Score Shayo

Website

Score Shayo ScoreShayo/Breaking News | Transfers | Results

Arsenal imeamua kuendelea na Mikel Arteta k**a sehemu muhimu ya mradi wake wa muda mrefu, baada ya klabu hiyo kuthibitis...
07/10/2026

Arsenal imeamua kuendelea na Mikel Arteta k**a sehemu muhimu ya mradi wake wa muda mrefu, baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa kocha huyo amesaini nyongeza ya mkataba wa miaka minne, utakaomuweka Emirates hadi Juni 2030.

Arteta, ambaye alijiunga na Arsenal mwezi Desemba 2019, sasa anaelekea kutimiza zaidi ya muongo mmoja akiwa katika nafasi ya kocha mkuu wa klabu hiyo. Uamu*i huu unaonyesha wazi namna uongozi wa Arsenal unavyotazama kazi yake na mwelekeo wa timu kwa miaka ijayo.

Kwa mtazamo wa kiufundi, kuendelea na Arteta kunaipa Arsenal nafasi ya kujenga timu ikiwa na mwendelezo wa falsafa moja. Kocha huyo amekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya kikosi, mfumo wa uchezaji na ushindani wa Arsenal katika michuano mikubwa.

Uongozi wa klabu hiyo umeamua kumuongezea mkataba ukizingatia mafanikio ambayo Arsenal imeyapata katika kipindi cha hivi karibuni, ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2025/26 na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huo huo.

Mkataba mpya pia unatajwa kuja na nyongeza kubwa ya mshahara, jambo litakalomuweka Arteta miongoni mwa makocha wanaolipwa zaidi duniani na anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu England.

Kwa Arsenal, hii siyo tu taarifa ya kuongeza mkataba wa kocha. Ni ishara kwamba klabu imeamua kuendelea na mradi uleule, ikiamini kwamba Arteta bado ana nafasi ya kuifikisha timu katika hatua nyingine ya ushindani wa ndani na Ulaya.

 Ally, Afisa habari klabu ya Simba Sports, ameeleza kwa kina namna maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Young Africans. aki...
07/10/2026

Ally, Afisa habari klabu ya Simba Sports, ameeleza kwa kina namna maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Young Africans. akisema kuwa kwa sasa hakuna mchezaji mwenye tatizo lolote, wachezaji wote wako vizuri.

Zipo fununu nyingi kuhusu Libasse Gueye, sijui ameumia, ni watu wanaotaka kuleta taharuki kwa mashabiki wa Simba. Niwatangazie tu Wanasimba kwamba Libasse Gueye yuko salama, hajaumia hata ukucha na yuko tayari kwa ajili ya mapambano ya mwezi Oktoba.

๐ŸŽ‚๐Ÿ’š LEO NI KUMBUKIZI YA KUZALIWA YA GWIJI WETU WA ZAMANI, JERSON TEGETE! ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟโšฝ๏ธJerson Tegete ni miongoni mwa washambuliaji ...
07/10/2026

๐ŸŽ‚๐Ÿ’š LEO NI KUMBUKIZI YA KUZALIWA YA GWIJI WETU WA ZAMANI, JERSON TEGETE! ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟโšฝ๏ธ

Jerson Tegete ni miongoni mwa washambuliaji waliowahi kuandika historia ndani ya Young Africans (Yanga) na kubaki kwenye kumbukumbu za mashabiki wa klabu hiyo. ๐Ÿ’š

Tegete alisajiliwa na Yanga akitokea katika kikosi cha Taifa Stars, tofauti na wachezaji wengine ambao husajiliwa kutokea katika vilabu vya Ligi Kuu. Uwezo wake akiwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ulimfanya Yanga kuona thamani yake na kumpa nafasi ya kuvaa jezi ya kijani na njano.

Akiwa Yanga, Tegete alionyesha uwezo wake kupitia nguvu, kasi, ufundi wa kufunga na kutumia vizuri nafasi akiwa ndani ya eneo la hatari. Alikuwa mshambuliaji ambaye mabeki walipaswa kuwa makini naye kila alipokuwa uwanjani. ๐Ÿ”ฅ

Moja ya sehemu zilizomfanya akumbukwe zaidi ni Kariakoo Derby, ambako aliwahi kuwa mwiba kwa Simba, akifunga mabao matano dhidi ya wapinzani hao katika kipindi chake akiwa Yanga. โšฝ๏ธ๐Ÿ”ฅ

Tegete pia aliwahi kuwa sehemu ya Taifa Stars, akibeba uzoefu wake kutoka Yanga na kuendelea kulitumikia taifa kwenye michezo ya kimataifa. ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Leo, tunapomkumbuka katika siku yake ya kuzaliwa, tunakumbuka pia mchango wake, mabao yake na nyakati alizowapa furaha mashabiki wa Yanga. ๐Ÿ’š๐Ÿ‘๐Ÿฝ

๐ŸŽ‚ Heri ya kumbukizi ya kuzaliwa, Jerson Tegete!

๐Ÿ’šโšฝ๏ธ Jina lako limebaki kwenye historia ya Yanga.

Young Africans imefunga makubaliano na mchezaji wake, beki wa kulia  Mwenda, baada ya kutoelewana kwa muda na klabu yake...
07/10/2026

Young Africans imefunga makubaliano na mchezaji wake, beki wa kulia Mwenda, baada ya kutoelewana kwa muda na klabu yake. Sasa atarejea tena kambini kuendelea kuipa huduma k**a kawaida.

Kwa sasa, jukumu lililobaki kwa mchezaji huyo ni kusubiri malipo yake, ikiwemo mishahara, kisha atarejea kambini muda wowote kuanzia sasa.

OFFICIAL || Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno,  Ronaldo, anakabiliwa na kosa la kuondoka kambini bila kupata ruhusa kut...
07/10/2026

OFFICIAL || Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo, anakabiliwa na kosa la kuondoka kambini bila kupata ruhusa kutoka kwa viongozi wa ndani ya timu ya taifa.

Cristiano Ronaldo anaweza kukabiliwa na kusimamishwa kuichezea timu ya taifa ya Ureno kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi sita, pamoja na faini ya โ‚ฌ500 hadi โ‚ฌ1,000.

07/10/2026

Unaikumbuka historia ya Kariakoo Derby ya mnamo mwaka 1997, ambapo mchezaji wa klabu ya Simba Sports, Abdallah Kibadeni, alikuwa akitumikia klabu hiyo kwa jezi nambari 10.

Abdallah @โ€œKingโ€ Kibadeni alijiunga na klabu ya Simba Sports mnamo mwaka 1970 baada ya awali kufanya mazoezi na Yanga lakini hakupata nafasi ya kusajiliwa. namba aliyopewa ilimpa nguvu na jina kubwa na kuonekana ni mchezaji hatari sana.

mchezaji huyo aliandika historia ndefu sana ndani ya soka la Tanzania na pia mpaka leo tunasema haijawahi kutokea mchezaji yoyote ambaye ameweka rekodi nzuri k**a .

pia Simba Sports mnamo mwaka 1974 alipata nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika. na katika kikosi hicho jezi namba 10, Abdallah โ€œKingโ€ Kibadeni alikuwa mmoja wa wachezaji wakubwa ambao walipasi katika michuano hiyo.

mnamo mwaka 19 Julai 1977, Simba iliifunga Yanga 6โ€“0, na Kibadeni akafunga hat-trickโ€”mabao matatu katika mchezo huo. Rekodi hiyo imetajwa kuwa bado haijavunjwa katika Kariakoo Derby. historia hii ilitunzwa na kuheshimiwa zaidi nchini Tanzania katika mchezo wa Kariakoo Derby.

sasa tunahitaji kuona kitu kizuri ndani ya tarehe 10. mchezo mkali sana Simba SC dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC wakifanya vizuri angalau apatikane mchezaji mmoja wa timu zote mbili ambaye anaweza kuweka rekodi yake juu ya Derby hii k**a ilivyowekwa na mchezaji wa zamani โ€œKingโ€. utakuwa mchezo mzuri k**a tutashuhudia jambo hilo likitokea tena kwa mara nyingine.

07/10/2026

BREAKING || RONALDO BADO YUKO TAYARI KWA URENO ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น๐Ÿ”ฅ

Kupitia vyombo vya habari nchini Ulaya, inaelezwa kuwa nyota wa timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo, amefafanua kuwa hajatoa kauli yoyote rasmi kuhusu kumaliza au kuendelea na maisha yake ya soka katika timu ya taifa.

Ronaldo bado yuko tayari kuichezea Ureno katika dirisha lijalo la kimataifa la mwezi Novemba.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Ronaldo inayosema ameamua kustaafu au kuachana na timu yake ya taifa. Badala yake, nyota huyo anaendelea kuwa available kwa Ureno, huku uwepo wake kwenye kikosi cha taifa ukiendelea kuwa wazi.

Kwa kifupi, Ronaldo bado hajafunga mlango wa Ureno. ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น๐Ÿ

kitu kilicho washangaza wengi kwenye mchezo wa Argentina dhidi ya Benin. ni kuwa Mwamu*i alimkabidhi Messi kadi nyekundu...
07/10/2026

kitu kilicho washangaza wengi kwenye mchezo wa Argentina dhidi ya Benin. ni kuwa Mwamu*i alimkabidhi Messi kadi nyekundu na ya njano baada ya filimbi ya mwisho, k**a kumbukumbu ya mchezo wake wa mwisho akiwa na Argentina.

sio kwamba mwamu*i alitoa kadi kwa makosa ya mchezaji, hapana ila alitoa kadi k**a kumbukumbu ambayo Messi ataikumbuka pia na mwamu*i mwenye furaha yake ni kutoa kadi kwa mchezaji mkubwa ๐Ÿ‘€๐Ÿ˜‚

imani yangu ni kwamba asilimia 90 ya mashabiki wa timu ya Argentina pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni kote wako ma...
06/10/2026

imani yangu ni kwamba asilimia 90 ya mashabiki wa timu ya Argentina pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni kote wako macho na wako tayari kushuhudia mchezo huu dhidi ya Benin. lengo la mashabiki kusubiri mchezo huo ni kushuhudia mchezaji bora duniani Lionel Messi ambaye atacheza mchezo wake wa mwisho akiwa na u*i wa timu yake ya taifa.

Address

Bunda
31501

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Score Shayo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share