23/10/2025
Hadithi fupi: “Mama wa Kamno”
Katika kijiji cha Mbuyuni, aliishi mwanamke mmoja aitwaye Mama Kamno. Jina lake halikutokana na ukoo, bali kwa sababu ya mtoto wake wa pekee, Kamno. Watu wote kijijini walimjua k**a mwanamke jasiri, mwenye bidii, na asiyeogopa kazi.
Baada ya mumewe kufariki katika ajali ya baiskeli, Mama Kamno alibaki peke yake kulea mtoto wake. Alikuwa akiamka alfajiri, akienda shambani kupanda mahindi na mihogo, kisha mchana kuuza mboga sokoni. Ingawa maisha yalikuwa magumu, hakuwahi kulalamika; kila mara alitabasamu na kusema, “K**a kuna jua leo, basi kesho itanyesha.”
Kamno alipokuwa akienda shule, Mama Kamno alihakikisha anaenda akiwa ameshiba na amevaa safi, hata k**a nguo zilikuwa zimechakaa. Alimfundisha kuwa elimu ndiyo urithi bora kuliko mali. Mara nyingi usiku, akiwa amechoka, aliketi karibu na taa ya koroboi akimsaidia mtoto wake kusoma.
Miaka ilipita. Kamno alifaulu vizuri shuleni, akapata nafasi ya kwenda chuo kikuu mjini. Kijiji kizima kilimzomea Mama Kamno kwa furaha—walijua jitihada zake hazikupotea. Wakati wa kuaga, machozi yalimtoka lakini moyo wake ulikuwa umejaa fahari.
Miaka michache baadaye, Kamno alirudi kijijini akiwa mwalimu. Alimjengea mama yake nyumba ndogo nzuri yenye bati jipya na sakafu safi. Mama Kamno alitabasamu akisema, “Sasa ninaweza kupumzika, lakini moyo wangu unacheka.”
Na tangu siku hiyo, watu wa Mbuyuni walitumia jina “Mama wa Kamno” kumaanisha mwanamke mwenye nguvu, moyo wa upendo, na imani isiyokufa katika watoto wake.
MWISHO
12/04/2025
MKEO AU MCHUMBA AKIKUACHA HIVI NDIVYO UTAKAVYOFANYA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Ili mwanamke asikusumbue kuna kanuni nyingi lazima uzijue na uzitumie.
Mojawapo ya Kanuni hizo
1. Demand and Supply Law.
Hii uliisoma kwenye Commerce bila Shaka kidato cha pili. Kanuni hii haipo tuu kwenye Masuala ya biashara na uchumi. Bali inatumika pia kwenye Mahusiano ya Mapenzi na Ndoa.
Mwanaume lazima uhakikishe demand yako kwa Wanawake ni kubwa. Yaani wanawake wengi wanakuhitaji.
Kadiri wanawake wengi wanavyokuhitaji ndivyo heshima yako ndani ya ndoa inavyozidi kuwa kubwa.
Kuhitajika Sana hii inamaanisha thamani yako iko juu. Na wanawake hawanaga nguvu kwa Wanaume wenye thamani kubwa.
Jinsi ya kuwa Mwanaume mwenye thamani;
a) Mwili wenye afya na uliopangika k**a Mwanaume.
Fanya utakavyofanya lakini kamwe usijeharibu mwili wako.
Mwili wenye nguvu,mwendo wa kujiamini, Sauti yenye Mamlaka ya Mwanaume mwenye akili anayejua anachozungumza. Sio uwe mjinga.
Hakikisha ukivaa nguo zinakukaa na kukuonyesha wewe ni mwanaume mwenye mvuto wa mwanaume sio mwonekano wa mwanaume aliyechoka, Mzee au Fukara.
b) Uwe na kipato cha uhakika.
Hii inatokana na kufanya Kazi. Hakikisha huutumii Muda wako kufanya vitu visivyo kujenga. Tafuta kuwa na nguvu ya kiuchumi lakini katika utafutaji huo usiathiri afya yako
Haitakuwa na maana yoyote Ile kuwa na Pesa alafu huna Afya Njema. Huna mwili wenye nguvu na uliojengeka k**a mwanaume. Huna nguvu za kiume.
c) Uwe na maarifa, ufahamu na ujuzi wa mambo Mengi.
Sio lazima uende shule siku hizi mitandaoni kuna kila kitu.
Kina Taikon Tupo kuilisha Akili yako vitu uwe na ufahamu.
Soma vitabu, soma Makala, fuatilia documentary.
Hata uwe na pesa Kiasi gani k**a wewe ni maamuma hakuna mwanamke atakayejivunia na kukuheshimu.
Wanawake na watu huheshimu wanaume wenye AKILI.
4. Maarifa ya Kiroho.
Unaweza ukawa na hayo matatu hapo juu lakini ukikosa maarifa ya Kiroho ni rahisi mambo madogomadogo hasa ya Mahusiano na Mkeo na watoto yakakusumbua pakubwa.
Utashangaa mtu kasoma, na msomi mzuri, anapesa, na anaafya Njema lakini anashindwa kuiongoza Familia yake. Mkewe na watoto wamemshinda.
Mtu huyo bila Shaka atakuwa na tatizo la msingi la kukosa maarifa ya Kiroho.
Afya Njema + Pesa + Elimu Dunia + Elimu ya Kiroho= Mwanaume mwenye Thamani
2. Kujua Saikolojia ya wanawake.
Ili Wanawake wasikusumbue lazima uwe master of the Games. Lazima ujue saikolojia Zao.
Ukishajua Saikolojia ya mwanamke ni kwamba wewe tayari ni mwanaume unayejitambua.
Kwa sababu mwanamke yupo ndani ya mwili wako hata kisayansi na kiimani IPO hivyo.
Kutojua mwanamke ni kwamba hujijui nusu yako nzima.
Hupaswi kumpenda mwanamke unconditionally. Na k**a utampenda unconditionally Basi hutakiwi kuonyesha hivyo.
Ukiwa na mwanamke cheza wanavyocheza lakini tumia AKILI.
Mwanamke usimuonyesha na Wala asigundue hauna options zaidi yake. Atakusumbua.
Huwezi Mtawala mwanamke ambaye ameshajua unampenda kuliko na huna uwezo wa kuwa na mwanamke mwingine zaidi yake. Na wanawake wengine hawakutaki.
Usikubali kuonyesha Madhaifu yako mbele ya mwanamke.
Na Wala usikubali kuonyesha strengths zako zote mbele ya mwanamke. Strengths zingine ziache k**a Ziada ya suprise siku akiondoka.
Strengths za MWANAUME ambazo hupaswi kuzionyesha zote;
1. Kipato chako.
K**a kiwango chako cha kipato ni Milioni Moja basi onyesha Laki sita yaani asilimia 60 tuu.
2. Uwezo wako WA kutatua matatizo.
Usiwe kiherehere wa kujifanya unajua kutatua matatizo harakaharaka. K**a unauwezo wa kutatua matatizo kwa asilimia 80% punguza asilimia 20% kisha onyesha 60%.
Kamwe usije onyesha uwezo wako wote mbele za MWANAMKE.
Samson kilimlamba.
Ingawaje Samoson alitumia Kanuni ya kujifanya Hana uwezo wa kutatua matatizo lakini Delila alimbana kwenye Kona akajikuta anaonyesha uwezo wake wote. Na hapo ndipo anguko lake lilipokuwa.
Kuna Muda mwanamke anaweza kukujaribu kujua uwezo wako wa ku-solve issues. Usipende sifa Sana.
Hata Mungu anaweza kukusaidia kila kitu lakini hafanyi hivyo Kiasi kwamba unakuwa na wasiwasi kwamba Hana huo uwezo. Hiyo kwa Sisi wanafalsafa ni Mbinu ya utawala na kuongeza heshima na uhitaji.
3. Usionyeshe uwezo na Mbinu zako zote katika utafutaji wa Mali.
Mwanamke akishagundua kuwa umefikia mwisho wa uwezo wako ndio huwa mwanzo wa kukudharau. Lakini pia KIUSALAMA kwako inakuwa haijakaa Sawasawa.
Wanawake huvutiwa na suprise. Na hujisalimisha kwa Wanaume wanaojua kutoa suprise kwao.
Utawasikia wakisema, aiseeh! Fulani kani-suprise KWELI. Sikutegemea kwamba angefanya hivi.
Suprise kwa mwanamke huichukulia k**a uwezo Mkubwa ambao ulikuwa Nje ya Akili yake Kabisa.
4. Usionyeshe Siri zako za kihalifu au uovu Mkubwa mbele ya mwanamke.
Hata kwa umri upi. Kamwe usije ukafanya Uhuni wako huko. Tunajua Sisi wanaume kwenye utafutaji kunakuwa na Mambo Mengi. Ikitokea ukawa na Jambo kubwa la kihalifu au uovu Mkubwa kamwe Mkeo au mwanamke unayeishi naye asijue.
Kwako haitakuwa Salama.
Na utakuwa mtumwa wake.
Sitaki kuwachosha!
Nimetoa maelezo hayo ili nitoe hoja za mambo ya kufanya pale Mkeo au Mchumba wako anapokuwa amekuacha;
1. Kamwe usimzuie Mwanamke anayetaka kukuacha.
Kwa Sisi Watibeli mwanamke hata akitania au akipitiwe kusema atatuacha au anatuacha tunavunja uhusiano siku hiyohiyo.
Watibeli kuna maelfu na maelfu ya wanawake wazuri, wasafi, wenye vipato wanaoomba kila siku kwa Mungu watupate. Hivyo hatuwezi kuwa na mwanamke anayetaka kutuacha hata kwa dakika Moja. Tunaheshimu maamuzi ya huyo Mwanamke.
Ni kosa kubwa kijana utalifanya kumlazimisha mwanamke ambaye hakutaki. Hata k**a mnawatoto ishirini. K**a hakutaki piga chini.
2. Usioe Wala kuwa na mwanamke mwingine kwa Muda angalau Miaka mitatu.
Endelea na mambo mengine. Hiyo haimaanishi hautapata huduma ya Ngono.
Wapo wanawake maelfu kwa maelfu unaweza kuwanunua kwa Mafungu k**a Nyanya wakakutuliza Hamu zako.
Kamwe usichukue Mke wa Mtu labda awe kwenye Masoko ya kujiuza huko. Hilo halitakuwa kosa Lako
3. K**a amekuacha wewe na mnawatoto asikupangie matumizi ya watoto.
Akikupeleka serikali au vyombo vyovyote toa Msimamo wako. Kwamba uwezo wa kuhudumia watoto wako wakiwa mbali na wewe hautalingana na ule ukiwa nao karibu.
4. Hakikisha Unakua na kuimarika kwenye idara zile muhimu.
Mwanamke anapokuacha atataka kujithibitishia na kuthibitishia watu kuwa uamuzi aliouchukua ulikuwa sahihi hivyo atatamani kuona haukui, hauimariki kiuchumi na kiafya au kwenye Jambo lolote
Hii itamfanya ajisikie NAFUU na kusema mbele za watu yeye ndiye alikuwa na Nyota na alikuwa anakupiga tafu.
Ndio maana Taikon Master nimekuambia ni lazima ukue kiuchumi, kiakili, mwili na afya yako iimarike.
Ukikua na kuimarika hii itamuweka sehemu mbaya na kujiona yeye ndiye alikuwa na Mkosi na jamii itaona hivyo Jambo ambalo kwake litakuwa pigo kubwa la kimedani.
Ndugu yangu, hupaswi ukiachwa au kuachana uende kunywa mapombe yakuumize, haupaswi kufanya ngono zembe nope!
Ili uimarike na kukua utatumia maelezo niliyoyatoa juu Kule, katika pointi inayofuata;
5. Tumia Mbinu, uwezo na maarifa na kipato ambacho hukumuonyesha kujiimarisha na kukua.
K**a ulionyesha uwezo na maarifa na kipato chote ni hakika itakuwia vigumu kukua na kuimarika maana tayari grafu yako ilikuwa kwenye peak.
Umeachwa sasa ndio ule Muda WA kutumia Yale ambayo hakujua unayo. Uwezo uliokuwa nao ambao haukuuonyesha ndio Muda wake huo.
Kipato au miradi uliyokuwa nayo uliyomficha ndio Muda wa kuidhihirisha Mmoja baada ya mwingine kwa mahesabu sio yote kwa pamoja.
Kisha baada ya Miaka kadhaa, tafuta kisichana kazuri kadogodogo,
Kwa Sisi Watibeli tunachukua Bikra Safi Kabisa k**a alivyokuwa yeye (Mke wa Awali).
Usijichukulie ilimradi. Onyesha wewe ni mwanaume wa thamani unayestahili vitu vipya na vizuri.
Wazee wako na mababu zako watakuwa very proud juu yako.
Nawe ukifa utakuwa Legend.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon Master.
Kwa sasa Dar es salaam
12/02/2025
"BORA NIISHIE JELA KULIKO NIKUACHE UISHI". Kuna cha kujifunza hapa
Veronika ndio jina alilokuwa anajiita mrembo huyo baada tu ya kufika mjini. alikuwa mwanamke mzuri mno pia mwenye uwezo wa kifedha kiufupi Veronika alijipata. hakuna aliyejua ametokea wapi wala kufahamu ndugu zake na hata mtaani kwetu alijulikana kwa jina moja tu la Veronika. Dada huyo alimiliki gari 2 za kutembelea, nyumba 1 na maduka 2 ya kuuza balo za viatu hapo mjini kenshansa.
Veronika alioneka sana sehemu mbali mbali za starehe huku akibadili wanaume kadri alivyopenda na alikuwa akitembea na mwanaume leo basi kesho awezi tena kukurudia kwamaana hakuona sababu au maana ya kugandana na mwanaume mmoja ka ruba. alitembea na vijana wengi sana na endapo ukafanikiwa kupelekwa kwake na kulala naye kwenye kitanda chake basi kuna uwezekano mkubwa sana ukapewa maisha na huyo dada japo umekutana naye siku hiyo.
Vujana wengi wenye tabia za U_marioo wajisogeza kwa mrembo huyo kwa lengo la kutafuta maisha bila kujua nyuma ya pazia kuna kitu gani au siri gani huyo dada anaitunza juu ya utajiri wake. haikuwa ngumu sana kukutana na Veronika kwani kila jioni ni lazima atapitia kwenye kumbi za starehe kusambaza upendo kwa vijana watakao bahatika kumuona au kukutana nao kwa siku hiyo.
Baraka ni miongoni mwa wavulana aliyeshiriki kimapenzi na mrembo Veronika na ishapita mienzi 3 sasa Baraka anasumbuliwa na tatizo la kusimama kwa uume (jogoo hapandi mtungi) yaani uume hauinuki kabisa hata k**a kitoga samaki mwenye nyama nyingi awe karibu yake kwa Baraka hatoweza kabisa kumtafuna samaki huyo. kutokana na shida hiyo kulimlazimu kijana huyo kufunga safari hadi Zambia ambapo ndio kwao ili kujaribu na tiba za nyumbani k**a ataweza pona.
Haikuchukua muda hadi mganga bingwa kabisa alipofikiwa na kijana huyo aliyeshindwa kuzicheza mechi za ugenini na nyumbani, mganga alipomuona kijana Baraka alionesha wazi shida ya kijana huyo ni kubwa na bila kuchelewa akaanza kumkagua kwa makini, baada ya muda kidogo mganga akaanza kuongea na kijana huyo. "sikia kijana wewe umekuta kimwili na mwanamke ambaye anajiweza sana kiuchumi na naamini umekutana naye mara 1 tu tangu umjue na yeye uchukua mbegu za mwanaume aliyefanya naye mapenzi kwa manufaa yake kimaisha. hivyo basi mbegu zako zimetolewa k**a malipo ya utajiri wake hivyo wewe uwezi simama tena hadi unakufa. Baraka alipiga magoti kuomba msaada kwa babu huyo ambaye alijulikana kwa Afrika kwa tiba zake
Tiba yako ni ngumu sana kijana na hii itapelekea vifo vya watu 7 kwenye familia yako pia hata tukifanikiwa kukurejesha k**a awali utoweza tena kumpa mwanamke ujauzito, kijana akiwa bado amepiga magoti machozi yalizidi kumbubujika kwa asira alizokuwa nazo. Mganga aliinuka toka kwenye kiti na kumuinua kijana na kumtaka asirudie tena kupiga magoti mbele yake. Mwishowe Baraka alitoka kwa mganga baada ya kujua jambo lake ni gumu kwani hakuwa tayari kuua familia yake aliyoipenda kwa ubaya aliofanyiwa na Veronika.
Baraka alijipanga vizuri kurudi Kenshansa kwa lengo moja tu la kulipoza kisasi kwa mwanadada mrembo Veronika huku akijiapiza moyoni mwake "BORA NIISHIE JELA KULIKO NIKUACHE UISHI"
MWISHO
06/11/2024
Kijana mmoja alifungua butcher ya nyama ya ng'ombe jirani kabisa na mitaa ya kwetu, hama kwa hakika watu tulimshangaa sana kwani ukata wa eneo letu sisi ndio tulikiwa tunaujua hivyo kwa kijana yule kuleta biasha ya nyama pale mtaani kwetu tuliona amejichanganya kwani tuliowengi pale mtaani tuna maisha magumu na ya chini sana hivyo kula nyama majumbani kwetu ilikuwa ni ubadhirifu wa fedha kiukweli.
Wiki moja baadaye kijana yule alichanganyikiwa kabisa kwani pesa ya mkopo aliyokopa ili afanyie biashara ndiyo hivyo kashaipoteza hana namna kwani toka ahamie pale mtaani hata kilo 3 hajauza na licha nyama kuiweka kwenye freezer imeshaanza dalili ya kuharibika anapoitoa nje ya jokofu, siku hiyo alikuja bibi mmoja akakaa nje ya butcher ya kijana huyo japo apumzike kabla ajaanza safari ya kwenda kwake
Kijana yule alimsalimia bibi yule hulu akionekana mwenye mawazo sana ili bibi yule alimuuliza mbona mjukuu wangu unaoneka huna kabisa furaha una shida gani, kijana akamwambia bibi nipo sawa ni biashara tu naifikiria, basi bibi akamwambia jikaze kijana wangu usisahau Mwenyezi Mungu yupo na wenye subra, kiukweli kijana alitiwa moyo kutoka kwa bibi yule na kabla bibi amwage kija aliingia ndani akamkatia bibi yule nyama robo na kumwambia bibi nenda hata angalau ukachomee hii, bibi aliipokea nyama ile akashukuru kwa kuinua mikono juu pamoja na ile nyama na kusema "MUNGU AKUZIDISHIE NA ABARIKI ULIPOTOA". Kisha akaondoka
Dakika 20 baada ya yule bibi kuondoka wateja walijaa kwenye butcher ya kijana yule wakigombea nyama na baada ya lisaa 1 nyama yote iliisha huku kijana akistaajabu kwa kilichotokea, kesho yake asubuhi na mapema aliwahi machinjioni akabeba nyama na kuwahi naho butchani k**a kawaida, cha ajabu ile anafika tu anamkuta yule bibi wa jana aliyepiga naye story amepumzika k**a kawaida, kijana alitua mzigo akamsalimu bibi kisha akafungua ofisi na kuanza kufanya usafi, baada ya muda bibi alimuaga kijana na kijana aliingia butchani kumkatia bibi nyama na tena leo akamkatia nyama robo akampa yule bibi, basi bibi akainua mikono juu na ile nyama akarudia maneno ya jana kisha akaondoka
Dakika chache kijana alijaliliwa na wateja akauza nyama yote na kumaliza hata akaagiza nyingine nayo ikaisha pia. Kiukweli tulianza kuogopa jinsi zile siku 2 alivyomaliza nyama kiajabu ajabu ila k**a ilivyo kaida Mungu achagui wa kumpa, hivyo tuliyaacha mambo ya Ngoswe.
Siku zilikimbia na biashara ya kijana huyo ilitaradadi hata baadhi ya watu walifika pale kufungua ma_butcher mengine ila hawakuweza fikisha hata wiki 1 walifunga. Kijana aliuza kilo 200 kwa siku za kawaida na siku za sikukuu hadi kilo 300, alipata oda nyingi za watu wa sherehe mbali mbali na misiba
Kila siku asubuhi bibi yule alifika pale butchani kuchukua nyama robo na kuondoka zake. Miezi ikapita kijana aliwaajili vijana wengine na akawa na gari ya kuleta nyama butchani, basi siku moja kijana yule asubuhi na mapema akiwa anafungua ofisi alimoita bibi yule bila kumpa salamu na kisha akatoka akamwambia "Bibi siku zote nakupa nyama bure hata siku moja ujasema kijana ebu leo kuchukua pesa hii, au unataka nifunge butcher" Bibi alinyamaza kwa muda kisha akamwambia "Mjukuu wangu mbona nami siku zote huwa nashukuru na kukulipa DUWAA kwa Mwenyezi Mungu, nakulipa malipo makubwa zaidi ya nikipokeacho" Kijana yule ali_panic akaanza toa lugha zisizo na staa kwa ajuza yule
Mwishowe akamwambia yule bibi "kwahiyo maneno yako utalinganisha na nyama ninayokupaga hadi useme unanilipa duwaa, saa njoo tuone hayo maneno yako k**a yatalingana uzito na robo ya nyama kwenye uzani" Basi bibi yule alijitahidi kupanda ngazi za pale nje hadi kuingia ndani na kweli yule kijana alichukua kikaratasi na kuandika "MUNGU AKUZIDISHIE NA ABARIKI ULIPOTOA" kisha akachora mikono ikiwa imenyooshwa juu k**a bibi anavyofanyaga akipewa robo ya nyama basi baada ya kuandika hayo maneno na kuchora kwa hasira akaiweka ile karatasi kwenye mzani sehemu ya kuwekea yale mawe ya uzito mbali mbali na kule kwenye bakuli au sinia akakata nyama inayolingana na robo akaweka, uwezi amini mzani uligona kuiinua ile karatasi ikabidi aongeze tena nyama kukata aweke ila wali karatasi ilikuwa nzito kuliko nyama aliyoweka mle kwenye sinia ambayo ilikiwa k**a kilo 2
Kijana haraka sana alitambua amekosea na machozi yakaanza kumtoka na kupiga magoti kwa yule bibi kuomba radhi na bibi alimnyanyua kijana yule na kumwambia "Binadamu tumeumbwa kukosea ila waomba toba ni kwa watu wenye hofu ya Mungu pekee nimekuelwa kijana wangu" Kijana alikata nyama nusu ak**apa yule bibi na bibi akaondoka. Kabla bibi ajaondoka kijana alimwambia bibi fika hapa kila siku hata usiponikuta kuanzia leo nitawaambia vijana wangu wakupe nyama nusu kila siku tafadhali bibi usihache kupita. Basi ile siku ndio ilikuwa ya mwisho kwa yule bibi kupita pale na yule kijana alipata somo kubwa sana juu ya ujio wa yule bibi kwenye maisha yake na toka hapo kijana akawa mtu wa misaada kwa waitaji wengi. MWISHO
05/11/2024
EPISODE 1. TUSICHOKE
Maisha ya wanaume wengi yamejaa siri nzito ambazo ukipata nafasi ukisikia siri za watu 10 au 8 basi hutotamani maisha ya hao watu na nina uwakika utainua mikono juu kuomba madhira hayo yasikukute kabisa.
Kijana Mashaka (30) anapigiwa simu na jamaa yake Dulla (36) wakutane stendi ili waeende kwa jamaa ambaye waliongea naye siku 3 nyuma kuhusu kukipata kihumbe cha kuleta fedha kwa njia ya kishirikina ya kwamba kimepatikana.
Mashaka hakutaka hata kumuaga mkewe kuwa anasafari ya nje ya mji badala yake anachukua begi na kutoka akiwa mtu mwenye hofu na mashaka k**a lilivyo jina lake, dakika 20 anakutana na Dulla na wote wanaulizana k**a kila mtu amebeba pesa la jambo lao baada ya hapo wanapakizana kwenye piki piki ambayo Dulla alitoka nayo kazini kwake na safari ya kuelekea chipolo polo inaanza.
Masaa 4 baadae kwa mwendo wa kasi wa piki piki wanafika nje ya hotel moja kubwa na kupaki piki piki yao na moja kwa moja wanaenda upande wa mgahawa k**a walivyokubaliana na mtu ambaye wamemfata kuwa wakutane sehemu ya chini ya hoteli hiyo ambako kuna mgahawa uliotulia. Dulla anachukua simu kupiga namba ya huyo na ghafla anatokea mzee mmoja anawapungia mkono na kuwataka wasogee alipo yeye, baada ya salamu mzee alijitambulisha yeye anaitwa Chandula (71) na yupo pale kwa kazi yao.
Vijana nadhani mambo yasiwe mengi bila shaka mmefika na na shilingi laki 4 tuanze jambo, wote wanaitikia ndio, basi Dulla anatoa bahasha iliyojaa maoko na kumkabidhi mzee, na bila kuchelewa mzee anawapa masharti ya kihumbe ambacho wamekitaka kuwa ni hatari kiasi gani wakienda tofauti. Vijana wangu kihumbe huyu unauwezo ukamtuma kazi yoyote na akaifanya kwa muda uliompangia anaweza kwenda bank yoyote kuchukua hela au duka lolote kwa masharti nitakayo wapa.
Baada ya mazungumzo machache wanainuka ili waelekee chumbani wakachukue kihumbe chao huku mzee Chandula akiwa amebeba bahasha yake, walipofika ndani chakushangaza Mashaka na Dulla hawakuwa wanaona kitu ijapokuwa mzee alikuwa anawaambia mali ndio hiyo hapo, walimueleza mbona hatuoni kitu mzee akashtuka na kuwatizama kwa makini kisha akatoa begi lake lililokuwa kitandani na kuchukua chupa ambayo ilikuwa na dawa akaimwaga chini kufanya duara kiasi k**a anakizungushia kitu na nyingine akawaekea kila mmoja kwenye kiganja cha mkono wa kulia na kuwataka wapake usoni wakianzia paji la uso kushuka chini.
Ghafla waliona kivuli cha mtu aliyekaa pasipo kumuona mtu kwenye lile duara la dawa. Ikabidi wamueleze mzee kuwa hawaoni kitu zaidi ya kivuli tu, vijana hilo sasa ni lenu mzigo ndio huo hapa biashara ishafanywa na katu pesa hairudi, basi ikabidi Mashaka na Dulla wamuombe mzee, wao watoke kidogo waongee jambo.....
22/05/2023
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian amesema jalada la uchunguzi wa tukio tata la Watoto pacha waliozaliwa kabla ya muda katika Kituo cha Afya Kaliua na mmoja wao kunyofolewa jicho la kulia na ngozi ya paji la uso, limekamilika na Watumishi wanne wa Kituo hicho watafikishwa Mahak**ani wakati wowote kuanzia sasa.
Akiongea na CG FM Dkt. Batilda amesema uchunguzi umebaini miili ya Watoto hao ilitunzwa katika chumba cha Wauguzi na sio katika wodi ya Wazazi k**a ilivyosemwa awali na Wauguzi hao.
RC Batilda amewataja Wauguzi hao kuwa ni Theresia Kakiziba, Asha Magidi, Paulo James na Benson Maikase na kwamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuwasimamisha kazi Wauguzi wengine wawili walioongezwa katika kesi hiyo.
Itakumbukwa tukio hilo lilitokea May 9, 2023 katika Kituo cha Afya Kaliua ambapo inadaiwa Mtoto mmoja kati ya wawili pacha waliozaliwa kabla ya muda na kufariki alinyofolewa jicho na kuondolewa ngozi ya paji la uso hali iliyozua taharuki iliyopelekea Familia ya Isaka Rafael kugoma kuzika miili ya Watoto hao hadi leo.
18/05/2023
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
amesema baada ya kufuatilia wamebaini kuna ukweli juu ya taarifa za miili ya Watoto njiti mapacha waliofariki Kituo cha Afya Kaliua kukabidhiwa kwa Wazazi huku Watoto wakiwa wameng’olewa macho, kukatwa ulimi na kuchunwa ngozi kwenye paji la uso.
Waziri Ummy amesema “Tumelifuatilia suala hili, kuna ukweli, Uongozi wa Wilaya ya Kaliua umeshaanza kuchukua hatua, baadhi ya Watumishi wa Afya waliomuhudumia Mama huyu wameshasimamishwa kazi, nakemea vikali kitendo hiki, ninamuagiza RMO Tabora kusimamia vyema Weledi, Maadili na Miiko ya Watumishi wa afya”
Sakata hilo limeibuliwa na Mzazi wa Watoto hao Kisaka Mtoisenga Mkazi wa Ushikola, Kaliua Tabora kupitia kwa Mwanamtandao maarufu na Mdau wa masuala ya Kijamii Malisa ambaye aliweka malalamiko ya Mzazi huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mzazi huyo amesema baada ya kupewa miili ya Watoto Watumishi wa Afya waliwaambia wakazike haraka kwakuwa Watoto njiti hawafanyiwi msiba na walipofungua box na kubaini miili imenyofolewa macho Watumishi hao wa Kituo cha Afya waliwajibu wakazike tu maana huo ni ushirika na hata walipoenda Polisi na kwa DC wa Kaliua waliambiwa wakazike tu kwakuwa ni ushirikina.
17/05/2023
kabla sijampokea Kristo niliishi maisha mabaya sana ambayo yalinifanya nizunguke kwa waganga wakienyeji na walozi kila uchwao, nilipenda sana ushirikina na maisha ya kutesa watu ila jambo kubwa nilikuwa natafuta pesa za mkataba
mwaka 2006 nikutana na mganga mmoja nchini malawi ambaye kwa sifa nilizopata juu yake niliamini mchezo umeisha, alikuwa ma sifa kibao ambazo zote nilizipenda ikiwemo kuua au kuzima kesi yoyote ile inayo kukabili, pia alikuwa bingwa wa kuweka tego kwa wanawake na zindiko za nyumba hata ulinzi wa kujikinga na watu nuksi na mwisho kutoa pesa za mkataba kwa siku 7 tu.
basi mtaalamu huyo alinifanyia mazindiko mawili kabla ajanipa hiyo dawa ya kupata pesa, kwanza kabisa nilipaswa kulala na mke wa mtu ambaye mumewe ni mchawi hatari na la pili kufufishwa na moshi mzito wa majani ya mlonge kwa masaa 6. basi nilielekezwa kijiji cha kwenda kukutana na wachawi hatari ambako naweza kumpata mke wa mtu ambaye mumewe ni mchawi gwiji. nilifika kwenye hicho kijiji na kwa bahati nzuri hicho kijiji kilikuwa na vilabu vya pombe kila kona na k**a unavyojua tabia ya walevi ukishamnywesha pombe unaanza pewa siri ya jambo lolote lile, kwangu aikuwa kazi ngumu sana kumpata mchawi anayeogopeka pale kijijini kwani siku ile ile hata kwa huyo mzee nilipelekwa na kiambiwa kuwa yeye ni muwindaji na kila siku lazima atoke alfajiri kwaajili ya kwenda kuwinda
niliweza tengeneza mazoea na mke wa mchawi huyo na japo huyo mchawi alikuwa ni mtu mzima sana ila alikaoa kabinti kadogo dogo hadi raha kwani kifuani kwa binti huyo alikuwa bado embe sindano zinanyonyeka kwa mabuda buda pia alibalikiwa nyama za kutafuna na ukabishiba bila ugali au wali yaani YALIYOMO YAMO
siku 2 baadaye mimi na yule mke wa yule mchawi tuliluwa marafiki sana kwani naye alikuwa anapenda sana maisha ya watu wa mjini na hapo kijijini alishachoka kuishi na yule mzee hivyo kwangu ilikuwa k**a namfundisha msichana aliyevunja ungo somo la reproduction. japo nilipewa kinga na mganga nisikutwe na majanga nitakapokutana kimwili na mke wa mchawi ila bado hofu kubwa nilikuwa nayo moyoni. tuliyapanga vizuri ya kwetu kwenda kuilipua kikamilifu amri ya 6 mimi na huyo mwanamke na kweli aliomba ruksa kwa mumewe kuwa siku ya kesho ataenda kumtembela mjomba ake mjini na bila hiyana alipewa ruksa na mumewe.
alfajiri na mapema mumewe alienda kuwinda k**a kawaida na sisi mida saa 2 asubuhi tuliwahi basi kwenda mjini, sasa picha linaanza nipo na mchuchu nyumba za wageni...
ITAENDELEA
17/05/2023
Nilikutana nae mara ya kwanza ndani ya Bajaj.Nikamuomba namba ya simu baada ya salamu na maongezi akanipa.
Tulipoachana nikampigia simu baada ya siku 2-3 nikamueleza ukweli kuw nmemuelewa na kumpenda.Baada ya mvutano wa siku nyingi hatimaye akanikubalia ombi langu.
Siku zilivyoenda nikashangaa haniombi hela wakati ananitembelea umbali mrefu kwa nauli yake kuja kuniona.
Siku moja akanitumia ujumbe kwa Mara ya kwanza akasema-:
"Baby nina shida na shilingi 15,000/= nahitaji kwenda saluni wiki ijayo nimeona nikujulishe mapema ili ujiandae taratibu"
Kwakuwa pesa nilikuwa nayo na sio kawaida yake kuniomba nikazama mfukoni nikamtumia 50,000/= kwenye namba yake akanijibu-:
"Baby asante nimepata ila nimekuomba 15,000/= inanitosha nakurudishia 35,000/= iliyobakia ili uendelee kuizungusha kwenye biashara itusaidie wote hapo baadae"
Kabla sijamkatalia kurudisha hela ujumbe ukaingia kwenye simu yangu kuwa nimepokea 35,000/= toka kwa Catherine.
Nilishikwa na mshangao aliponiambia anahamu ya kukutana na Mimi maana tokea tufahamiane sijawahi kumhitaji faragha kwa hiyo 10,000/= inamtosha saluni na 5,000/= atatumia kwa nauli ya kuja kwangu na kurudi kwao.
Wakati najiandaa kumpa ratiba ya mtoko ghafla nikatoka kwenye ndoto hii ya ajabu.
Naamin ndoto yangu itatimia siku moja😂😂😂😂😂
Kinadada neno moja kwenye ndoto yangu😂😂🏃🏃
SHARE kwenye magroup matano ebu na wenzio wacheke😁😁😁💪
17/05/2023
Kutoka kwa Malisa GJ
Naitwa Kisaka Mtoisenga, mkazi wa Ushikola, Kaliua, Tabora. Tarehe 9/05/2023 saa 4 usiku mke wangu alijifungua watoto wawili mapacha kituo cha afya Kaliua. Watoto walizaliwa njiti (premature) na miezi 7 lakini tunamshukuru Mungu walizaliwa salama.
Kwa kuwa kituo cha afya Kaliua hakina uwezo wa kuhudumia watoto njiti wakatupa rufaa kwenda hospitali teule ya wilaya (Mission) yenye mashine za kuatamia watoto njiti (Incubators). Kituo hakina gari la wagonjwa, hivyo wakatuambia tukatafute usafiri.
Nikamuacha mke wangu na watoto wakiwa wazima wa afya, nikaenda kutafuta usafiri. Muda huo haikua rahisi kupata gari, nikapata Bajaji. Tulipofika wahuhudu wakasema tusubiri wawaandae watoto. Tukasubiri hadi saa 5 dereva akaanza kulalamika. Wahudumu wakasema tuendelee kusubiri. Ilipofika saa 6 dereva akataka kuondoka. Nikasema akiondoka sitapata Bajaji nyingine usiku huo. Nikawauliza wahudumu wakasema wanamalizia kuwaandaa watoto.
Nimwambia dereva nitamuongezea hela asubiri kidogo. Baadae wahudumu wakatoka na kutuambia bahati mbaya watoto wamefariki. Wakasema watatupa maiti kesho yake asubuhi.
Asubuhi wakatupatia maiti zikiwa ndani ya mabox, kwenye chumba maalumu cha upasuaji, ambacho kina giza. Wakatusisitiza tukazike siku hiyohiyo kwa haraka kwa sababu watoto njiti hawafanyiwi msiba.
Tulipofika nje kabla ya kupanda gari tukafungua mabox. Tukakuta watoto wameng'olewa macho, wamekatwa ulimi na wamechunwa ngozi kwenye paji la uso. Tukahamaki. Tukarudi kuuliza nini kimetokea, hawakutupa majibu ya kuridhisha.
Tukaenda Polisi, lakini wakatuambia tukazike tu maana wao hawashughuliki na ushirikina. Tukaenda kwa Mkuu wa wilaya, alipoona maiti akasema huo ni Ushirikina. Akatushauri tukazike tu maana hata tukienda mahak**ani hatuwezi kushinda. Nikamuuliza kwanini ushirikina ufanyike hospitalini? Nikakataa kuzika.
Nikataka uchunguzi ufanyike. DC akaagiza maiti zipelekwe hospitali ya Urambo. Hadi leo zipo huko sijui nini kinaendelea. Naomba unipazie sauti Rais asikie. Watoto wangu wametendewa unyama kwenye kituo cha afya, halafu nanyimwa haki kwa kisingizio cha ushirikina? Naumia sana.
Mtag Mhe.Rais na viongozi wengine wanaohusika ili wachukue hatua.!
14/05/2023
watu wengi upenda kuyafananisha na asali mapenzi yanapoaanza na yanapoenda mlama ufananisha na shubiri. vile kila mmoja anavyomchukulia wa muhimu mwenzie hata kuboleka kwa dk 5 asipomuona hama kumsikia, kuna texts nyingi sana za emonj makopa kwa penzi jipya hata utani wa hapa na pale, bila kusahau ubunifu utasikia 'nakuomba uende kazini usije nilaza njaa' hata na kuelezea maisha yao ya usoni.
kwa muda hali hii unza kukifu na kujenga mazoea ya kupuuza vitu vidogo vodogo 'leo ulienda kazini?'. mwanaume anakuwa kwenye wakati mgumu sana akiamini mapenzi yameisha huku akirudisha kumbu kumbu za mahusiano yake ya nyuma yalivyopotea kwa kunyang'anywa tonge na muuza genge wa mtaa wa pili halikadhalika hali hiyo hiyo umtesa mwanamke akiamini ameshachezewa na kuachwa k**a mwanzo na yule mkaka muuza chips baada ya kutoka na rafiki yake Coletha
hacha niongee kitu hapa, kweli kunakuchokana kwenye mahusiano ila ni hatari kufanya jambo kwa mazoea naomba nitoe mfano:-
kuna mtu alitabiliwa kuwa tajiri baada ya miezi 2 ila utapotea baada ya wiki 2 na aliambiwa k**a utataka utajiri wako hudumu kila unapoingia kitandani kulala sema "AHSANTE EE MWENYEZI KWA YOTE" kwa siku za mwanzo lilikuwa ni jambo dogo sana kusema hivyo ila baada muda alipofika kitandani alisema "E MUNGU K**A JANA" yaani aliona kero kushukuru na kuona taabu kurudia rudia hivyo na mwisho akaleta mazoea na hatimaye utajiri ukayeya.
kubali kujishusha ukibaini kuna tofauti pia kuwa mpole na msikivu mwenzio anapolaumu au anapocomment jambo fulani, mfanyie out k**a za mwanzo mpenzi wako k**a za mwanzo huku ukimletea zawadi hata za shilingi 500 kuonesha umemkumbuka, jitaidini kutiana moyo kwenye utafutaji na changamoto za maisha ila kubwa jifunze kumuelewa mwenzio.
hakuma mtu sahihi aliye andaliwa kwa ajili yako ila yupo mtu anayekubali kuishi na wewe kwa jitihada zako