06/03/2026
Je, huu ni msimu wa Arsenal wa kumaliza ukame wa Ligi kuu ya Epl?
Usomaji maandishi tu kupunguza gharama za dataChanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Wachezaji wa Arsenal Eze na Hincapie
Maelezo kuhusu taarifa
Author,Ahmed Omar Bahaj
Nafasi,BBC Swahili, Akiripoti kutoka,Nairobi Kenya
4 Machi 2026
Muda wa kusoma: Dakika 3
Kinyang'anyiro cha ligi ya soka ya Premier chazidi kupamba moto
Je, Arsenal ataumaliza mwendo ashinde taji la ligi ya Epl?
Je, huu ni msimu wa Arsenal wa kumaliza ukame wa Ligi kuu ya Epl?
Matumaini ya Arsenal ya kumaliza ukame wa miaka 21 wa kushinda kombe la ligi kuu ya Epl nchini England yamefufuka upya baada ya kuvuna ushindi katika mechi zake mbili zilizopita tena zote za debi la London.
Kwanza Walimtitiga Tottenham 4-1 alafu wakamkaranga Chelsea 2-1 ,zote hizi zikiwa mechi ngumu.
The gunners bado wako kileleni mwa jedwali la EPL wakiwa na alama 64, kwa jumla wanaongoza kwa alama 5, lakini hii baada ya kucheza mechi 29 ikiwa ni mechi moja zaidi ya washindani wao Manchester City walio nyuma yao kwa karibu katika nafasi ya pili wakiwa na alama 59.
Pep Guardiola wa City anasubiri kwa hamu Arsenal ateleze tena tu apoteze alama ,ili ambakure nyama mdomoni, lakini Mikel Arteta na vijana wake ndio mwanzo wamepata ari mpya ya kupambania taji kufa kupona.
Ubashiri wa SUPERCOMPUTER YA Opta unasemaje?
Tovuti mashuhuri ya kimataifa ya uchambuzi YA SUPERCOMPUTER YA OPTA ,inabashiri kuwa nafasi za Arsenal kushinda ligi msimu huu zimepanda kutoka asilimia 82 hadi 88.