13/12/2025
🕊️ Taarifa ya Masikitiko | Soka la Afrika Limeguswa
Klabu ya Yanga na familia ya soka kwa ujumla imepata pigo kubwa baada ya kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa nyota wao wa zamani, Chico Ushindi, aliyefariki leo akiwa nyumbani kwao Lubumbashi – DR Congo 🇨🇩.
Chico atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alipokuwa akiitumikia TP Mazembe, baadaye Yanga SC, na hivi karibuni akiwa mchezaji wa FC Bazano ya Ligi Kuu ya Congo.
Kifo chake ni pengo kubwa katika soka la Afrika.
Pumzika kwa amani, shujaa wa soka. 🤍⚽
13/12/2025
UPDATES : Akili kubwa, Simba SC mnaweza kuanza na huyu, Nermin Basic ( ) raia wa Bosnia, mpeni mpunga aje kusuka mpango k**a Mkurugenzi wa ufundi (Technical Director )
Katika klabu yenye bajeti ya kati, TS Galaxy huwa inawapa mechi ngumu wote wa Afrika Kusini, mechi ya mwisho ni juzi tu walitoka 0-0 na Kaizer Chiefs, sasa fikiria akija kwenye klabu ya Simba, kwa Ligi yetu unadhani uteja wa Mnyama utaendelea?
Kimsingi huyu ni kocha lakini ili kwenda kisasa, Simba impe jukumu hilo ili kuwachorea mchoro mzima wa soka la kisasa.
Waiteni viongozi wa Simba hapa, waambieni ubongo wa soka upo hapo.
13/12/2025
Mshambauliaji wa klabu ya Simba Seleman Mwalimu (19) amechaguliwa kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kuelekea AFCON 2025.
Mwalimu amechukua nafasi ya Abdul Seleman Sopu (24) ambaye ameondolewa kikosini baada ya kupata majeraha.
11/12/2025
Ikiwa Nimueendelezo wa timu za Afrika kuita wachezaji watakao wakilisha nchi zao kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON 2025) itakayochezwa nchini Morocco, Taifa la Zambia wamebisha hodi mara nyingi kwa mchezaji kinda wa Manchester City Jadie Katongo ambaye ana uraia wa nchi ya Uingereza lakini pia anaweza kuitumikia Zambia kutokana na baba yake ni mzaliwa wa Taifa hilo.
Alipo Itwa hivi maajuzi alisema, kwa sasa hatoitumikia Zambia hadi hapo atakapokuwa mkubwa na hajaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa la Uingereza.
"Nitakuja Tu Kuichezea Zambia Nikiwa mkubwa alafu Uingereza iwe Imenikataa," alisema Jadiel Katongo wa Manchester City alipokataa kuitwa kwenye kikosi cha Chipolopolo cha AFCON.
11/12/2025
MARTIN ZUBIMENDI, MAHUSIANO ANAYAFICHA ZAIDI YA NYETI YA ALBINO.
---------------------------------------------------------------
Paundi million 55 zilimtoa "Anoeta" uwanja wa Real Sociadad. kwenda "Emirates stadium" akiwa k**a mpagani asiyefahamu chochote kuhusu ibada za soka la England.
Safari ya kwenda Arsenal ilikuwa kufuata utakaso wa kiroho. Awe sehemu ya waumini kwenye maombi ya kuvunja laana na mikosi. Ya the gunners kutoshinda mataji.
Arsenal ilimpokea k**a muumini mgeni, anayemiliki ubongo uliokosa mafundisho ya utatu mtakatifu wa soka la kiingereza. Yaani nguvu, kasi, na uharaka wa kutafsiri matendo ya hisia za ubongo.
Ubatizo wa maji mengi kupitia mikono ya padri "Mikel Arteta." Hii ni sakramenti iliyomtakasa miguu akaingia haraka kwenye mfumo.
Kwa sasa Zubimendi ameiva. Lile ni toleo jipya la "defensive midfielder" aliyeitwa kwenye wokovu wa kisoka.
Google wanasema: Zubimendi ni moja kati binadamu aliyebarikiwa miguu yenye pua za ajabu. Linapokuja suala la kusoma mikimbio ya wenzie pamoja na kunusa njia sahihi za mpira."
Umri wa Zubimendi ni miaka 26 sasa. Alizaliwa Hispania April 2, 1999. Sehemu inayoitwa "San Sebastiàn" eneo linalovuna sifa kwa kumiliki beach bora, inayokutanisha binadamu waliofaulu somo la jinsi ya kuishikisha adabu pesa."
Zubimendi ni mtoto pekee kwa wazazi wake. Baba yake Zubimendi ni "physical education lecturer," na kocha wa mpira kwa timu za madaraja ya chini. Wakati mama wa Zubimendi ni mwalimu.
Ule upole alionao Zubimendi haukuja k**a zawadi toka mbingu ya 7. Bali utotoni mkazo wa mama yake, ulimtaka atangulize utu na ubinadamu ndani ya kiwanja.
Nidhamu na somo la unyenyekevu. Vibaki kuwa nguzo muhimu hata timu yake inapopoteza."
Makuzi mema toka kwa wazazi sahihi. Yamemtengeneza awe ndani ya daraja la nidhamu ya upekee. Katika career yake hakuna aliyewahi kujua Zubimendi anatoka na nani?! Mahusiano yake huwa anayaficha zaidi ya nyeti ya albino."
Imeandikwa na BABRY SPORTS HQ
11/12/2025
Mecky Mexime baada ya kuingia Mbeya City amependekeza majina ya wachezaji wa Simba Mzamiru Yassin na Awesu Awesu ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Viungo hawa wote wawili wapo kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Awesu ilikuwa aondoke dirisha kubwa kwenda Jkt Tanzania lakini Fadlu akahitaji asalie zaidi kikosini hapo.
Kuongezeka kwa jina la Kulandana inawezekana Mbeya City wakamuongeza mchezaji mmoja tu kati ya hawa.
11/12/2025
👋🇩🇪Mpira umeanza kumuacha, Mwili umeanza kukataa yanayopanga akili...Anaitwa Antonio Rudiger.
ila kile chobo/Nyobo aliyopigwa na Cherki, duh😅mpaka mwenyewe akacheka
11/12/2025
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Hoteli ya Jewel, Misri kujiandaa na Fainali za AFCON 2025, Morocco
11/12/2025
UCHAMBUZI WA GEORGE AMBANGILE
✍🏻Timu mbili ambazo zilikuwa na maono tofauti tena katika sura zote mbili ( yani kushambulia na kuzuia ) .
1: Azam FC :
A: wao ni kutumia maeneo ya pembeni , kufanya uwanja uwe mpana na kutenengeza idadi kubwa ya wachezaji pembeni ( wide overloads ) akijumuika na namba 10 wao Feisal .
B: Na hata kiulinzi walihakikisha : Vertical na Horizontal hakuna space kwa Simba kuitumia vizuri ( mistari yao yote mitatu ipo karibu karibu sana hasa kipindi cha pili .
2: Simba SC :
A: Wao wanatumia sana maeneo ya ndani ( central areas ) wingers wawili kuingia ndani wakiungana na namba 10 wao dhidi ya viungo wawili wa kati ( Himid & Kanoute ) kipindi cha kwanza Simba walipatia sana kilochokosekana ni action bora ya mwisho pale ambapo wanakuwa nyuma ya kiungo cha Azam .
B: Wakizuia Simba bado wanakuwa ndani sana kiasi kwamba Azam wakifanya tu Switching of Play wanakuwa na hatari au namba 10 wa Azam akihamia pembeni kidogo tu ( drifting wide ) kutoka kwa Kante & Kagoma , Simba wapo matatizoni .
✍🏻Tofauti kubwa ya kipindi cha pili ipo kwenye maeneo matatu
1: Azam kiulinzi waling'amua mapema nguvu ya Simba ilipo na kuifanyia kazi , kufunga spaces kwenye halfspaces
2: Simba level ya Intensity ilishuka sana hasa bila mpira , recovering ilikuwa slow , spaces zikaanza kuwa kubwa na nyingi
3: Movements za wachezaji wa pembeni wa Azam , namba 10 wao na passing game ya Akaminko ( Forward passing )
4: Finishing ya Azam , Top Class .
NOTE
1: Foba kuonesha mamlaka golini pale alipohitajika
2: Mpanzu alionekana kuwafikirisha sana wachezaji wa Azam hasa kwenye mpambano wowote wa mmoja Vs mmoja
3: Himid aligoma kuwa abiria uwanjani
4: Morice muda wote yupo kwenye space na kutunza mpira vizuri
5: Feisal alihakikisha space Simba waliacha kipindi cha pili walipe gharama kubwa
6: Movements na Finishing za Kitambala na Nado🔥
7: Saadun wingplay yake 🔥 Top . Angekuwa makini basi hat trick ya assists
FT: Simba SC 0-2 Azam FC