31/08/2026
SOMALIA KUNUFAIKA NA UZOEFU WA TPSC KATIKA KUANZISHA CHUO CHA TAIFA CHA UTUMISHI WA UMMA
Dar es Salaam, Agosti 31, 2026
Serikali ya Somalia imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha mageuzi ya utumishi wa umma kwa kujipanga kuanzisha Chuo cha Taifa cha Utumishi wa Umma huku ikilenga kutumia uzoefu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) katika uendeshaji wa taasisi ya mafunzo ya watumishi wa umma.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Shirikizo ya Somalia, Mhe. Hirsi Jama Ganni ulipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) akiongoza ujumbe wa serikali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya siku nne nchini Tanzania iliyolenga kujifunza uzoefu wa Tanzania katika mageuzi ya sekta ya umma, mabadiliko ya kidijitali na maboresho ya mifumo ya Serikali.
Mhe. Ganni amesema Somalia imeweka mageuzi ya utawala wa umma kuwa moja ya vipaumbele vya kitaifa na kwamba mafanikio ya Serikali yanategemea kuwa na watumishi wenye ujuzi na uwezo wa kubadilisha sera na mipango kuwa matokeo halisi kwa wananchi.
“Somalia inapanga kuanzisha Chuo cha Taifa cha Utumishi wa Umma kitakachokuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali, kuanzia mafunzo ya awali kwa watumishi wapya hadi mafunzo kwa viongozi waandamizi. amesema Mhe. Ganni”
Akizungumzia ziara hiyo, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho, amesema ujumbe huo umetembelea Tanzania kwa lengo la kujifunza namna utumishi wa umma unavyoendeshwa nchini, huku ziara ya TPSC ikiwa na msisitizo wa kujifunza kuhusu uanzishwaji na uendeshaji wa chuo cha utumishi wa umma.
Dkt. Mabonesho amesema Somalia ilikuwa na chuo cha utumishi wa umma hapo awali, lakini taasisi hiyo ilishindwa kuendelea kufanya kazi kutokana na changamoto zilizotokana na vita, hivyo sasa nchi hiyo inapanga kuanzisha upya taasisi hiyo kwa kujifunza kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.
25/08/2026
Tunawatakia Heri ya Sikukuu ya Mawlid Al Nabi!
24/08/2026
Join our short course training programme for September 2026. Scan the QR code to register or visit our website at www.tpsc.go.tz for online calendar and application
------------------------------------------
Jiunge na mafunzo ya muda mfupi kwa mwezi Septemba 2026
Skani QR kodi ili ujisajili au tembelea tovuti yetu ya www.tpsc.go.tz
21/08/2026
Wanafunzi wa shule za sekondari jijini Tanga wameendelea kutembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) ili kupata taarifa na fursa za mafunzo katika Maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Sekondari ya Usagara jiji Tanga.
Tunawakaribisha utembelee banda letu uweze kujipatia taarifa muhimu kuhusu:
🔶Mafunzo ya Muda Mrefu
(Astashahada & Stashahada na
Shahada )
🔷Mafunzo ya Muda Mfupi kwa
Watumishi wa Umma
Maonesho haya yatafikia kilele tarehe 24 Agosti 2026.
Nyoote mnakaribishwa sana!
Karibuni TPSC, Karibuni Tanga!
21/08/2026
Join our short course training programme for September 2026. Scan the QR code to register or visit our website at www.tpsc.go.tz for online calendar and application
------------------------------------------
Jiunge na mafunzo ya muda mfupi kwa mwezi Septemba 2026
Skani QR kodi ili ujisajili au tembelea tovuti yetu ya www.tpsc.go.tz.
18/08/2026
DIB WAPATAC MAFUNZO YA UONGOZI ELEKEZI KWA WATUMISHI WAKE
Morogoro, Agost 17 2026:
Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board – DIB) imeanza mafunzo ya uongozi kwa Timu ya Menejimenti pamoja na mafunzo elekezi ya awali (Induction) kwa watumishi wapya waliojiunga na Bodi hiyo.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa DIB, Ndg. Isack Nikodem Kihwili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Timeless, Morogoro, yakilenga kuwawezesha viongozi na watumishi wa Bodi kuongeza ufanisi, weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma.
Akifungua mafunzo hayo, Ndg. Kihwili amekishukuru Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo, akieleza kuwa yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha utendaji wa DIB na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
“Ninawasihi viongozi na watumishi wote kuwa wasikivu wakati wote wa mafunzo na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawezeshaji ili kuhakikisha tunapata maarifa na ujuzi utakaotusaidia kuboresha utendaji wetu,” amesema Ndg. Kihwili.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Ndg. Baraka Mwabenga, akimwakilisha Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho, amesema kuwa Chuo cha Utumishi wa Umma kina jukumu la msingi katika kuwaandaa watumishi wa umma kwa kuwapatia mafunzo katika hatua mbalimbali za utumishi wao.
Amesema kuwa, Chuo hutoa mafunzo kwa watumishi wa umma kuanzia hatua ya kuajiriwa, mafunzo elekezi ya awali, maendeleo ya kitaaluma na kiutendaji, hadi mafunzo ya kuwaandaa watumishi kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
“Chuo kinaendelea kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata maarifa, ujuzi na umahiri unaohitajika katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuendana na mabadiliko yanayotokea katika utumishi wa umma,” amesema Ndg. Mwabenga.
Mafunzo ya uongozi kwa Timu ya Menejimenti ya DIB yanafanyika kwa muda wa siku tano, kuanzia tarehe 17 hadi 21 Agosti 2026, huku mafunzo elekezi kwa watumishi wengine yakifanyika kwa muda wa siku 12, kuanzia tarehe 17 hadi 28 Agosti 2026.