03/10/2025
Leo tutakua na mechi ya kirafiki MwaBan sports legends vs Wanafunzi Mwadobana secondary, muda wa saa kumi jioni katika Viwanja vya shule ya msingi Mwadobana, karibuni sana 03/10/2025
MwaBan Sports Legends unites veteran athletes and public servants from Mwadobana & Banemhi. Est. 2022.
We promote football, netball & athletics for health, unity, and lifelong sports passion.
03/10/2025
Leo tutakua na mechi ya kirafiki MwaBan sports legends vs Wanafunzi Mwadobana secondary, muda wa saa kumi jioni katika Viwanja vya shule ya msingi Mwadobana, karibuni sana 03/10/2025
18/09/2025
Ijumaa ya kesho 19/09/2025 sports legends tutakua katika Dimba la Mwadobana primary, burudani inaendelea
11/09/2025
Ni keshoo mapema asubuhi, njoo tuimarishe afya zetu
11/09/2025
Habari za jioni wadau wa MwaBan sports legends.
Kesho Tarehe 12/09/2025 Saa 2:30 asubuhi tutakua na mechi ya Veterans Simba vs Yanga katika Viwanja vya shule ya Msingi Kilabela A.
Karibuni sana.
05/09/2025
Baadhi ya picha za matukio wakati wa uzinduzi wa ya MwaBan sports legends katika uwanja wa Shule ya msingi IKUNGULYANDILI Bariadi
05/09/2025
Leo 05/09/2025 Katika kilele cha uzinduzi wa ya MwaBan , tukio kubwa lililovutia hisia za wengi lilikuwa ni mchezo wa kirafiki wa watani wa jadi– timu ya Simba Veterans dhidi ya Yanga veterans, zikiwa na wachezaji wastaafu na mashabiki mahiri kutoka Kata za Mwadobana na Banemhi*.
Mchezo huo wa heshima ulifanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi IKUNGULYANDILI ukiwa sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha kuanzishwa kwa umoja huo wa michezo mnamo mwaka 2022. Simba, wakiwa na safu ya ushambuliaji iliyopangiliwa kwa ustadi, walifanikiwa kuichapa Yanga mabao matano kwa bila (5-0) katika mchezo uliokuwa wa kuvutia, wa kiungwana na wenye burudani ya hali ya juu.
Ushindi huo wa kihistoria uliwaweka Simba juu kisimba, lakini zaidi uliakisi malengo ya MwaBan Sports Legends – kuleta mshik**ano, burudani, na kuenzi michezo k**a chombo cha umoja na afya.
Mchezo ulihitimishwa kwa uzinduzi rasmi wa ya MwaBan Sports Legends , ikiwakilisha urithi mpya wa michezo katika jamii.
04/09/2025
*Historia ya Umoja wa MwaBan Sports Legends*
Umoja wa *MwaBan Sports Legends* ulianzishwa rasmi mwaka *2022* na waasisi wake wawili: *Mwalimu Sokoine Tumuti Laizer*, ambaye ndiye Mwenyekiti wa kwanza, pamoja na *Mwalimu Sirili Asenga* (Katibu). Wazo kuu lilikuwa ni kuwaunganisha *watumishi wapenda michezo* katika Kata ya *Mwadobana*, wakijikita zaidi kwenye michezo ya *mpira wa miguu (football)*, *mpira wa pete (netball)* na *jogging* kwa ajili ya afya na kuendeleza mshik**ano kazini.
Umoja huu ulianza k**a kikundi kidogo cha watu wachache waliokuwa na mapenzi ya dhati kwa michezo, lakini baadaye *uliungana rasmi na watumishi wenzetu kutoka Kata ya Banemhi*, na hivyo kuzaliwa kwa jina la pamoja *“MwaBan Sports Legends”*, likiwa ni kifupisho cha *Mwadobana na Banemhi*.
Tangu kuanzishwa kwake, Umoja huu umeendelea kustawi na kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo katika ngazi ya kata na tarafa, . Mbali na michezo, umoja huu pia umejikita katika kuimarisha afya, mshik**ano kazini, na kuhamasisha ushiriki wa watumishi katika shughuli za kijamii.
Ifikapo *November *2025*, Umoja huu utakuwa umetimiza *miaka minne* ya kuenzi michezo, afya bora, na mshik**ano wa kikazi. Hii ni ishara kuwa michezo ni zaidi ya burudani – ni chombo cha kuunganisha watu na kuimarisha jamii.
*Kauli mbiu yetu:*
*“Tunakumbuka tulikotoka, tunajenga tunakokwenda – kupitia michezo.”*