Chikao Media

Chikao Media

Share

Page hii ni maalumu kwa kuweka habari za kimichezo na burudani hapa

09/05/2026

Na wakitoka hapo wanaanza kuimba nani k**a mama 🤣💔



07/05/2026

Ahmed Ally akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa Simba dhidi ya JKT, Azungumza juu ya upekee wa goli la Chama.

06/05/2026

😂😂😂 ila goli la chama 😂💔

🎥 Laxy



06/05/2026

Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga) imetangaza rasmi kumfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves, kufuatia maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Mei 6, 2026, uongozi wa Yanga umemshukuru kocha huyo kwa mchango wake ndani ya klabu na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.

Katika kipindi hiki cha mpito, timu hiyo itaongozwa na makocha Abdihamid Moalin pamoja na Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko ya kiufundi ndani ya kikosi hicho huku mashabiki wakisubiri kuona mustakabali wa timu yao katika mechi zilizosalia za msimu.

06/05/2026

Baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wameanza kuonyesha kutoridhishwa kwao na nyota wao Kylian Mbappé kupitia maoni kwenye chapisho lake la Instagram, wakimtaka aondoke ndani ya kikosi hicho.

Miongoni mwa ujumbe unaosambaa ni k**a:
“Mbappé, tafadhali ondoka kwenye timu yangu,”
“Mbappé out,”
na “Baki Italia, usirudi Madrid.”

Hali hii inaashiria kuongezeka kwa presha kutoka kwa mashabiki kufuatia kiwango chake cha hivi karibuni uwanjani.

Sponsored:

05/05/2026

Clatous Chama huenda akaingia kwenye historia ya soka kutokana na bao lake la kuvutia alilofunga katika dabi dhidi ya Young Africans SC, ambalo linatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuwania tuzo ya FIFA Puskás Award.

Bao hilo la kipekee limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka, wengi wakilisifu kwa ubunifu, umaridadi na ubora wa hali ya juu. Ikiwa litateuliwa rasmi, litakuwa heshima kubwa kwa mchezaji huyo pamoja na ligi ya Tanzania kuonekana zaidi kimataifa.

Sponsored:

05/05/2026

Bakari Nondo Mwamnyeto ameendelea kuonyesha ubora wake ndani ya kikosi cha Young Africans SC (Yanga), baada ya kufunga bao muhimu la kusawazisha katika dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC iliyomalizika kwa sare ya 2-2 tarehe 3 Mei 2026. Nahodha huyo pia ni tegemeo kubwa katika timu ya taifa ya Taifa Stars, akitambulika kwa uongozi wake thabiti na uwezo wa kuiongoza safu ya ulinzi kwa ufanisi.

Mbali na mchango wake uwanjani, Mwamnyeto bado anaendelea kuitumikia Yanga chini ya mkataba wa miaka miwili unaotarajiwa kumalizika Juni 2026. Katika msimu huu, amekuwa sehemu muhimu ya kikosi kilichoshiriki mashindano makubwa k**a CAF Champions League na NBC Premier League, akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio na mwendelezo wa matokeo mazuri ya timu hiyo.

Akiwa na umri wa miaka 30, uzoefu wake mkubwa pamoja na utulivu wake uwanjani vinaendelea kuwa silaha muhimu kwa Yanga katika harakati za kutwaa mataji zaidi, ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Sponsored:

04/05/2026

Simba hawakuwaheshimu Yanga baada ya kupata matokeo ya mapema.

Bashiri na kwa kuanzia dau la Tsh1000 uingie kwenye droo ya kushinda TV mpyaa.

Tembelea: www.kingbet.co.tz

03/05/2026

Mchezo wa Kariakoo Dabi umetamatika kwa suluhu ya mabao mawili 2-2 mchezo uliocgezwa kwenye uwanja wa Mej Gen Isamuhyo, Baada ya matokeo hayo gepu la point litasalia kuwa 5 vile vile yanga akiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na Simba akiwa nafasi ya pili.

03/05/2026

Klabu ya Inter Miami CF imeongeza juhudi katika harakati za kumsajili kiungo wa Manchester United, Casemiro, huku ikimuweka k**a chaguo lao kuu la kuimarisha safu ya kiungo.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo bado yanaendelea vizuri, na kiungo huyo raia wa Brazil anaonesha kuvutiwa na wazo la kuhamia Miami, licha ya kuwa na ofa nyingine mezani.

Inter Miami inaonekana kuwa na dhamira ya kuongeza wachezaji wenye uzoefu mkubwa ndani ya kikosi chao, na Casemiro anachukuliwa k**a sehemu muhimu ya mkakati huo. Endapo dili hili litakamilika, linaweza kuwa miongoni mwa usajili mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ndani ya Major League Soccer katika msimu ujao.

03/05/2026

Selemani Mwalimu Baada ya kuibuka kuwa mchezaji bora wa kombe la Mapinduzi, timu yake ya Wydad Casablanca imempongeza kwa hatua hiyo nzuri na muendelezo bora ambao ameendelea kuuonyesha katika ligi ya kuu Tanzania tangu alipojinga na Simba kwa Mkopo.

Ikumbukwe mwishoni mwa msimu huu mkataba wa mkopo ambao unamfanya Mwalimu kuichezea Simba unafikia tamati na itambido arejee kwenye klabu yake.



Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address

Temeke
Dar Es Salaam