22/07/2026
πΉπΏ KARIBU TPC! πΉπΏ
Tunayo furaha kubwa kumkaribisha Coach Bahati Mgunda k**a Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Tanzania Paralympic Committee (TPC).
Coach Bahati analeta uzoefu mkubwa katika maendeleo ya michezo ya watu wenye ulemavu, akiwa na weledi katika ukocha, ujenzi wa uwezo wa wanamichezo na makocha, pamoja na kuhamasisha ushiriki jumuishi kupitia michezo.
Tunaamini mchango wake utaendelea kuimarisha safari ya kukuza na kuinua michezo ya Paralimpiki nchini Tanzania, huku tukiwajengea wanamichezo wetu mazingira bora ya kufikia mafanikio ya kitaifa na kimataifa.
Karibu sana Coach Bahati Mgunda!
Pamoja tutaendelea kujenga Tanzania yenye usawa, fursa na mafanikio kupitia michezo.
π² Follow us:
15/07/2026
Karibu sana Coach Innocent Maseke Jonas kwenye Kamati ya Ufundi ya TPC.
07/07/2026
Habari njema kwa wadau wote wa michezo!
Mafunzo ya Ukocha na Uamuzi (Coaching and Officiating) ya Para Volleyball sasa yatafanyika rasmi kuanzia tarehe 09.07.2026 hadi 13.07.2026 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Hii ni fursa ya kipekee ya kujifunza, kuongeza ujuzi, na kuunga mkono harakati za kukuza michezo ya watu wenye ulemavu nchini. Wadau wote mnakaribishwa sana mje tushirikiane kusukuma mbele gurudumu hili!
Weka alama kwenye kalenda yako, usipange kukosa!
30/06/2026
Karibu Ndani ya Familia ya TPC, Dr. Janeth Mlay!
Mstari wa mbele kuelekea mafanikio mapya unazidi kuimarika! Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) tunafarijika na kufurahia sana kukukaribisha Dr. Janeth Mlay katika familia hii kubwa ya Para-Sports ukiwa ni Mkurugenzi wa ufundi na mjumbe wa k**ati ya utendaji ya TPC..
Tunaamini kwa pamoja tutaandika historia mpya ya mafanikio, kuibua vipaji, na kuweka viwango vya juu vya kiutendaji na kiufundi katika michezo ya watu wenye ulemavu nchini.
Kazi ndio kwanza inaanza! Letβs make history together! ππ₯
PamojaTunaweza
29/06/2026
SAVE THE DATE! ποΈπββοΈπΉπΏ
Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) ikishirikiana na Tanzania Para Swimming Association (TPSA) inakuletea Tanzania National Para Swimming TALENT Identification Gala
Hii ni fursa ya dhahabu ya kuibua na kukuza vipaji vya waogeleaji wenye ulemavu nchini, kuelekea maandalizi ya mashindano makubwa ikiwemo LA 2028!
Usipitwe na tukio hili kubwa la kihistoria. Endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa zaidi za jinsi ya kushiriki na kujisajili!
22/06/2026
Chama cha Sitting Volleyball kinaendesha mafunzo maalum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hii ni fursa ya kipekee kwa wote wenye nia na shauku ya kuendeleza mchezo wa Paravolley nchini!
Michezo ya watu wenye ulemavu inahitaji nguvu yetu sasa hivi. Ni wakati wetu wa kuamka, kuwajibika, na kuonyesha uwezo wetu.
Tarehe: 24 - 28 Mahali: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Usikae pembeni! Jiunge nasi sasa tufanye mapinduzi kwenye Paravolley. Karibuni wote! ππ₯
18/06/2026
UONGOZI MPYA: KARIBU KATIBU MKUU! π
Tunapenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Ndugu Ramadhan Namkoveka kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Utendaji ya Tanzania Paralympic Committee (TPC).
Udumu katika kuiongoza michezo ya walemavu na kuifikisha katika kilele cha mafanikio nchini na kimataifa. Kila la heri katika majukumu haya mapya ya kujenga na kuendeleza vipaji!