Sophie Sports

Sophie Sports

Share

Football updates and news

11/08/2021

UEFA SUPER CUP 2021🏆

Ni mechi ya ufunguzi katika mashindano ya UEFA- UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA UEFA EUROPA LEAGUE.
Ni mechi itakayowakutanisha washindi wa michuano ya UEFA- Champions League na UEFA EUROPA League WA msimu uliopita; Chelsea na Villarreal mtawalia.

Mechi yenyewe itachezwa katika uwanja wa Windsor Park Belfast, Northern Ireland🇬🇬, majira ya saa nne usiku wa tarehe 11 Agosti 2021.

Muamuzi wa mechi hii atakuwa ni raia kutoka Urusi🇷🇺-Sergei Karasev huku akisaidiwa na wenzake Igor Demeshko, Maksim Gavrilin, huku forth official akiwa ni raia wa Balerus🇧🇾-Alexey Kulbakov.

Mashabiki watakaoruhusiwa kuingia uwanjani ni wapatao 13000

Nani ataibuka kidedea?...Tuchel au Emery?🤔
Tukutane ndani ya dakika 90'

Photos from Sophie Sports's post 11/08/2021

LIONEL MESSÌ TALK🗣️
Baada ya kukamilisha uhamisho wake hiyo jana na kilabu cha PSG ya Ufaransa 🇫🇷, na kutia sahihi mkataba utakaodumu hadi Juni 2023, Messì alikuwa na haya ya kusema;

🗣️"Nina furaha kubwa kuanza maisha mapya ndani ya PSG"

🗣️"Kila kitu kuhusu PSG kinaendana Sawa na malengo yangu kabisa"

🗣️"Natambua ukubwa na uwezo wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji waliopo hapa"

🗣️"Kwa pamoja natamani tufanye mambo makubwa Kwa ajili ya kilabu na mashabiki wa PSG"

🗣️"Siwezi kungoja kutia wayo wangu katika uwanja wa Parc Des Princes"

Baada ya uhamisho wake Lionel Messì msimu huu unaoanza atavalia jezi nambari 30.

07/08/2021

THE COMMUNITY SHIELD 🏆
FT: LEICESTER CITY 1-0 MANCHESTER CITY
89'K.Ihenacho(pen)

Kelechi Ihenacho kupitia penalti anaizamisha timu yake ya zamani na kuipa Leicester City ubingwa wa kombe la ngao la jamii msimu huu.

Kinachofuatia ni ufunguzi wa mechi za EPL rasmi wikendi ijao. Leicester City watakuwa wageni wa Wolves katika mechi Yao ya ufunguzi msimu huu.
Manchester City nao wataanza kampeni ya kutetea taji lao la ligi wakiwa nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspurs tarehe 15.

07/08/2021

THE FA COMMUNITY SHIELD 🏆
WEMBLEY STADIUM
7:15PM EAT

Naam, unaambiwa ni mechi ya ufunguzi inayokutanisha mabingwa wawili tofauti. Mmoja ni bingwa wa EPL🏆 huku mwingine ni bingwa wa kombe la Emirates FA Cup🏆.

Manchester City walijitakia nafasi ya kucheza mechi hii baada ya kuzipiku timu zingine 19 na kunyakua ubingwa wa EPL 🏆 msimu uliopita.

Leicester City nao walijikakamua na kushinda timu ya Chelsea kwenye fainali ya kombe la Emirates FA cup 🏆. Iakuwa usiku wa Nani leo?🤔

Mara ya mwisho timu hizi zilikutana ilikuwa katika pambano la ligi pale King Power Stadium. Mechi yenyewe iliishia 0-2 Kwa faida ya vijana wa Pep Guardiola.

Huenda isiwe kombe la maana Kwa macho ya wengi lakini ni kocha yupi hangependa kuona akianza msimu angalau na kombe kabatini😁..tusubiri dakika 90'⚽

05/08/2021

RASMI- Lionel Messi aondoka Barcelona.
" Pande zote mbili zinasikitishwa kuwa matamanio ya mchezaji na kilabu hayajaweza kuafikiwa".

CHANZO- Goal

Photos from Sophie Sports's post 05/08/2021

✍️... EPL🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 REMINDER⚽
LEICESTER CITY-PART 2
.....INAENDELEA;

Baada ya kufanikiwa kusalia kwenye ligi kuu, Nigel Pearson akaachishwa kazi Kwa matamshi yake ndani ya press conference Kwa kumtukana mwandishi wa habari....' and I.. think you are an ostrich 😂,' ndio matamshi yaliomwachisha kazi kocha huyu. Kibarua kikawa kumtafuta meneja wa kumrithi.

Mara jina likatokea; Claudio Ranieri- washika dau wa soka wakashangaa Sana na uamuzi huu, moja wao akiwa Gary Linker. Lakini msimamo wa mabosi wa Leicester City ukawa ndio huo, Claudio Ranieri ndiye haswa😃.

Msimu wake wa Kwanza akiwa mkufunzi, hakuna aliyetabiri kuwa angefanikiwa na kilabu hiki cha East Midlands.

Mechi baada ya mechi... Wikendi baada ya wikendi... Goli baada la lingine... The Foxes wakaanza kutamba. Kila wikendi ungewasikia watangazaji wa soka wakitaja majina k**a👉 Jamie Vardy, Albrighton, Mahrez...yote kisa, maajabu walikuwa wakiyafanya uwanjani..ukawa ni mwendo wa pointi tatu kila wikendi. Mashabiki wakaaanza kuamini kuna Jambo la kutokea😃....

Hata inapofika Januari mwaka wa 2016 Leicester City ndio walikuwa kileleni, wakawa k**a ndovu aliepanda mtini hakuna ajuawe alivyofika pale😅...

Mechi moja nusura iwapokonye roho mashabiki wa Leicester city 😂.... February Ile Danny Welbeck anazamisha free kick yake Ozil kwenye wavu wa Shmichael, wakajua kombe limewatoka vile, kumbe ya Mungu mengi tu 😁....

Wapinzani wao wa karibu Spurs wakawa na mechi ya MUST WIN dhidi ya Chelsea kuzuia kombe lisiende King Power stadium. Mashabiki wote wa Leicester City, ikiwemo Mimi😂 tulikuwa kwenye banda umiza😂😂 tupo nyuma ya Chelsea . Ila kipindi cha Kwanza kinakamilika; Chelsea 0-2 Spurs.Duh🙆‍♂️...tukajua hapa pagumu....
Kipindi cha pili Cahili pamoja na Eden Hazard wakahakikisha Spurs wanapoteza alama mbili na kupeleka ubingwa 🏆wa kihistoria King Power statdium...

Ukawa ndio ubingwa 🏆Bora wa muda kuwahi kushuhudiwa EPL...hivi kutatokea surprise nyingine msimu mwingine 🤔au ndio hivo?

Tbt hiyo👇

04/08/2021

✍️.... EPL🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 REMINDER⚽
LEICESTER CITY-PART 1
12 May 2013- Vicarage Road–shambulizi la kushtukiza kupitia timu ya Watford lilizamisha matumaini ya mashabiki wa Leicester city( matumaini ya kujikatia tiketi ya kucheza Ligi Kuu Uingereza)💔

Msimu uliofata Leicester City wakatawazwa mabingwa wa SKYBET CHAMPIONSHIP na kufuzu kucheza Ligi Kuu baada ya kumaliza msimu wakiwa na alama 102😃

Msimu wa Kwanza EPL haukuwaendea Sawa vijana wa Nigel Pearson wenye jina la utani The Foxes. Kila mechi walizidi kuipoteza alama, Jambo lililopelekea wao kushikilia nafasi ya mwisho kwenye jedwali la EPL Kwa siku 140😳. Wadadisi wa soka walikuwa na uhakika timu hii ingeshushwa daraja lakini bado mechi 9 tu ligi ikamlilike, yakatokea yakutokea...

9 MATCHES TO GO; amini usiamini The Foxes walijikakamua na kushinda mechi Saba Kati ya tisa zilizosalia na kujiweka salama kwenye ligi Kuu. Wak**aliza wakiwa nafasi ya 14😃.....ITAENDELEA.

Photos from Sophie Sports's post 12/06/2021

Fikra zetu na maombi kwake Eriksen 🥺

11/06/2021

EURO 2020
𝐌𝐀𝐓𝐂𝐇 𝐅𝐀𝐂𝐓𝐒.
Turkey 🇹🇳 Vs Italy 🇮🇹

1.Mara ya mwisho Italy na Turkey kukutana kwenye michuano ya kimataifa ilikuwa Euro 2000 tarehe 11 Juni , mechi ya ufunguzi. Mechi yenyewe iliishia 2-1 kwa faida ya Italy.

2.Italy hawajawai kupoteza michuano mikubwa ya kimataifa-Iwe Euro ama world cup kwenye uwanja wa Stadio Olimpico. Wameshinda 6 na kutoka Sare 2.

3.Michuano zote nne za ufunguzi katika Euro ambazo Turkey wameshiriki wameishia kuzipoteza.

4.Licha ya kucheza michuano 38 katika dimba la European championship, Italy hawajawai kufunga zaidi ya magoli mawili kwa mechi moja😂

5. Turkey katika michuano ya kufuzu Euro 2020 wameruhusu magoli chache (3). Rekodi bora ya ulinzi pamoja na Ubelgiji🇧🇪

6.Kwake Roberto Mancini(THE BOSS) itakuwa shindano lake kubwa la Kwanza k**a mkufunzi wa Italy.

7. Kwake Senol Gunes itakuwa shindano lake kubwa la pili k**a mkufunzi wa Turkey baada ya kuwafikisha nusu fainali na kumaliza wa tatu katika Kombe la Dunia mwaka wa 2002.

09/06/2021

RASMI:
Maurizzio Sarri ameatia sahihi mkataba wa kuisuka Lazio hadi Juni 2023.

Source: Fabrizio Romano

07/06/2021

FC Barcelona wanapania kumpa Memphis Depay mkataba utakaodumu hadi Juni 2024.
Pia Barca wameweka mezani mkataba wa Miaka mitatu ulioimarishwa ili kukamilisha dili hiyo haraka iwezekanavyo, ili kuzuia kitendo alichokifanya Wijnaldum aliyebadili nia na kuniunga na PSG.

Source : Fabrizio Romano

01/06/2021

RASHMI:
Henrikh Mkytaryan America sahihi mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia AS Roma Hadi Juni 2023.
(Source: Fabrizio Romano)

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Arusha