31/05/2026
Simba SC imefungua mazungumzo na Fiston Mayele ili kuangalia uwezekano wa kumsajili k**a mchezaji huru.
Mayele ni mchezaji huru hadi kufikia June. Miongoni mwa timu zinazomhitaji ni Kaizer Chiefs. Ila Simba SC wameingia mazima. Taarifa kutoka kwa chanzo changu, mazungumzo yameanza na huenda yakakamilika siku chache hapa Dar es Salaam.
28/05/2026
Matar Cisse Wapo Katika Mpango Wa Kumpeleka Winga Wa Simba Libasse Gueye Nchini Belgium(Ubelgiji) Katika Timu ya Standard Liege Kufanya Majaribio Mwishoni Mwa Msimu Huu
Standard Liege Endapo Watavutiwa Na Kiwango Cha Libasse Gueye Watapeleka Ofa Simba ya Kumsajili Libasse Gueye
Matar Cisse Chini Ya Kampuni Yake Ndie Aliyesimamia Usajili Wa Libasse Gueye Kutoka Teungueth FC Kujiunga Na Simba.
26/05/2026
Glody Likonza Ni Miongoni Mwa Majina Yanayotizamwa K**a ingizo Jipya Katika Eneo La Kiungo Wa Kati(Namba Nane 8) Upande Wa Simba
Glody Likonza K**a Usajili Wake Utakamilika Atakua Ndie Mrithi Wa Allasane Kante Ambaye Amekalia Kuti Kavu Katika Kikosi Cha Simba
Likonza Kwa Sasa Anacheza Usm Alger Ya Nchini Algeria Glody Likonza Amekua Akipata Nafasi Finyu Katika Kikosi Cha Usm Alger Chini Ya Kocha Lamine Ndiaye
Usajili Wa Likonza Unaweza Kukamilika Endapo Simba Wataamua Kuachana Na Allasane Kante.
25/05/2026
Simba wameingia rasmi kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji hatari wa ASEC Mimosas, Kelvin Bakare, raia wa Ivory Coast ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba umeanza kufanya mawasiliano ya awali kwa ajili ya kumfuatilia mshambuliaji huyo wenye kasi, nguvu na umaliziaji mzuri ndani ya ligi ya Ivory Coast. Bakare ameonyesha kiwango cha juu akiwa na ASEC Mimosas, ambapo ameripotiwa kufunga mabao 17 katika mashindano mbalimbali msimu huu na kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu hiyo kutwaa ubingwa.
Mshambuliaji huyo ameendelea kuvutia macho ya vilabu kadhaa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza k**a namba 9 wa kisasa, huku akitajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia mipira ya juu, kucheza kwa nguvu pamoja na kutengeneza nafasi ndani ya eneo la hatari. Kiwango chake hicho kimeifanya Simba kuona kuwa anaweza kuwa suluhisho la kuongeza makali ya safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.
Hata hivyo, Simba haitakuwa peke yake katika mbio hizo kwani taarifa zinaeleza kuwa klabu ya Al Masry kutoka Misri pamoja na Grenoble Foot inayoshiriki Ligue 2 nchini Ufaransa nazo zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma za mshambuliaji huyo. Ushindani huo unaweza kufanya dili hilo kuwa gumu kutokana na thamani yake kuendelea kupanda baada ya msimu mzuri aliokuwa nao akiwa na Asec mimosas.
25/05/2026
Kelvin Nashon Naftal ameripotiwa kujiunga na Simba akitokea katika Klabu ya Pamba Jiji ya Mwanza.
Nashon (26) anakuwa mchezaji wa pili kumalizana na Simba kabla ya ligi kumalizika mara baada ya taarifa kusambaa zikimhusisha nyota wa TRA Chobwedo kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi.
24/05/2026
Ana lazimisha kufunga sehemu ambazo unaona wazi hawezi kufunga, mpanzu alikuwa ameanza kubadilika ila naona anarudi kuwa yule wa msimu ulio pita.
Simba asipo Pata point tatu Leo lawama lazima ziende kwake.
22/05/2026
Nathaniel Chimbalo Amefikia Makubaliano Ya Kujiunga Na Simba Kwa Mkataba Wa Miaka Miwili
Chilambo Anaenda Kuungana Na Kapombe na Duchu Kwa Msimu Ujao
Chilambo Ni Mchezaji Mwenye Sifa Na Uwezo Wa Kutumia Miguu Yote Miwili Hivyo Ni Faida Kwa Simba Kumsajili Chimabo Sababu Anao Uwezo Wa Kutumia Mguu Wa Kulia Na Kushoto Kwa Ufasaha.
21/05/2026
Ametoa assist Kwa Magoli yote ya Simba Leo hivyo na kumfanya kuibuka Nyota Bora Wa Mchezo.
Mwaga moto Kwa Chama.
21/05/2026
-Leo kuanzia Goals mpaka assists ni usajili wa dirisha dogo la mwezi January...Chama, Oura na Libasse 🔥
Chama ametoa assist 2 kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union...
Kumfananisha Chama na Okello ni kuukosea mpira...
Chama anakuwa mchezaji wa kwanza Duniani kutwaa Tuzo 5 za MoTM mfululizo...Haijawahi kutokea kwenye ligi yoyote Duniani.
21/05/2026
Huyu Chama kumzungumzia Kwa Sasa ni tabu mno mana hatumuelewi.