28/07/2026
Hatimaye Yanga SC imefanikiwa kumpata mmoja wa washambuliaji bora zaidi barani Afrika, Peter Shalulile, nahodha wa timu ya taifa ya Namibia na nyota wa zamani wa Mamelodi Sundowns. Usajili huu unatajwa kuwa miongoni mwa usajili mkubwa zaidi wa msimu kutokana na rekodi na uzoefu mkubwa alionao.
Shalulile amejijengea jina kwa uwezo wake wa kufunga mabao, harakati nyingi uwanjani, kasi, pamoja na kutumia vizuri nafasi chache anazopata. Kwa miaka kadhaa ameendelea kuwa miongoni mwa washambuliaji waliotisha zaidi katika soka la Afrika Kusini.
Ujio wake unaongeza nguvu kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Yanga huku mashabiki wakiamini kuwa atakuwa silaha muhimu katika kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Karibu Jangwani, Peter Shalulile! 💚💛
24/07/2026
Rais wa Yanga amemtambulisha Ibrahima Toure kuwa sehemu
ya kikosi cha Wananchi kuelekea msimu ujao. Mashabiki wamepokea ujio huo kwa hamasa kubwa huku wakisubiri kuona uwezo wa nyota huyo ndani ya uwanja.
24/07/2026
Klabu ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji wake mpya,
Housseine Zakouani, ambaye tayari ameanza kupewa sifa kubwa kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao.
Mashabiki wa Yanga wanaamini ujio wa Zakouani utaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, huku wakisemani aina ya mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha mchezo muda wowote.
#
24/07/2026
KATORO: Rais wa Yanga, Hersi Said ametangaza rasmi kwamba ufunguzi wa Wiki ya Mwananchi mwaka 2026 utafanyika ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, na kilele chake kitakuwa ni Agosti 9, 2026.
24/07/2026
Simba SC imemtambulisha rasmi mshambuliaji lbrahim Doumbia
baada ya kumsajili kutoka AS Korofina ya Mali kwa mkataba wa miaka miwili. Straika huyo mwenye umri wa miaka 19 aling'ara msimu uliopita kwa kufunga mabao 17 na kutoa asisti 5, akimaliza k**a mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali. Katika mashindano yote,
Doumbia alifunga mabao 22 ndani ya mechi 26 na pia ni sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Mali U-20.
Simba inaamini usajili wa Doumbia utaongeza makali ya safu ya ushambuliaji
kuelekea mashindano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
22/07/2026
Mchezaji wa Wydad Casablanca Seleman Mwalimu amekubali
kuongeza mkopo wake mwingine wa Mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Simba
Awali kulikuwa na taarifa huwenda Wydad wangemtoa kwa mkopo barani ulaya lakini Simba Sc wameamua kusalia na mchezaji huyo ambaye msimu jana aliitumikia Simba Sc,
Sele Mwalimu alikuwa na mkataba wa miaka minne na timu ya Wydad Casablanca ya Nchini Morocco,