28/08/2026
Asanteni Shule ya Karatu New Vision kwa kuniamini Mc Hongoli Kusherehesha mahafali ya tatu ya Darasa la Saba hakika ilifana sana hadi wakati mwingine tena.
Graduation team
Music The Real dj
Photographer📸 Richard Julius
Catering
27/08/2026
Asante Mungu Nimetimiza Mwaka Mmoja kwenye kazi ya u-Mc Mungu ni Mwema sana Mwaka Mmoja wa kujitafuta,kujifunza,Kukua na baadae Matokeo.
Kwenye Safari hii nipende kuwashukuru Wadau wote walioniamini kwenye kazi/Sherehe zao ikiwemo Harusi,Send Off,Mahafali,Engagement,Misiba,harambee,Shughuli za Kiserekali Nk.
Shukran za Kipekee ziende kwa Dj Wangu Godwell Mbise The Real dj ambae amekuwa anafanya kazi kwa kujituma wakati wote,hata Video au Posta zote yeye ndio anazianda 🙏
Niwashukuru Wapiga picha wote ambao nimeshafanyanao kazi,Pia niwashukuru Ma Mc’s ambao wamekuwa wakinipa ushauri mara kwa mara ya kuenenda katika kazi hii. Watu wa Sound hakika ilikuwa safari nzuri sana Asanteni.
Niwaahidi ya kwamba nitaendelea kufanya kazi kwa bidii ubunifu wa hali ya juu na kuzingatia Misingi ya kazi hii yenye ushindani mkubwa.
Kwenye mafanikio hapakosekani Changamoto Naomba unishauri chochote katika mwaka wangu mmoja wa kazi ya Mc ilinizidi kuwa bora zaidi.
MC HONGOLI NIITE NAMI NITAKUITIKIA
0750704851.
25/08/2026
WHAT A LOVE ❤️ 💍
Huu hapa Usingizi wa Aggy rasmi sasa ni Mr & Mrs Erick Luanda
Agness Michael Send Off Highlights
Mc Hongoli
0750704851
Photo 📸 Richard Julius
Dress Bellah Couture
Makeup MKONO WA DHAHABU
Music Master The Real dj
25/08/2026
Picha za boss wangu Agness Katika siku yake ya SendOff
Slide namba ngapi imekubamba.
📸 Richard Julius
20/08/2026
Picha za Kazini kwangu Leo Polisi Tanzania dhidi ya JKT Tanzania,Mungu ni mwema tumemaliza salama tukutane mechi ijayo TRA United vs Dodoma Jiji.
📸 FADHIL IBRAHIM
20/08/2026
MAJESHI DABI🙌 Imempendeza Mwenyezi Mungu nimeteuliwa na Bodi ya ligi kuu kusimamia na kuratibu mchezo wa ligi kuu namba 14 kati Polisi Tanzania dhidi ya JKT Tanzania inayopigwa leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
IMANI INALIPWA KWA UWEZO
15/08/2026
Siku ya kwanza kazini nimeteuliwa na bodi ya ligi kuu kusimamia na kuratibu mchezo wa ligi kuu ya Nbc kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Azam Fc utakaochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,imani inalipwa na uwezo tukutane Uwanjani.
10/08/2026
Leo nimeshiriki warsha ya waratibu wa mchezo (General coordinator) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa NSSF Mafao House Ilala Dar Es salaam,iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na bodi ya ligi kuu (TPLB). Asanteni sana TFF & TPLB kwa Semina Nzuri sasa Nipo tayari kuanza msimu mpya wa mashindano 2026/27 tukutane uwanjani.
📸 Honest Amon Mwanitega