03/09/2026
Mimi bwana nilikuaga na mpenzi wangu anaitwa Sam π tulipendana sana tu tena kipindi hicho me ndo Bado binti yani Bado mbichiiii.. Sam tulikutana ghafla sio kwamba tulikua ni watu tuliofahamiana sana yeye ni boda Sasa me nikawa naenda sehemu kusalimia ndugu zangu ikabidi wampe Sam namba yangu ili anipokee stend......
Nilifika akanipokeaga na kunipeleka mpka home na kiukweli Sam ni handsome japo me wakati huo sikumuwazia nikamchukulia k**a boda tu ππ zilipita k**a siku tatu kule nilipoenda kulikua na dada wa kazi Sasa nilikuaga nalala nae hiyo siku yule dada akanambiaga anaomba sim amtafute mtu mi nikampa.. akanambia me sijui kusoma Wala kuandika naomba niandikie af mtumie msg ya "mambo"
Katika kuandika si nikakuta ni namba ya Sam boda bwana me nikatuma k**a alivyonielekeza ππ akajibu poa me hapo nikataja jina la huyo mdada akanambia mwambie nakusalimia nikatuma, hiyo hakujibu kesho yake akaja kunibeba maan nilikua nilikua napeleka chakula hospital kulikua na mgonjwa Sasa usiku si ndo akaanza kunichatisha Mimi akanitongoza pale na me nilikua single af nikiangalia kaka mwenyewe mzuri anavutia we nikakubari π
Mida wote nilokaaga pale kwa mama angu mdogo sikuwahi kwenda kwa Sam Wala kukutana faragha zaid ya kuwasiliana tu na lbd akiagizwa aje nyumbani ndo tunaonana hivyo tu basi mi nilirudi kwetu huku tukiwa tunawasiliana mpk siku hiyo ananiambia anatuma nauli niende,,,,,, Sasa me kwakuwa nimempenda af nikiangalia naaga vip nyumbani Sam namtaka na nyumbani naagaje si nikatoeokaga bhna πππ aaaaah!!! Jaman! ACHA kabisa π
Mie huyo nikaenda mpka kupanda gari huyo kwa Sam nakwambia mapenzi yamenoga sam kanipeleka kwao hiyo siku siwezi kusahau nilivaa vitenge ilihali sikuwahi kujifunga funga vitenge nyieeeeee ππ nakwambia penzi tu lilikuaga Lele Lele π mama nae alipoa baada ya kuanza kutumiwa viela vya kulipa vikoba uko akawa kimya mpole na Mimi si ndo nikaona hapa ndo hapa... Baby anaondoka asubuhi akijisikia upwiru Anarudi mbio mbio mpaka home mchana wa jua Kali nampooza kazi zinaendelea,
SASA SIKU HIYO BWANA KARUDI MCHANA UPWIRU UMEMSHIKA K**A KAWAIDA TUKAWA TUPO CHUMBANI TUNAPETIANA PETIANA SI MLANGO UKAGONGWA, SAM AKAENDA KUFUNGUA NA MBABA UMESIMAMA ME NIKAWA ZANGU CHUMBANI HAPO NIMEPANDISHWA MORI NASUBIRI WAONGEE AONDOKE BABY WANGU AJE NDANI TULIANZISHEEE ππ
CHA KUSHANGAZA NIKAWA NASIKIA ANAMGOMEA KUINGIA CHUMBANI WAKAWA WANABISHANA BWANA π₯± ME NIKASEMA WATAJUA WAO ME NIKACHUKUA SIM NIKAANZA KUSIKILIZA ZANGU KWAYA MARA NIKASIKIA SAM ME KICHWA KINAUMA KANINUNULIE PANADOL πππ€£ YANI WANANGU HAPO ME SIJASHTUKA WALA ET NIENDE SEBLENI NIKAONE YANAYOENDELEA NIKAWA NIMETULIA NACHEZEA SIM TU.... SAMA AKAMWAMBIA HELA HII HAPA KANUNUE YULE DADA AKAKATAA BASI WAKATULIA ASA YEYE BWANA BAADA YA KUONA KAVURUGA IKABIDI AMPIGIE RAFIKI AKE MMOJA HV BODA MWENZIE AMBAE TUMETOKA MKOA MMOJA KWAHY SAM ALIPOANZA KUWA NA MIMI AKAANZAGA KUMWITA YULE SHEM, AKAMPIGIA SHEM WAKE AJE KUMSAIDIA.. YULE KAKA BAADA YA KUFIKA AKAMWAMBIA WE CHA MSINGI CHAGUA MMOJA TU HAPO MAAN HUNA NAMNA π€π ME NIKADAKIA NIKASEMA KABLA HAJACHAGUA ME NAOMBA TU ANIPE NAULI NIONDOKE COZ SIWEZI KUWA NA MTU MWENYE TABIA K**A ZAKE AKAKATAAGA SI AKAMPIGIA NDUGU YAKE HV AJE AMTOE HUYO DADA MAAN MPKA USIKU ULIINGIA YULE DADA ALIKUA BADO KAKAA PALE TU ππππ
MIMI NILIPOONA HATOKI IKANIBIDI NITOKE NIKAWA NAPUNGA UPEPO NJE NAJIZUNGUSHA NJIAN NAENDA NARUDI NAENDA NARUDI SAM NAE AKAJA SIJUI ALIJUAGA NIMEENDA KUJIUA AKANIBEMBELEZAAA WEEEE ME NIKAKUBARI KURUDI YULE DADA NAE AKAAMBIWA NENDA NYUMBANI USIKU UMEINGIA NDO AKATOKAGA PALE NA MIKWALA K**A YOTE π€£π€£π€£
SASA SIJUI NINGEAMBIWAGA MIMI NDO NIRUDI SIJUI INGEKUAJE NA NYUMBANI NILITOROKAGAA ILA TULISOLVE SAM AKANAMBIAGA NIMPELEKE HOME TUKAENDAGA MPAKA HOME AKAJITAMBULISHA TUKAENDELEA NA MAHUSIANO MPKA TULIPOKUAJA KUCHOKANA KILA MTU AKAFATA NJIA YAKE ππππ KINA SAM AISEEEE WAPUUZI SANA ASIKWAMBIE MTU
~Mdada wa Mbaliπ
02/09/2026
01/09/2026
30/08/2026
28/08/2026
27/08/2026
26/08/2026
25/08/2026