiwa sana na Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

15/02/2021

.... JEHOVAH JIRE, The Lord will provide!
Mwanzo 22: 13-14...

Ndipo Abrahamu akainua macho yake, na hapo karibu mbele yake kulikuwa na kondoo dume aliyenaswa kwa pembe zake kichakani. Kwa hiyo Abrahamu akaenda na kumchukua kondoo dume huyo na kumtoa dhabihu ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Naye Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire. Ndiyo sababu mpaka leo inasemwa: “Katika mlima wa Yehova itaandaliwa.”....So Abraham called that place The Lord Will Provide. And to this day it is said, “On the mountain of the Lord it will be provided. Hii wiki Jehovah Jire ataonekana katika maisha yako, HE WILL PROVIDE! Mahitaji yako yote anayajua, anakuandalia ushuhuda. Uwe na wiki ya baraka, Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

11/02/2021

...WAOVU NI CHUKIZO MBELE YA MUNGU. Methali 3:19-35..
Usipange maovu dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe bila wasiwasi. Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote. Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake. Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu. Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.
Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha. Neno liko wazi... Mungu hapendi uovu. Wacha kupangia mtu maovu, wacha kugombana na watu ovyo ovyo, usiwe mwenye dharau Mungu asikudharau, waovu watapata fedheha na aibu sana. Barikiwa na Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

05/02/2021

...NJIA ZA MUNGU HAZIELEWEKI! Luka1: 18-22

....Zakariya akamwambia huyo malaika.."Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu." How can i be sure of this?Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema. Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia." Zekaria alishangaa watapata mtoto vipi ilhali ni wazee. Kuna hali zinakuwa ngumu sana hadi unaona hakuna njia kabisa. Unajiuliza itafanyika vipi, njia itatoka wali, ripoti ya daktari imekufikia na hakika unaona giza kabisa. Leo Niko hapa nikutue nguvu ya kwamba mwangalie Mungu, yeye ndiye anayejua njia itatoka wapi, anajua vile atakavyofanya ili upate huo muujiza, ni kazi yake, mwachie! Uwe na wikendi tulivu tuonane Jumapili tupeperushe bendera ya 5am-10am.... Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

04/02/2021

...OMBI LAKO LIMEJIBIWA, YOUR PRAYER HAS BEEN HEARD! Luka 1:5-19
...........Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake....". Zekaria na mkewe waliishi maisha ya kumpendeza Mungu, maisha yaliyonyooka, lakini hawakuwa na mtoto na walikuwa wazee. Lakini waliletewa habari njema na malaika kwamba maombi yao yalikuwa yameshajibiwa na mtoto watakaopata ataleta furaha sana. Huwezi kaa vizuri na Mungu, utafute uso wake na mwishowe akuaibishe, haiwezekani! Hata katika uzee wako, atatimiza ahadi yake na atakuondolea aibu. Umemtafuta huyu Mungu sana, ameshasikia ombi lako na anakutengenezea ushuhuda, wengi watafurahia baraka yako na itawasaidia. Barikiwa leo na Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

03/02/2021

... USIOGOPE MUNGU ATAKUSAIDIA,THE LORD YOUR GOD WILL HELP YOU! Isaya 41: 11-13.
“Naam! Wote waliokuwakia hasira, wataaibishwa na kupata fedheha. Wote wanaopingana nawe, watakuwa si kitu na kuangamia. Utawatafuta hao wanaopingana nawe, lakini watakuwa wameangamia.Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia,
‘Usiogope, nitakusaidia.’ Usiogope wapinzani wako, watakuinukia kwa hasira lakini hawatakushinda, wataangamia na hutawaona tena. Kuna watu ambao ni sumbua sana, kazi yao ni kushusha na kupinga watoto wa Mungu na kukuonyesha kwamba hauwezi chochote. Biblia inasema kuwa usiwaogope, Mungu ameshikilia mkono wako na ameahidi kukusaidia. Tulia, usijibishane na wao, usikose usingizi, mwangalie Mungu msaada wako! Uwe na Jumatano njema na Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili

02/02/2021

HI MEMBERS

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Bungoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address

Bungoma