Rebooting has Completed Sasa tumerudi hewani.
Kaa tayari.
Chelsea Headquarters Tz
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Chelsea Headquarters Tz, Sports Event, kendricklaneez@gmail. com, Dar es Salaam.
27/08/2024
The Bluez remember the name.
Neto+Felix=
NetFlix
Back2Business
16/11/2021
We are Roman empire
07/07/2021
⚽️FOOTBALL BUILDUP:
...........................................
The Playmaker:
-Ni yule mchezaji ambaye ana control mchezo mzima kwa timu husika offensively playing. Mara nyingi anahusika katika kusambaza mipira kila eneo la uwanja kwa mijongeo ya pass zake zinazopelekea kutengeneza nafasi za magoli.
Playmaker anaibeba timu kupitia vision, ufundi/ ujuzi, ball control yake, ubunifu (creativity), passing ability, maamuzi sahihi (decisive).
Ipi position ya Playmaker?, mara nyingi tumeona kwamba wale centre midfielders ndio huwa wanakuwa playmakers kwenye timu zao maana wao ndio huchukua game.
Hapa kuna attacking midfielders ,wao hucheza zaidi kwenye upper zone wanakaa katikati ya viungo (CM) na washambuliaji (forwards) wanakuwa free role, hujulikana k**a advanced playmaker (Trequartista kwa lugha ya kiitaliano) wanacheza kwenye position ya no.10.
Aina hii ya play maker anaweza kusit katikati ya dimba au akatokea pembeni. Huyu anaichezesha timu akitokea eneo hilo kwa kupiga pass sahihi kuwafikia washambuliaji ama pembeni kwa mawinga,atapiga cross,atatengeneza nafasi za magoli (assists, key passes) na kufunga magoli, atahold Possession on Opponents half kwenye ⅓ ya mwisho ya uwanja.
Playmakers hawa ni highly technical skills, na very tactical intelligence, wapo chapu na wanajua kutembea na mpira, ni wenye vision ya hali ya juu na wana uwezo mzuri wa kushuti, kupiga crosses, kuassist, kupass, kudribble, kufunga na kuanzisha mashambulizi, kutengeneza nafasi za magoli, playmakers wengi wa aina hii ni wazuri kwenye mipira iliyokufa (set pieces) penalt, free kicks, corner, kiufupi ni dead ball specialist. Playmakers hawa mara nyingi wanafiti kwenye mfumo wa 433, 343. Lionel Messi, Eden Hazard, Maradona, Dinho, KDB, ni mfano wa advanced playmakers.
Kuna aina nyingine hii ya playmaker "Deep lying playmaker" huitwa Rejesta kiitaliano. Hawa jukumu lao kuu ni kuchezesha timu kuanzia dimba chini (deep position), wanacheza nyuma kidogo ya mstari wa viungo wa kati na wanaonekana kuwa ni defensive midfielders (holding defensive midfielder) kwani hucheza juu kidogo ya mstari wa ulinzi (defensive line), wanatumia eneo hilo lenye space kuichezea timu nzima kwa pasi ndefu na fupi, hawa hawashambulii kwenda langoni wao wanaituliza timu na kukeep possession from the deep possession. Huwezi kuwaona wakiassist sana ama kufunga.
Deep lying playmaker ni technical, visionable, na wana uwezo mkubwa wa kupiga pass. Wanafahamika zaidi kutokana na uwezo wao wa kupiga pasi ndefu zenye kuvuka mstari wa viungo na mabeki kwenda kwenye forward line. Playmaker wa aina hii pia ni wazuri kwenye tackles na Interceptions. Wanacheza kwenye position ya no.6/8. Aina hii ya playmakers wanafaa kwenye mfumo wa 4231,3421,4141,4123. Andrea Pirlo na Jorginho ni mfano wa deep lying playmaker,
Playmaker sio lazima atokee eneo la midfielder, play maker anaweza kutokea eneo la pembeni akicheza k**a winga, pia anaweza kuwa CF. Kinacho define uplaymaker ni technical ability, good ball control, holding possession (umiliki), game balacing, dribbling skills, good passing ability, anaifanya timu icheze kwa kuunganisha team members kufanya shambulio.
Kuna tofauti ya kimajukumu inayotofautisha kati ya midfielders na playmakers.
Midfielder huwa analimitiwa na position yake, anacheza eneo husika kwenye pitch iwe nyuma ya washambuliaji ama eneo la mbele la mabeki. Wakati Playmaker ni yule mchezaji mwenye uwezo wake binafsi, ikiwa na maana kwamba playmaking ni ule ubora wa mchezaji binafsi (individual quality). Playmaker anaplan mchezo mzima kwa vision na passing ability yake na kutengeneza nafasi kwa wengine kuattack.
Playmaker anahitaji kuwa na skills zifuatazo:
Passing skills ( pass ndefu na fupi).
Ball control skills, uwezo mzuri wa kukaa na kutembea na mpira.
Dribbling skills, uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira mguuni.
Off the ball position intelligence, ufahamu wa kukaa eneo sahihi wakati akiwa hana mpira.
1v2 Possession, playmaker anatakiwa awe mzuri pale ambapo kunakuwa hakuna nafasi nyingine inabidi awe na uwezo wa kuwatoka wapinzani...
The switch up, awe mzuri kwenye suala la kubadilisha upande kutoka eneo moja la uwanja hadi mwingine..
Technical and Ball control + vision, ajue kuisaidia timu kwa kuwachezesha team members kwa kuwapush kwenda mbele kufanya shambulizi.
Kwa maana hiyo pale Chelsea FC tuna deep lying playmaker type kutokana na mfumo unaotumika wa 3421, Jorginho ndiye controler akichezesha timu kuanzia eneo la dimba la chini.
Hakim Ziyech pia ni play maker mzuri hasa alipokuwa akicheza Ajax, ila kwa pale CFC hajapewa majukumu hayo labda kutokana na mfumo uliopo.
Pia timu inaweza kucheza na multiple playmakers, kucheza na playmaker zaidi ya mmoja kunaifanya timu iwe hatari zaidi.
07/07/2021
Back to work
07/07/2021
Maurizio Sarri;
"Nilifanya makosa. Sikutakiwa kuondoka Chelsea. Lakini nilitaka kurejea Italia, ni kosa nililolifanya kutokana na maamuzi yangu."
"Marina Granovskaia alitaka niendele kubaki. Lakini leo nakiri kabisa lilikuwa kosa kubwa sana kutamani kurudi Italia kwa gharama yeyote."
Kwasasa Maurizio Sarri ni kocha wa Lazio ya nchini kwao Italia.
07/07/2021
Wanafunzi wapya ndani ya Chelsea FC Academy. The Class of 2021.
- Midfielder (attacking midfielder/box to box midfielder), amejiunga na Chelsea U15 akitokea AFC Wimbledon. Anatengeneza nafasi na ni fundi wa kuzifumania nyavu..
- Huyu amejiunga na Chelsea U13 akitokea kitaani kwao huko Cambridge United . Ni Foward huyu na anaweza kucheza akitokea upande wa kushoto ama centre na ana jicho la goli.
- Huyu ni centre midfielder left footer anauwezo pia wakucheza k**a box to box midfielder na anaweza kuoperate kila upande wa uwanja. Ni U18.
- Huyu dogo ni mlinzi wa kati (centre defender) anaweza kutumikia pia k**a beki wa pembeni (fullback) au akacheza centre midfielder coz ji versatile. Amekulia Chelsea huyu tangu akiwa na umri wa miaka 8, now yupo U18 team.
- Tudo ni Mshambuliaji anayetumia guu la shoto, anaweza kucheza as a centre midfielder pia. Alkiwepo CFC CFC tangu akiwa na miaka 9. Huyu dogo anasema chuo kimoja pale Eton College anasomea masomo ya Kiingereza, Kilatini, Kigiriki, Kijerumani, Hesabu na Fizikia..
- Mlinzi wa kulia (Right defender), anauwezo mkubwa wa kupanda na kushuka yaani kushambulia na kuzuia ata the sametime. U18.
- Kiungo cha kati (CM), dogo anaufundi mwingi na ulewa wa game. U16.
- Ni Mshambuliaji anayeweza kucheza kwenye position tofauti. U18.
- Ni Foward aliyejiunga na Chelsea baada ya kuondoka West Ham, anapendelea sana kufunga huyu. U18.
- Billy ni centre midfielder ndio position anayoimudu lakini pia anaweza kudrop kwenye defensive line kusaidia kudefence. Unaambiwa dogo ni talented ana ufundi mguuni.
Kila la kheri boys vipaji vyenu vikawe vyenye kustawi..
Am back blues fans
31/03/2021
YUPI TUTAFANIKIWA KUINASA SAINI YAKE NA NANI UNADHANI ANATUFAA ZAIDI?
👤Erling Haaland ⬅️Borrusia Dortmund.
👤Romelu Lukaku ⬅️Inter Milan.
👤Gabriel Menino ⬅️Palmeiras.
👤Ibrahim Konate ⬅️RB Leipzig.
👤Eduardo Camavinga ⬅️Rennes.
👤Jesus Corona ⬅️FC Porto.
👤Paul Dyabala ⬅️Juventus.
👤Nicklas Sule ⬅️Bayern Munich.
👤David Alaba ⬅️Bayern Munich.
👤Sergio Agüero ⬅️Manchester City.
👤Martin Ødegaard ⬅️Real Madrid.
👤Eden Hazard ⬅️Real Madrid.
👤Giannluigi Donnaruma ⬅️AC Milan.
31/03/2021
UEFA imethibitsha kuwa mechi zote mbili za robo fainali ya UEFA Champions League FC Porto vs Chelsea FC/Chelsea FC vs FC Porto zitachezwa kwenye uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan huko Seville Hispania
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Culinary Team
Attire
Contact the business
Website
Address
Dar Es Salaam
255