11/05/2026
Mdau DM: “Milioni 10 Bora Zingetumika kwa Watoto Yatima!”
Mfanyabiashara na mwanachama wa Club ya YANGA SC, Jennifer Jovin, maarufu k**a NIFFER, ameichangia Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kulipa faini ya Shilingi Milioni 30 iliyotolewa na Bodi ya Ligi, kutokana na kosa la kutotumia vyumba rasmi vya kubadilishia nguo siku ya Kariakoo Derby dhidi ya Mej Isamuyo.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wamesema kwamba bora hiyo milioni moja Niffer angeitumia kuwasaidia watoto yatima, kuwa pesa hizo zingekuwa na manufaa makubwa zaidi kwa jamii.
Je, unakubaliana na maoni ya mdau huyu?
11/05/2026
RAIS DKT SAMIA KUSHIRIKI UAPISHO WA RAIS MUSEVENI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kesho tarehe 12 Mei, 2026, anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Kampala, Uganda kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Uganda uliofanyika tarehe 15 Januari, 2026, Rais Museveni alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.
Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Uganda, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshik**ano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda..
11/05/2026
Ila Wabongo hawana jema 🤣🤣
11/05/2026
MAKAHABA 39 WAKAMATWA NA POLISI
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limefanikiwa kuwatia mbaroni jumla ya watu 39 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya ukahaba. Operesheni hiyo kabambe imefanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja, ikianzia Aprili 14 hadi Mei 11, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha maadili na usalama ndani ya makao makuu ya nchi.
K**anda wa Polisi mkoani Dodoma, Gallus Hyera, amebainisha kuwa watuhumiwa hao walinaswa katika maeneo mbalimbali yanayozunguka jiji la Dodoma, operesheni hiyo ni endelevu na imelenga kurejesha nidhamu na utulivu katika maeneo ya umma ambayo yamekuwa yakitumiwa vibaya.
11/05/2026
Wakenya Wamefanikiwa sana Mitandaoni Siri ni nini✍️
Lillian Reuben
11/05/2026
Rais Macron ameweka saini nchini Kenya 🇰🇪 ya zaidi ya Euro 💶 bilioni moja za uwekezaji kutoka Ufaransa.
11/05/2026
MAITI YAKUTWA DARAJA LA SALENDER POLISI YACHUNGUZA TAARIFA ZA KIFO
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepokea taarifa ya kifo cha mtu ambaye tarehe 11 Mei, 2026 saa 04:30 Asubuhi mwili wake ulikutwa kwenye maji eneo la daraja la Salender Ilala na mwili huo ambao haukuwa na jeraha lolote.
Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wa mwili huo ni wa mtu aitwaye Aisha Miraji mkazi wa Nzasa Temeke ambaye tarehe 10 Mei, 2026 wakati akiwa na wazazi wake anapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili kwa maradhi ambayo kwa muda tofauti tofauti katika miaka mitano yalikuwa yanamsumbua, aliwapotea akiwa eneo hilo la Muhimbili mpaka mwili wake ulipokutwa tarehe na eneo lililotajwa hapo juu.
Wazazi wake marehemu wamezielezea changamoto za kiafya za mtoto wao alizokuwa anazipitia. Hata hivyo Polisi wanachunguza taarifa hiyo.