KwetuHabari

KwetuHabari

Share

Media
Breaking news|Current news|Sports|entertainment. We will Update you 24/7

05/12/2025
30/11/2025
26/11/2025

📌VIDEO

Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba akiwajibu wanaharakati wa mitandao wanaosema anaweza kuwa Waziri Mkuu atakayekaa kaa muda mfupi madarakani.

26/11/2025

📌VIDEO:

Washirika wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Joseph Gwajima wakifanya usafi baada ya kuruhusiwa Serikali kuendelea kufanya ibada.

26/11/2025

📌VIDEO:

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaanza kutekeleza mradi wa kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwa wananchi kupitia miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na wakala kote nchini.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma Novemba 25, 2025 wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba na Menejimenti ya REA kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na REA.

21/11/2025

VIDEO:

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amelaani vikali tabia ya baadhi ya watu kueneza taarifa za uongo na zisizofanyiwa uchunguzi, akisema hatua hiyo imefika kiwango cha kuwaumiza na kuwavuruga wananchi.

Photos from KwetuHabari's post 22/09/2025

🆕️
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkwawa, ambaye pia ni Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Mkwawa Rally of Tanzania yanayohusiana na kalenda ya African Rally Championship (ARC) Ahmed Huwel Mkwawa, ameweka wazi dhamira yake ya kukuza na kuendeleza vipaji vya madereva chipukizi wa mbio za magari hapa nchini.

Huwel amesema lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa na hatimaye kuliletea taifa heshima na ushindi.

Akizungumza mkoani Morogoro wakati wa kufunga mashindano hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu, Ahmed amesema kuwa, Tanzania imebarikiwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji ambao wakipewa nafasi, mafunzo na msaada wa kutosha, wana uwezo mkubwa wa kung'ara kimataifa.

Katika mashindano hayo, Ahmed pia ameshiriki na kuibuka mshindi wa tatu, jambo lililoonyesha dhamira yake sio tu k**a mdhamini bali pia k**a mshiriki mwenye uwezo mkubwa.

Ahmed ameongeza kuwa yeye pamoja na makampuni yake wako tayari kushirikiana na vijana wanaoonyesha vipaji katika mchezo wa mbio za magari, kwa kuwapatia mafunzo, vifaa na kuwafungulia fursa za kushiriki mashindano mbalimbali huku akitoa wito kwa taasisi za serikali, mashirika binafsi, kampuni na wadau wengine wa michezo kuungana katika juhudi hizo ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na mashindano yenye viwango vya juu kimataifa.

Photos from KwetuHabari's post 22/09/2025

🆕️
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameiagiza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Wilaya ya Karatu kuongeza kasi katika mchakato wa kumpata Mkandarasi wa kupeleka Maji kwenye Matenki pamoja na usambazaji wa maji kwa wananchi wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha kutoka kwenye chanzo cha Maji cha Bwawani.

CPA Makalla ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu Septemba 22,2025 Mjini Karatu kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo, akitembelea na kukagua chanzo cha Maji cha Bwawani, Karatu Mjini, Chanzo ambacho kiliharibiwa na Mafuriko ya Mvua na kuathiri upatikanaji wa maji Karatu na hivyo kulazimu serikali kutenga fedha ili kunusuru chanzo hicho cha Maji ambacho kimekuwa tegemeo la uzalishaji maji kwa Mji wa Karatu pamoja na maeneo ya jirani.

Mhe. Makalla pia ameipongeza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Karatu kwa usimamizi mzuri wa utoaji wa huduma za Maji kwenye Wilaya hiyo ambao umefikia asilimia 71 kwasasa, akihimiza Jamii pia kushirikishwa na kupewa elimu katika utunzaji wa vyanzo vya maji vilivyopo kwenye maeneo yao.

"Niwasihi tushirikiane pia na wananchi wa maeneo haya kuona kwamba tunatunza vyanzo vya maji lakini pia na sisi wenyewe k**a Mamlaka ya Maji kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kutokuchafua vyanzo vya maji." Amesisitiza CPA Makalla.

Awali katika taarifa yake, Meneja wa Mamlaka ya Maji Karatu Injinia Steven Siayi, amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa serikali imeshatoa zaidi ya Milioni 145 kwaajili ya kufikisha maji kutoka kwenye chanzo hicho kwenda kwenye tenki la ujazo wa maji Lita 225, 000 na baadae kusambaza Maji kwa wananchi, akisema kisima hicho kilichonusuriwa kina uwezo wa kuzalisha Maji Lita 28,000 kwa saa.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address

Sinza
Dar Es Salaam