Kendrick info

Kendrick info

Share

Karibu kwenye ukurasa wetu wa Facebook kwa habari za siasa, burudani, michezo, na matangazo.

Wasiliana nasi kwa WhatsApp: 0792884973 kwa matangazo na maelezo zaidi.📥🤖🤖

06/05/2026

YANGA WANAROHO MBAYA SANA 😆!!

Yanga imemfuta kazi KOCHA wao mkuu Pedro Goncalves bila huruma yoyote baada ya kutovutiwa na kiwango Cha timu Yao .

Yanga bhana hawacheki na wowote ukizingua wanakupa za uso .

03/05/2026

PRESHA YA KUTOSHINDA ISAMUHYO INAWASUMBUA YANGA.

Nimeona viongozi wa Yanga wakiandika na kusema maneno ya hovyo na mabaya juu ya uwanja wa Major General ISAMUHYO.

Ikanikumbusha msimu juzi Yanga walivyokuja pale wakati wa mvua k**a huu wakawa na maneno k**a haya na mechi ikachezwa ikaisha 0-0. Msimu jana mechi ilikuwa kiangazi hakukuwa na maneno na mechi ikaisha tena 0-0. Msimu huu mechi na JKT bado wanaanza na Simba ambao wanakodi kiwanja pale, lakini maneno machafu yameanza.

Mtu anirekebishe, mimi najua mechi ni kesho tarehe 3 Mei, 2026 saa 12:00 jioni au kuna mabadiliko? Yanga wamecheza mazoezi muda wa mechi kikanuni siku 1 kabla ambayo ni leo tarehe 2 Mei 2026, kuna masaa 24 mpaka kufika muda wa mechi, wanalijua hili?

Leo unafanya ukaguzi na kudharau watu wa Club Licensing, unaiita kiwanja cha Major General ISAMUHYO “Zizi la Ng’ombe” ilihali nyinyi miaka 90 hata “Banda la Kuku” hamna..!! What a shame..!

Halafu mazoezi yamefanyika mpaka yameisha ila unasambaza video ya kipande kidogo cha kiwanja ambacho kimetuamisha maji kiasi kidogo sana sio cha kukataza mechi kuchezwa kwa mujibu wa kanuni, msingi wa kufanya mazoezi ni kuyaona hayo mapungufu ili yasiwe mageni siku ya mechi, lakini wanaleta Usimba na Yanga kwenye kiwanja cha JKT na kudharau juhudi za watu wengine walioamua kuutumikia mpira kwa dhati sio maneno ya kilasiku TUTAJENGA UWANJA LAKINI HAKUNA NI BABAISHA BWEGE TU.

Kwangu huu uwanja Yanga hawaupendi tu kwakuwa ni SEHEMU NGUMU kwao, hawajawahi kufunga hata bao tangu waanze kucheza hapa, hizi zingine ni presha tu wanaona k**a kiama kimefika kesho.

Simba ni klabu ambayo ipo katika KLABU 10 BORA Afrika wamekubali kucheza hapa pamoja na umuhimu huo waliokuwa nao, hawajawahi kukebehi jitihada hizi za JKT Tanzania kujenga huu uwanja, k**a wanakubali klabu hii KUBWA TANZANIA NA AFRIKA kwa ubora, nani tena anajipa umuhimu kuizidi Simba SC hapa Tanzania?

Nakumbusha tena, mechi ni kesho saa 12:00 jioni, kuna muda mrefu sana, mezeni maneno yenu kuweni na subra, sifa ya uongozi ni pamoja na subra, mngesubiri hata siku ya mechi ifike mchana mchana au jioni ndo mseme hivi.

AMEANDIKA JEMEDARI SAID KAZUMARI.

WANANCHI mnasemaje hapa?

02/05/2026

"Nadhani tukijitazama kwa uhalisia, baada ya mchezo wa kesho tutakuwa ama tumepunguza tofauti hadi pointi mbili, au tano, au zitakuwa nane

Tukipoteza na kubaki nyuma kwa pointi nane, naamini itakuwa ngumu sana kufikia malengo yetu, kwa sababu sioni Yanga wakipoteza pointi nyingi kiasi hicho."

🗣STEVE BARKER, Kocha Mkuu wa Simba SC

29/04/2026

Afisa Habari wa Young Africans (Yanga SC), Ali Kamwe, amewatuliza mashabiki wa klabu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Muungano Cup dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC. Katika ujumbe wake wa "Alhamdulillah," Kamwe amekiri kuwa haukuwa usiku mzuri kwa Wananchi kuona taji hilo likienda kwa mtani, lakini amesisitiza kuwa matokeo hayo ni sehemu ya mchezo wa mpira wa miguu. Ameitaka klabu hiyo kutumia muda huu kutafakari na kujipanga upya kwa ajili ya vita kubwa zaidi inayofuata katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC.

​Ali Kamwe ameweka wazi kuwa lengo kuu la Yanga sasa limehamia kwenye kutafuta alama tatu muhimu katika mchezo wao ujao wa dabi ya Ligi Kuu dhidi ya Simba, akidai kuwa alama hizo zina uzito mkubwa zaidi kwa sasa kuliko kitu kingine chochote. Alinukuliwa akisema:

​"Sio usiku mzuri kwetu Wananchi, Tumepoteza Fainali ya Muungano mbele ya Mtani wetu. Sio muda wa kuumia sana na kusikitika. It’s a part of Football. Tutumie muda huu kutafakari na kujiandaa kwa nguvu kubwa kwenye mechi ya Ligi Kuu... POINTI 3 Za Ligi Kuu mbele ya Mtani ni Muhimu sana kwa sasa kuliko kitu chochote kile."

​Kauli hii ya Kamwe inaashiria kuwa Yanga imeshageuza ukurasa na kuelekeza nguvu zote kwenye kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu, huku wakipanga kulipiza kisasi cha kupoteza fainali hiyo ya Zanzibar pindi watakapokutana tena kwenye ligi.

29/04/2026

Ila Simba 😅😅

29/04/2026

Kikosi cha mnyama

Tupe utabiri wako

27/04/2026

Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC inayotarajiwa kupigwa Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, itaamuliwa na waamuzi kutoka Morocco 🇲🇦.

Shirikisho la Soka Tanzania limewasilisha ombi rasmi kwa Shirikisho la Soka la Morocco ili kupata waamuzi hao kwa ajili ya mchezo huo mkubwa wa Ligi Kuu NBC.

Waamuzi waliopangwa ni:
Hamza El Faruq — Refa wa kati
Lahsene Azkawi — Msaidizi wa kwanza
Hamza El Nasri — Msaidizi wa pili
Mostafa Kchaaf — Mwamuzi wa akiba (Fourth Official)

21/04/2026

"Klabu ya Simba bado hawajachagua uwanja wa dabi ya Mei 3" Clifford Ndimbo Afisa Habari wa TFF akiongea na PMTV

Ikumbukwe Dimba SC ndo mwenyeji wa mchezo huo na uwanja wao wa nyumbani Mej Isamhuyo uliopo Bunju na baadhi ya mashabiki wanataka kikapigwe huko kwasababu ndo uwanja wao wa nyumbani😁

Mara ya mwisho Yanga walipeleka mechi Zanzibar kule Gwantanamo kitu ambacho mashabiki wengi wa soka na wa Simba hawakufurahia kwasababu mbalimbali ikiwemo uchumi na taarifa.

Mashabiki wa Simba mnatamani mechi ichezeshwe wapi?? Maamuzi ni yenu lakini uwanja lazima ukidhi vigezo vya bodi ya ligi

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Accra?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Accra