Chita michuzi

Chita michuzi

Share

UKURASA WA TAARIFA MBALIMBALI ZA KIAFYA NA KUJULISHANA JUU YA VIATARISHI MBALIMBALI VYA MAGONJWA !

HUSUSANI MAGONJWA YA AFYA YA AKILI YA UTATUZI WAKE ASANTENI!!DR NYABUYA ,MD

02/05/2026

Dr Godfrey Nyabuya MD ,
Psychiatric resident at MUHAS
Father-Mentor
C.E.O
Contact
+255 718710224
[email protected]

Elimu ya afya ya akili na tiba ya uhakika
Elimu katika Taasisi za KIJAMII- kanisani,Msikitini, seminar za vijana na wazee ,wajasiliamali,Vyuoni,shuleni na familia

KARIBUNI SANA 🙏🏿

25/04/2026

ATHARI ZA MALEZI NA AFYA YA AKILI
Sehemu ya pili(2)
Je ? ATHARI ZA malezi zinaweza kusababisha changamoto zipi za afya ya akili

1: URAIBU kwa mujibu wa tafiti za kitaalam asilimia 40% ya waraibu ni waathirika wa moja Kwa moja wa ATHARI ZA kimalezi
mfano wa ushuhuda
kijana mmoja alijikuta kwenye uraibu wa madawa ya kulevya na pombe baada ya kuona wazazi wake ni waraibu basi nae akajikuta humo

2: WASIWASI WA KUPITILIZA - ANXIETY
malezi Yana mchango mkubwa wa kusababisha mtu mmoja kushindwa kuimili hisia zake na kuwa mtu wa kuogopa, kushindwa kijiamini

3: Depression -SONONA
malezi Yana mchango mkubwa kuchochea ama kuongeza nafasi ya kuugua au kupata ugonjwa wa sonona haswa Kwa watoto ambao wamekumbana na changamoto za kimalezi

4: Post traumatic stress disorders - PTSD
ATHARI ZA kimalezi zinazalisha changamoto za KISAIKOLOJIA ambazo uchochea vijitabia ambavyo utokea na kuathiri mfumo wa maisha ya mwanadamu Kwa ujumla

hayo ni baadhi tu basi Kwa pamoja Jamii, serikalini wazazi na walezi ni jukumu letu kuweka misingi ya malezi ya uhakika na salama Kwa watoto na Jamii mzima inayotuzunguka

ATHARI ZA MALEZI ni kubwa sana hasa Kwa Jamii ya Sasa ambayo misingi ya familia yaani BABA,MAMA NA WATOTO imeanza kupotea na
kuibuka mitindo mipya ya MALEZI k**a vile SINGLE PARENTING STYLE yaani single mother,au single father
Muda mchache wa kukaa na familia haswa Kwa wazazi na watoto ,mitandao ya KIJAMII
Tukutane sehemu ya pili tuone baadhi ya changamoto za afya ya akili zinazotokana na ATHARI ZA MALEZI

Godfrey Nyabuya MD MMED
+255718710224
[email protected]

25/04/2026

ATHARI ZA MALEZI NA AFYA YA AKILI
sehemu ya kwanza (1)

MALEZI Yana sura Pana sana kwenye maisha ya Kila siku ya mwanadamu

Ulivyo Leo Kwa kiasi kikubwa ni mchango wa MALEZI uliyopata Kwa wazazi ,mzazi na Jamii Kwa ujumla

Je ? MALEZI Yana mchango upi kwenye changamoto ya afya ya akili

Malezi Kwa ujumla umfanya mtu awe na uwezo wa :
1: kukabiriana na changamoto
2: kutatua
3: kuvumilia
4: Upendo
na mengine mengi mazuri

Upande wa Pili -Malezi yanaweza kumfanya mtu awe:
1: uwezo mdogo wa kutatua changamoto
2: hasira
3: uraibu
4: chuki
5: Mauaji

ATHARI ZA MALEZI ni kubwa sana hasa Kwa Jamii ya Sasa ambayo misingi ya familia yaani BABA,MAMA NA WATOTO imeanza kupotea na
kuibuka mitindo mipya ya MALEZI k**a vile SINGLE PARENTING STYLE yaani single mother,au single father
Muda mchache wa kukaa na familia haswa Kwa wazazi na watoto ,mitandao ya KIJAMII
Tukutane sehemu ya pili tuone baadhi ya changamoto za afya ya akili zinazotokana na ATHARI ZA MALEZI

Godfrey Nyabuya MD MMED
+255718710224
[email protected]

15/04/2026

SEHEMU YA PILI
KUJIKOJOLEA KITANDANI !!
NIFANYE NINI??
DOCTOR NISAIDIE!!!!
KARIBUNI TUJIFUNZE
JE KUJIKOJOLEA NI TATIZO LA TATIZO NINI??
DR GODFREY: Pole sana na hongera Kwa ujasili 'Tatizo la kujikojolea k**a linavyoitwa au kushindwa kuzuia aja ndogo hasa nyakati za usiku unapolala.

NINI KIFANYIKE?
Kwanza kabisa 1: kupata tiba Kwa watoa huduma sahihi
Ili tuweze kufahamu sababu haswa inayopelekea kushindwa kuzuia haha ndogo

Kwa kifupi kufanya baadhi ya vipimo lakini na kuongea na mgonjwa Ili KUWEZA kufahamu haswa changamoto anazolitia

hii Kwa kiasi kikubwa imekua ikisaidia wengi kuondokana na tatizo Ili

TIBA : WASILIANA NAMI ILI TUWEZE KUONGEA NA KUKUSAIDIA

NB: TUSIPIGE WATOTO SABABU YA KUJIKOJOLEA TUNAZIDI KUMSABABISHIA TATIZO WASILIANA NAMI KWA TIBA YA UHAKIKA NA SALAMA


+255718-710224
[email protected]

15/04/2026

KUJIKOJOLEA KITANDANI !!
NIFANYE NINI??
DOCTOR NISAIDIE!!!!
KARIBUNI TUJIFUNZE
JE KUJIKOJOLEA NI TATIZO LA TATIZO NINI??
DR GODFREY: Pole sana na hongera Kwa ujasili 'Tatizo la kujikojolea k**a linavyoitwa au kushindwa kuzuia aja ndogo hasa nyakati za usiku unapolala.

Ni Tatizo ambalo limekua likiwatesa watu wengi sana wanaume Kwa wanawake

KIBIOLOGIA tatizo Ili Lina sababu kadhaa ambazo kimsingi zinaweza sabaisha moja Kwa moja ama si moja Kwa moja Yaani " direct effect na indirect effect"

Nitaorodhesha hapa sababu hizo :

1: Sababu za kimaumbile -
Kuna maumbili ya watu baadhi kushindwa kuhimili Hali ya kuzuia mkojo la sababu ya misuli kuchelewa kukomaa hivyo kushindwa kuzuia vzr haja ndogo

2: Magonjwa katika mfumo wa fahamu- -k**a vile kifafa ,hapa wenye DALILI ama ugonjwa wa kuanguka na kukaamaa viungo Yaani kifafa wapo kwenye kundi kubwa la watu wanaoshindwa kuzuia haja zao hasa nyakati za usiku ambazo Hali hiyo uwakuta bila kuwa na ufahamu

3: Magonjwa ya mfumo wa mkojo-
hapa Kuna aina nyingi sana za magojwa ya mfumo wa mkojo

4: Changamoto za KISAIKOLOJIA-
hapa tuna kundi kubwa sana ambalo Kwa kiasi kikubwa ndio linachukua asilimia kubwa sana na linahitaji msaada mkubwa sana

ungana nami sehemu ya pili

+255718-710224
[email protected]

10/04/2026

KARIBU SEHEMU YA PILI (2)
BI-POLAR NI NINI?
Karibu sana Kwa Dr Godfrey tuweze kujifunza :
Maana
Huu ni ugonjwa ambao umewekwa kwenye makundi ya magonjwa ya akili ambayo Yana husisha Kwa kiasi kikubwa HISIA
Je hisia nazo zinakuaje BI-POLAR
2- POLAR MANIC AND DEPRESSED

2: DEPRESSED "HISIA ZA HUZUNI SANA"
Hizi uambatana na dalili haswa za sonona au hisia za uhuni
Mtu anaonekana mwenye huzuni, amejikunja na hana nguvu
Dalili zake:

•Huzuni kali

•Uchovu mwingi

•Kukosa matumaini

•Kujitenga na watu (withdrawal)

NATOA ELIMU NA TIBU YA AFYA YA AKILI KWA TAHASISI MASHULENI MAKANISANI NA MISIKITINI
FOR CONTACT 0718-710224
email: [email protected]

10/04/2026

BI-POLAR NI NINI?
Karibu sana Kwa Dr Godfrey tuweze kujifunza :
Maana
Huu ni ugonjwa ambao umewekwa kwenye makundi ya magonjwa ya akili ambayo Yana husisha Kwa kiasi kikubwa HISIA
Je hisia nazo zinakuaje BI-POLAR
2- POLAR MANIC AND DEPRESSED
""hisia za furaha sana(MANIC) na hisia za huzuni sana(DEPRESSED)"
1-MANIC "HISIA ZA FURAHA SANA(Msisimko kupita kiasi)
Mtu anaonekana mwenye furaha sana na nguvu nyingi
Dalili zake:

•Kuwa na furaha kupita kiasi (euphoria)

•Kuwa na nguvu nyingi sana

•Kufanya maamuzi hatarishi (mfano matumizi mabaya ya pesa)

•Mawazo kwenda kwa kasi (racing thoughts)
TUKUTANE SEHEMU YA PILI (2)
NATOA ELIMU NA TIBU YA AFYA YA AKILI KWA TAHASISI MASHULENI MAKANISANI NA MISIKITINI
FOR CONTACT 0718-710224
email: [email protected]

20/02/2026

HISIA ZA HASIRA -MAHUSIANO YANAVUNJIKA
SEHEMU YA PILI

Doctor: Mhh! sawa

Client: Na Sasa nimekuja maana kazi imefika kipindi boss ameshindwa kuvumilia Hali yangu maana nimekua nikimfokea mpaka yeye bila kujali

Doctor: sawa sawa ! Hali hii inaelezeka kitaalamu Hali ya kihisia pia uratibiwa na sehemu zetu za ubongo
katika Hali hiyo ,Kuna sababu nyingi ambazo kuchangia kushindwa kudhitibiti hisia zako na kujikuta kuangukia kwenye maamuzi ya hisia Kali Yani hasira ama tabia hatarishi .......
na tiba zake zimejigawa katika makundi kadhaa ikiwa KIBIOLOGIA KISAIKOLOJIA NA KIJAMII
Hongera Kwa kuja kupata huduma na kupata utatuzi juu ya changamoto ulionayo

WASILIANA NA Dr Godfrey Nyabuya
afya ya akili talks #
Private consultation
Public consultation
natoa elimu kwenye Jamii kanisani na misikitini pamoja na Taasisi mbali mbali
karibu
+255 718-710224
[email protected]

20/02/2026

HISIA ZA HASIRA -MAHUSIANO YANAVUNJIKA :-
FUATILIA MAZUNGUMZO HAYA

Doctor:Karibu sana

Client: Asante Dr ,mimi nimekua nikisumbuliwa na Hali ya hasira Kali sana

Client: Imefikia wakati na umri wa huu WA miaka 35 Sina Rafiki kabisa hata ndugu zangu awawezi kupokea simu zangu
mke wangu alishakimbia ,majirani ndio kabisa yani
Nikisikia ama kupewa taarifa yoyote nisioitarajia basi nashindwa kuhimili hisia zangu za hasira ambazo nimekua nikitoa maamuzi bila busara na baadae ndio nitajutia
k**a vile kutukana , kupiga kubomoa vitu
ata kuvunja mahusiano na huyo mtu

Doctor: Pole sana na napata Picha Hali unayopitia !! mhh unaweza kuendelea

Client: Yani mpaka sasa Nina watoto 6 na Kila mtoto na mama yake na hata huyu wamwisho sipo na mama yake na naishi mwenyewe bila mtoto yoyote watoto wananiogopa nifanyaje ?

Doctor: Pole sana aisee
je unaweza nishirikisha uliwahi kufanya chochote katika kukabiliana na Hali hiyo

Client: Ndio Doctor Nilianza kua sio muongeaji lakini pia kuondoka eneo ambalo linanipa hisia za hasira doctor na sijafanikiwa

TUKUTANE SEHEMU YA PILI YA MAZUNGUMZO

14/02/2026

URAIBU WA POMBE 🍻
SEHEMU YA PILI
Doctor: Pole sana Kwa yote unayopitia
Je ulishawai kujalibu kutumia pombe na Kwa kipindi gani ?

Client: Ndio doctor niliweza kuacha Kwa muda wa miezi 6

Doctor: hongera sana na kitu gani haswa kilifanya ukarudi kwenye matumizi ya pombe ?

Client: Doctor marafiki lakini pia nikipitia changamoto za maisha naona kunywa pombe ndio suluhisho pekee doctor

Doctor: sawa nimekulewa na mimi nitakusaidia Kwa kwanza kukufahamisha juu ya tatizo linalokusumbua
Kwanza una changamoto ya uraibu Yani matumizi ya pombe kupindukia ambayo yanasqbabisha unaangukia kwenye changamoto ya afya ya akili au DALILI za afya ya akili
KWA MATIBABU ZAIDI YA KIBIOLOGIA ,KISAIKOLOJIA NA KIJAMII
tunaweza kuliondoa au kutatua tatizo Kwa kiasi kikubwa
Wasiliana. Na mtaalam wa magonjwa ya afya ya akili
DR GODFREY NYABUYA
0718-710224
emails: [email protected]

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Ubungo
Dar Es Salaam