MANJA SPORT news

MANJA SPORT news

Share

page inahusu habari za michezo na burudani

05/01/2022

Klabu ya Yanga leo Jumatano, imesaini mkataba wa makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Card kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ambayo inaingia katika mfumo mpya wa uendeshaji ambapo kadi moja itauzwa TZS 29,000.

Kadi hiyo upande wa mbele una maelezo mbalimbali pamoja na picha na jina la Mwanachama huku upande wa nyuma ukiwa na picha ya jengo la Makao Makuu ya Yanga na kauli mbiu ya ‘daima mbele, nyuma mwiko’.

05/01/2022

RASMI : Mchezo wa kesho wa Nusu Fainali ya Kombe la Carabao Cup hatua ya mkondo wa kwanza kati ya Arsenal dhidi ya Liverpool umeahirishwa. Baada ya Liverpool kuomba mchezo huo kuahirishwa kutokana na mlipuko wa COVID-19 katika klabu hiyo.

05/01/2022

28🕞 Simba 1-0 selem view
25' Pape osuman sakho

Mapinduzi cup🏆

04/01/2022

🚨Taarifa kutoka katika chanzo cha uhakika kinadai Mchezaji Clotous Chama amekutana na Eng Hersi nchini Zambia hotelini

-kuna mazungumzo yanaendelea Kwa pande mbili ,huku Berkane wakiusishwa kudai Dola laki 2 Kwa Mchezaji huyo
haijajulikana k**a Yanga watakuwa tayari kutoa kiasi hicho kinachotajwa !

04/01/2022

🚨Klabu ya Simba imemtangaza Mtangazaji kijana wa Michezo, kuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo. Kabla ya kujiunga na Simba, Ahmed alikuwa akifanya kazi Azam Media.

🇹🇿

31/05/2021

TUKISEMA UKWELI ETI TUNAONGEA SANA.

Follow MANJA SPORT news

Nilishawahi kuandika hapa kwamba Yanga inahitaji uongozi bora au viongozi waliopo wakasome Qualities of good leadership,k**a wanajua Qualities za kiongozi basi wamesahau wakumbushwe,Kama hawajasahau basi waiache Yanga maana wanaiharibu Brand ya Yanga kwa makusudi.Nikaambulia kutukanwa.

Nilisema hayo baada ya kupata taarifa kwamba Carlinhos anajiamulia mambo ya kufanya na viongozi wakawa wanamtetea,Carlinhos alikuwa hataki kulala na wachezaji wenzie kambini alikuwa anataka kulala peke Yake.Viongozi wakamkingia kifua.

NILIKUWA NAWAKUMBUSHA TU EMBU TUENDELEE....

Hili la Carlinhos badala ya watu wa timu fulani kucheka na kufurahia tuchukue k**a Somo,kwani hii haijatokea kwa Yanga tu.Simba walikuwa na Junior Lukosa na Peter Mduhwa hawa waliishia kuvaa jezi tu.Azam walikuwa na Thierry Akono akaishia kuwa mtalii wa miezi kadhaa na kusepa.

Kwanini haya Yanatokea? Kifupi ni kwamba yanatokea kwa sababu timu zetu hazitumii Scouting kufanya sajili zao.Kifupi wakiona tu jamaa mweupe au mtu aliwahi kufunga magoli 17 na Esperance wanasajili.Nimesahau au wakiona ana Rasta.

Timu zetu zingekuwa zinatumia Scouts kufanya Sajili Yanga wangeijua tabia ya Carlinhos mapema sana hivyo wasingemsajili au wangemsajili na wangejua namna ya kuishi na Carlinhos.

Namaliza kwa kusema Africa ni africa,yaani mtu k**a carlinhos anaachana na klabu kwa sababu za kitoto kabisa.Eti kwa sababu ya mapenzi.Japo kunaweza kuwa na sababu nyingine ila na mapenzi ni moja ya sababu,yaani anataka kuwa karibu na mke wake.

follow hussein manja,

16/04/2021

:
👉Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wanapaswa kuonyesha ukubwa walionao kwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zote za ligi pamoja na zile za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

👉Tayari Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiwa inaongoza kundi A na pointi 13 inafuatiwa na vigogo Al Ahly ambao wana pointi 11 wakiwa nafasi ya pili.

👉Aprili 30 inatarajiwa kuchezwa droo ya michuano hiyo mikubwa. Gomes amesema kuwa anasubiri kuona wapinzani atakaopangiwa kucheza nao huku akibainisha kuwa wote anawatambua kutokana na kuwa na data zao pamoja na uzoefu wa soka la Afrika.

👉"Ukizungumza kuhusu Simba kwa sasa ni moja ya timu kubwa Afrika, hivyo nimewaambia wachezaji kwamba lazima waonyeshe ukubwa wao kwenye mechi zote ambazo tutacheza iwe ni kwenye ligi ama robo fainali.

👉"Kwa wakati huu tunawekeza nguvu zetu kwenye mechi za ligi ila haina maana kwamba tutapuuzia kuhusu mechi zetu za robo fainali kwani hiyo nayo ni mipango yetu kuona kwamba tunafanya vizuri.

👉"Natambua soka la Afrika vizuri na changamoto zake, nimefundisha Algeria ninazitambua timu za huko namna ilivyo na Afrika Kusini pia nina marafiki na data zao ninazo hivyo hakuna haja ya kuwa na hofu katika hilo," amesema

👉Timu ambazo zinaweza kukutana na Simba kwenye hatua ya robo fainali ni pamoja na CR Belouizdad ipo nafasi ya 10 na pointi 26 baada ya kucheza mechi 15 na MC Alger ipo nafasi ya 11 na pointi 25 baada ya kucheza mechi 16 hizi ni za Algeria na Kaizer Chiefs ni ya Afrika Kusini ipo nafasi ya 9 na pointi 24 baada ya kucheza mechi 20

16/04/2021



WAWA: HAKUNA WA KUZUIA UBINGWA SIMBA

BEKI wa kati wa Simba, Muivory Coast, Pascal Wawa ameibuka na kuweka wazi kuwa kutokana na ubora wao kwa sasa haoni atakayeweza kuwazuia kutetea ubingwa wao msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

Wawa ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi ljumaa, Wawa alisema: Nadhani bado tupo kwenye ubora ndiyo jambo kubwa la kumshukuru Mungu kwa sababu licha ya ushindani na ugumu wa ligi lakini bado tumekuwa na uwezo wa kupata matokeo bora zaidi kwa upande wetu.

Kiukweli naamini nafasi ya kutetea ubingwa wetu ipo wazi na hakuna ambaye anaweza kuzuia hilo kwa sasa kutokana na kuwa kwenye kiwango bora cha ushindani, kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kushinda mechi zetu ili malengo yatimie bila ya kuangalia nani anaongoza ligi" alisema Wawa.

MANJA SPORT news 12/04/2021

NEXT MATCH (VPL) SIMBA SC Vs MTIBWA SUGAR

"Simba Sc Wamesharejea nchini, tayari sasa kwa kuuvaa Mchezo na Mtibwa Sugar Juma tano hii Saa moja kamili Jioji, Simba wakiwakalibisha Mtibwa Sugar Katika uwannja wa Mkapa Stadium":-Afeicasport

MANJA SPORT news page inahusu habari za michezo na burudani

MANJA SPORT news 11/04/2021

V.A.R KUTUMIKA KWA MKAPA HIVI KARIBUNI

Shirikisho la mpira wa Miguu barani Afrika CAF limepanga wiki ijayo kuvitembelea viwanja vyote vitakavyotumika kwenye michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kuona uwezekano wa kuvifanyia majaribio ya Teknolojia ya VAR

Awali technilojia hiyo ilikuwa ikitumika kwenye mchezo wa Fainali tu ila mwaka huu CAF wataitumia kuanzia michezo ya Robo Fainali.

Uwanja wa Benjamini Mkapa ni moja ya viwanja vitakavyotumika kwenye Robo fainali ya Ligi ya mabingwa afrika Ukiwa ni uwanja wa nyumbani wa Simba SC.

MANJA SPORT news page inahusu habari za michezo na burudani

11/04/2021

CAF CONFEDERATION CUP

Namungo wamesafiri mpaka Zambia kukipiga na Nkana kwenye kombe la shirikisho la Afrika.

Mpaka sasa Namungo ana hali mbaya kwenye kundi akiwa hajafanikiwa kufunga hata goli 1 na yupo mkiani.

Kila la kheri Namungo.
Bendera ikapepee vyema huko Zambia.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Morombo
Arusha