Manuva Sports

Manuva Sports

Share

The official Manuva Sports account | Sports News 📰 | House 🏡 Of Sports

11/05/2023

Nchi umekubali kwa kauli moja ubora wa Bacca, Wachambuzi 99% wamesema ndio Man of the match.

"Mchezaji bora siku ya leo alikuwa Bacca, kwa sababu kabla ya mchezo wa leo hatari ya Marumo Gallants ilikuwa ni kwa striker wao, Ranga Chivaviro ambaye kwenye ligi ya Afrika kusini ameshafunga magoli (10) ..."

"... Akiwa miongoni mwa Wachezaji wa juu kabisa wanaoongoza kwa kufunga, kwa upande wa CAFCC ana maholi (5) sawa na Mayele, hivyo mpaka hapo ni mchezaji hatari"

"Kwa hiyo huyu mchezaji hatari alitakiwa awekewe ulinzi ili asiwe hatari, na hilo jukumu leo alipewa Ibrahim Bacca. Bacca leo amewania mipira mara (6) na akashinda (5) akipoteza mpira (1), na kwenye mipira hiyo amewania na Chivaviro mara (3) akashinda"

"Na katika mipira ya vichwa ameruka mara (6) huku ikipata (3) na katika yote hiyo ameruka na Chivaviro na akashinda.. Kwangu Bacca (25) ndiye Man of the match"

©️ Abissay stephen
Mchambuzi Kipenga extra EA-Radio


"Ibrahim Bacca leo sio tu alikuwa beki bora kwa Yanga Africa, ni mchezaji bora kwenye mechi.. Pamoja na sifa nyingi ambazo nimezitaja kuhusu Bacca, leo nimegundua pia kuwa ana leadership Quality"

"Kitambaa anacho Bakari Nondo, lakini Bacca anaongoza kwa matendo yake. Just wooow 🙌"

"Bacca ananifirisi maneno ana vitu vingi ambavyo vinamaanisha mchezaji wa kiwango cha juu. Anafanya vitu vingi kwa usahihi tena kwa muendelezo"

"Anazungumza sana, ana organize sana wenzake. Kwenye Mchezo huu Yanga wamefanya Tackles (15) na zimefanikiwa kwa (83%), Bacca amefanya clean Tackles (6). Anashinda vita zake angani na ardhini na ni mshindani kwelikweli"

©️ Wilson Oruma
Mchambuzi wa Efm radio


"Wananchi anytime wanaweza kutinga fainali aisee.. Game tough ya marudiano lakini mbili nyingi"

"Hawa Gallants ni watu na nusu, Yanga wawe makini lakini wana advantage kubwa .. Achana na bao la Aziz Ki na utundu wa kichaa msomi bwana Morrison katika bao la pili, lakini yule BACCA ni TOP TOP TOP defender"

©️ Edo Kumwembe
Mchambuzi wa Wasafi fm Radio


10/05/2023

Mama ame-tweet tayari….

"Hongereni Yanga kwa ushindi katika mchezo wenu wa raundi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup).

Nawatakia maandalizi mema kwa mchezo wenu wa raundi ya pili, muendelee kuiheshimisha nchi yetu.

Hamasa yangu inaendelea". Je, k**a Mama amepongeza, wewe ni nani?

FT: Yanga 2-0 Marumo

View all 21 comments

10/05/2023

Dogo kichuya ahama simba sc kujiunga young African

FT: Yanga 2-0 Marumo

10/05/2023

Mashabiki Yanga "AUCHO APEWE MAUA YAKE"

10/05/2023

... Endeleeni kuongea 🗣️

Lakini yeye kachagua kuwajibu kwa vitendo kwa kufunga magoli muhimu tu !

Magoli yote ya Aziz Ki msimu huu !

⚽ vs 🇹🇳 Club Africain - CAF
⚽🅰️ vs 🇸🇸 Zalan - CAF
⚽🅰️ vs Simba
⚽🅰️ vs Azam
⚽⚽ vs Mtibwa
⚽ 🅰️ vs Rhino Rangers (FA)
⚽ vs Namungo
⚽ vs Transit camp
🅰️🅰️ vs Coastal Union
🅰️ vs Real Bamako - CAF
⚽⚽⚽ vs Kagera sugar
⚽ vs Singida Big stars
⚽ vs 🇿🇦 Marumo Gallants - CAF

14 - Goals
07 - Assists
01 - Hat-trick

Msimu unaendelea ...



#
Udaku:

10/05/2023

🏟️ YANGA 2️⃣-0️⃣ MARUMO GALLANTS

Wananchi wanatakata Lupaso bao la Stephen Aziz Ki likiwapa Uongozi katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya Nusu fainali .

Pasi kisu kutoka katikati ya Kiwanja inatua Winga ya kulia Kwa Kisinda ambaye anamkamua beki na kutoa Assist Kwa Azizi Ki ambaye anakutana na Mpira njiani na kupiga k**a penalty ngoma Kambani.

Shambulizi la kush*tukiza Fiston Mayele anamuwekea njiani Benard Morrison ambaye anaweka Mpira nyavuni na kuwapa furaha Wananchi.

🤪Yanga wapewe Kombe lao la shirikisho mapema tuu ndugu zangu .

Gallants wamecheza vzri sana lakini Yanga wamesepa na ushindi.

Kuna muda unatakiwa ucheze Soka lisilo vutia lakini usepe na ushindi.

Azizi Ki ⚽
Morrison ⚽







10/05/2023

FT: Young Africans 🇹🇿 2️⃣ ➖ 0️⃣ Marumo 🇿🇦

⚽ Aziz KI
⚽ Bernard Morrison

Nusu Fainali ya CAF Confederation Cup

10/05/2023

Simba SC hajapiga hatua yoyote ndani ya misimu miwili.

LIGI KUU YA NBC 🇹🇿
2021/22 Nafasi ya 2️⃣
2022/23 Nafasi ya 2️⃣

MASHINDANO YA CAF
2021/22 Robo Fainali
2022/23 Robo Fainali

ASFC 🇹🇿
2021/22 Nusu Fainali
2022/23 Nusu Fainali

10/05/2023

CEO wa Simba afunguka kuhusu posho ! Amesema wanadaiwa Milioni 20 tu !

"Timu yetu imeshatoa bonus zaidi ya BILIONI 1.1, na kiasi kilichobaki (Tunachodaiwa) ni Milioni 20 pekee, tena ni Bonus ya ligi ya ndani (NBC premier league)"

"Wewe vuta picha, klabu inalipa zaidi ya BILIONI 1.1 unashindwaje kulipa Milioni 20 haiingii akilini, hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu" - Imani Kajula

"Vuta picha Wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na Milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya (30), kila mmoja atapata kiasi gani ! .. "

"... Ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi !! "

"Kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema klabu ya Simba itawalipa Wachezaji Bonus, ila huwa tunatoa kwa ajili ya kuwahamasisha tu wapambane zaidi kwenye kile wanachokipambania"

©️ Imani Kajula
Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba

Follow

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address

Dar Es Salaam