04/07/2026
🤷♂️ Je! Huwa unabadilisha Mswaki wako baada ya mda gani?
👉Mswaki unafaa kubadilishwa kila baada ya miezi miwili (2) hadi mitatu (3), au mapema zaidi k**a bristles zimeharibika au zimechoka. Hii inasaidia kuzuia mkusanyiko wa bakteria na vijidudu vingine vinavyoathiri afya ya meno na kinywa.
👉Mda mzuri wa kupiga mswaki ni mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kabla ya kulala.
👉 Kila kipindi cha kupiga mswaki kinapaswa kuchukua angalau dakika mbili (2).
👉 Inafaa kupiga mswaki baada ya kula ili kuondoa mabaki ya chakula na kuzuia mkusanyiko wa plaque na bakteria.