22/07/2026
Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo hii kuelekea nchini Rwanda kwaajili ya kushiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup.
Simba imepangwa kundi B katika mashindano hayo, pamoja na Mogadishu City Club ya Somalia 🇸🇴, Jamus FC ya Sudan Kusini 🇸🇸 na Singida BS ya Tanzania 🇹🇿.
Mchezo wetu wa kwanza utapigwa Julai 25 majira ya saa 12 jioni dhidi ya Mogadishu CC.
22/07/2026
🚨OFFICIAL Phil Foden amesaini mkataba mpya na Manchester City ambao utamuweka klabuni hadi majira ya joto ya mwaka 2030.
🗣️ Foden: "Kuichezea klabu hii ndio kitu pekee ambacho nimekuwa nikikitamani maisha yangu yote, na ni heshima kubwa kila mara kuvaa jezi yake... nanifuraha sana kufanya tena kazi na Enzo Maresca."
22/07/2026
Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji amekutana na kufanya mazungumzo na wachezaji wapya watatu ambao tayari wametambulishwa Kelvin Nashon, Nathaniel Chilambo na Bakari Msimu.
Mo Dewji amewakaribisha wachezaji hao kwenye familia ya Simba na kuwaeleza malengo ya Simba ya ndani na kimataifa na hivyo kuwataka kujituma wakati wote wanapokuwa kwenye majukumu ya kuipambania nembo ya klabu.
Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori alikuwepo pia katika kikao hicho.
22/07/2026
Rais wa Yanga SC, Hersi Said amelikaribisha rasmi jopo linalounda benchi jipya la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Kocha Mkuu Mangoba Mngqithi.
22/07/2026
Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji na Mwenyekiti wa Klabu na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu mipango ya timu kuelekea msimu wa 2026/27.
22/07/2026
Mshambuliaji hatari, Seleman Mwalimu ataendelea kuitumikia Simba SC kwa msimu mwingine wa 2026/27 baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kutoka Wydad Casablanca 🇲🇦.
Msimu uliopita Mwalimu alifunga mabao tisa (9) katika ligi kuu ya Tanzania (NBC Premier League).
22/07/2026
Klabu ya Young Africans imemtambulisha beki wa kati, Mohamed M***a baada ya kukamilisha uhamisho wake akitokea Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma.
Mohamed 22, amesaini mkataba wa miaka miwili na sasa anatua kwenye kikosi cha Wananchi kuimarisha safu ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa 2026/27.
22/07/2026
Mwamuzi wa soka wa Uingereza, Anthony Taylor, ametangaza kustaafu uamuzi baada ya miaka 20 katika taaluma hiyo.
Amesema kuwa shinikizo kubwa pamoja na matusi ya mara kwa mara aliyokuwa akipokea yamechangia kuharakisha uamuzi wake wa kuachana na kazi hiyo.
Taylor mwenye umri wa miaka 47 ni miongoni mwa waamuzi mashuhuri zaidi katika soka la kimataifa. Katika kipindi cha kazi yake, amechezesha jumla ya mechi 831, zikiwemo 432 za Premier League.
Mbali na mechi za ligi, Taylor pia ameongoza michezo katika mashindano makubwa duniani, ikiwemo UEFA European Championship na kombe la Dunia.
Akizungumza kuhusu uamuzi wake, amesema anajivunia mafanikio aliyopata katika kipindi chake cha uamuzi, lakini mazingira ya shinikizo na ukosoaji mkali dhidi ya waamuzi yalimfanya aone kuwa wakati wa kuhitimisha safari yake umefika.
Kuondoka kwa Anthony Taylor kunahitimisha safari ya mmoja wa waamuzi waliotambulika zaidi katika soka la kisasa, baada ya kusimamia baadhi ya mechi muhimu zaidi katika mchezo huo duniani.