Mwandishi wa habari za michezo za kitaifa na kimataifa.
Manothu.com
PATA HABARI ZA SOKA ZA HAPA BONGO NA ULAYA HAPA
Kupitia ukurasa huu utaweza kujipatia habari mbalimbali za soka kutoka hapa nyumbani na zile za majuu katika ligi kubwa ulaya>>>LIKE PAGE HII KUYAPATA YOTE HAYO.
OZIL: FURAHA YETU NI KUWA JUU YA TOTTENHAM.
📝Lotti Junior.
Mchezaji nyota wa klabu ya Arsenal fc ya jijini England amesema wanafuraha kuwa juu ya Tottenham katika kipindi ambacho mbio kuelekea mwisho wa msimu katika ligi kuu England zinazidi kupamba moto.
Washika mitutu hao waliwabamiza Newcastle hapo jana (jumatatu) na kuweza kuwapiku mahasimu wao kutoka London(Spurs) katika nafasi ya tatu.
Spurs wamedumu kwa muda mrefu katika nafasi ya tatu na kuonekana k**a ndio washindani wakuu wa Liverpool na Manchester city katika mbio za ubingwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Lakini kwa sasa klabu ya Arsenal imeweza kugeuza meza,na kiungo mshambuaji Ozil ni mwenye furaha sana kuwa katika nafasi ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya kuelekea ukingoni mwa msimu huu.
"Mipango yetu ni kuwa katika klabu nne za juu, hakika tunafuraha sana kwamba tupo juu ya Tottenham. Mara zote tuna ushindani mkubwa nao" Ozil akielezea baada ya ushindi wa hapo jana.
"K**a tutacheza k**a leo,tuna mechi chache usoni na tunataka kushinda.Tunataka kuchukua alama zote na kuingia katika nne bora mwishoni mwa msimu".
©2019
24/03/2019
Miamba wa Soka Nchini Morocco, klabu ya RSB Berkane Imethibitisha kumsajili Mshambuliaji hatari wa Kimataifa wa DR Congo na Klabu ya AS Vita Club, Jean-Marc Makusu Mundele, nyota huyo atajiunga na wababe hao baada ya msimu huu kumalizika.
- Mundele 26, Mshambuliaji mwenye nguvu, ujanja na akili nyingi ndani ya dimba amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Vita Club chini ya kocha Ibenge.. Lakini dau La uhamisho €430,000 sawa na zaidi ya Bilioni 1 na 138m za kitanzania zimefanikisha usajili wake kwenda uarabuni kwa Mara ya tatu baada ya mwaka 2017 kuitumikiaWadi Degla SC ya Misri na Mwaka 2015 aliitumikia MC Oran ya Algeria kwa mkopo akitokea Standard Liège ya Ubelgiji.
- Vita Club wameanza kutafuta Mchezaji ambaye atakuja kuziba nafasi yake ndani ya kikosi hicho, na anaetajwa zaidi ni Mshambuliaji hatari wa klabu ya GOR Mahia na timu ya taifa ya Rwanda, Jacques Tuyisenge.
22/03/2019
MBAO YAIMARISHA BENCHI LAO LA UFUNDI
:
Mbao FC imemuongeza Kocha Fulgence Novatus kwenye benchi lao la ufundi k**a kocha msaidizi ili kuongeza nguvu na kujaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi tangu mwanzo wa msimu huu wa ligi. Na hii ni siku moja baada ya kumtangaza Kocha Salum Mayanga k**a Kocha mkuu wa kikosi hicho ambaye ndio amempendekeza Novatus kuwa msaidizi wake.
:
Fulgence Novatus alipata kuifunsisha Mbao FC msimu uliopita kwenye kipindi cha mwisho wa msimu baada ya kuachana na Kocha Etienne Ndayiragije.
22/03/2019
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda (FUFA), limemtangaza Samuel Fabin Kwesi raia wa Ghana kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na miaka 20.
:
Fabian Kwesi atakioongoza kikosi cha Uganda U-17 katika fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Tanzania Aprili 14 - 28.
21/03/2019
Leo vimezaliwa hivi vyuma, Siku ya Washindi hii leo🏆💪💪
21/03/2019
BREAKING NEWS:
:
Uongozi wa Mbao FC umefikia makubaliano na Kocha Salum Mayanga kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.
Kabla ya kutua Mbao FC, Mayanga ameshawahi kufundisha Timu ya Taifa na Mtibwa kwa mafanikio.
20/03/2019
Ligi ya Mabingwa Barani AFRIKA | Drop ya Hatua ya Robot Fainali:
♦QF1 : CS Constantine 🇩🇿 - 🇹🇳 Espérance de Tunis
♦QF2 : Mamelodi Sundowns 🇿🇦 - 🇪🇬 Al Ahly
♦
QF3 : Horoya AC 🇬🇳 - 🇲🇦 Wydad Casablanca
♦QF4: Simba vs 🇨🇩Tpmazembe
.
20/03/2019
CAF CONFEDERATION CUP
Quarter-Finals
Nkana FC 🇿🇲 vs 🇹🇳 CS Sfaxien
Etoile Sahel 🇹🇳 vs 🇸🇩 Al Hilal Club
Hassania Agadir 🇲🇦 vs 🇪🇬 Zamalek SC
Gor Mahia FC 🇰🇪 vs 🇲🇦 RS Berkane
1st Leg - 7th April, 2019
2nd Leg - 14th April, 2019
20/03/2019
FC Barcelona wameripotiwa kuwasilisha ofa ya Euro Milioni 60 kwa Ajax kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati Matthijs de Ligt. kwa mujibu wa taarifa kutoka Sport.
Barcelona wanaamini kwamba wanaweza kufanikisha dili hilo la kumnasa Matthijs de Ligt ndani ya kipindi cha mwezi mmoja .
Barca wamewasilisha ofa ya Euro Milioni 60 pamoja na bonasi na mkataba wa miaka mitano kwa mshahara sawa na ule atakaopewa Frenkie de Jong kiungo huyo ambaye dili lake la kwenda limekamilika.
20/03/2019
Ndani ya U LIVE ya 107.3 U FM with supero brother 🔥🔥
:
U LIVE inakuwa hewani kila siku majora ya saa tisa kamili mpaka saa moja. Si Ya Kukosa Hii.
15/10/2018
Usiache kuisikiliza ya 107.3
Hapa inazungumzwa kila taarifa ya kispoti unayohitaji kuisikia. 🔥🔥
Click here to claim your Sponsored Listing.