Coach Jointy Himself

Coach Jointy Himself

Share

FOOTBALL IS OUR LIFE

19/02/2026

Manchester United

19/02/2026
03/02/2026

With Manchester United – I just got recognised as one of their top fans! πŸŽ‰

31/01/2026

β—β—β—π“π„π“π„π’πˆ 𝐙𝐀 π”π’π€π‰πˆπ‹πˆ ππ€π‘π€ππˆ.π”π‹π€π˜π€

🚨 Maskauti wa Manchester United wanamfuatilia kwa karibu Iliman Ndiaye. πŸ‘€

Mshambuliaji huyo wa Everton ana wapenzi wengi ndani ya Old Trafford huku United wakilenga zaidi wachezaji wenye uzoefu wa Premier League.

Hatua yoyote inaweza kutegemea kocha atakayeteuliwa kuinoa timu ya kwanza, huku Ndiaye pia akivutiwa na klabu kadhaa baada ya kung’ara na Senegal kwenye AFCON. πŸ‡ΈπŸ‡³

Chanzo: TEAMtalk

🚨 Barcelona wamefikia makubaliano kumsajili beki wa Genk mwenye miaka 18, Juwensley Onstein. Tayari amepita vipimo vya afya (medical).

Barcelona wamewashinda AC Milan katika mbio za kumsaini.

Chanzo: SPORT

🚨 Nottingham Forest wako kwenye mazungumzo kumsajili kipa wa Wolves, José SÑ.

Hatua hii inakuja baada ya kuthibitika kuwa John Victor ataikosa sehemu yote iliyobaki ya msimu kutokana na jeraha la goti.

Chanzo: BBC Sport

🚨 Barcelona wanamfuata beki wa kati mwenye miaka 18, Ruud Nijstad kutoka FC Twente.

Atakuwa kipaji cha tano kusajiliwa dirisha hili na beki wa tatu wa kati mwenye mguu wa kushoto, jambo linaloonyesha namna Barcelona wanavyofanya scouting barani Ulaya kwa sasa.

Chanzo: Diario Sport

🚨 𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š: Fulham wamekubaliana dili ya pauni milioni 27 na Manchester City kumsajili Oscar Bobb.

Chanzo: Sky Sports Football

🚨 Moussa Diaby tayari ameonyesha mwanga wa kijani kujiunga na Inter. 🟒

Uhamisho huo ungekuwa wa mkopo kutoka Al-Ittihad ukiwa na kipengele cha kununua cha €35M, na sasa unategemea msimamo wa Al-Ittihad kuhusu muundo wa makubaliano.

Chanzo: Fabrizio Romano

🚨 Chelsea wanapanga kumsajili JΓ©rΓ©my Jacquet. πŸ”΅πŸ‡«πŸ‡·

Maendeleo yamepatikana upande wa mchezaji, huku mazungumzo yakiendelea na Rennes. Klabu ya Ufaransa haitaki kuuza Januari lakini inaweza kushawishika kufanya dili la mapema kuelekea majira ya joto β€” na Chelsea wanajaribu kulazimisha makubaliano yapite.

Liverpool pia wapo kwenye mbio na wamezungumza na mawakala wa mchezaji. Bayern pia wamewasiliana, lakini klabu za Premier League ndizo zilizo na makali zaidi kwa sasa.

Chanzo: Fabrizio Romano

Uamuzi huo unakuja baada ya mazungumzo yasiyozaa matunda ya kuongeza mkataba kati ya mshambuliaji huyo wa Kifaransa na klabu.
Ilikuwa ni ombi la Benzema mwenyewe, si uamuzi wa SΓ©rgio ConceiΓ§Γ£o.

Chanzo: Ben Jacobs

🚨 Juventus wanaongeza juhudi ili kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27, Randal Kolo Muani, ambaye yuko kwa mkopo Tottenham kutoka Paris St-Germain, na Spurs wanaweza kumuangalia mshambuliaji wa Crystal Palace wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta (28) k**a mbadala iwapo Muani ataondoka.

Chanzo: Mail

🚨 Mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee pia ni chaguo kwa Juventus, huku Manchester United wakiwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye miaka 24 kuondoka kwa mkopo.

Chanzo: Gazzetta dello Sport

🚨 Manchester United pia wanatafakari mustakabali wa Harry Maguire. Klabu haijafanya mazungumzo makubwa ya mkataba na beki huyo wa England mwenye miaka 32 ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu. Timu za Italia na Uturuki zimewasiliana na wakala wake.

Chanzo: The Athletic

🚨 Saudi Pro League inapanga kumsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Ousmane Dembélé (28) baada ya Kombe la Dunia lijalo

Chanzo: Sky Sports

🚨 PSG wameanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba kocha Luis Enrique, ambaye mkataba wake wa sasa na mabingwa wa Ulaya unaisha mwaka 2027.

Chanzo: Le Parisien

🚨 Kiungo mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz (20) ameunganishwa na klabu kadhaa za Premier League lakini yuko karibu kuongeza mkataba wake na Juventus.

Chanzo: Sky Sports Germany

🚨 Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa Ujerumani Leon Goretzka, ambaye mkataba wake na Bayern Munich unaisha majira ya joto, na mchezaji huyo mwenye miaka 30 anafikiria ofa hiyo.

Chanzo: Sky Sports Germany

🚨 Fiorentina waliopo kwenye hali mbaya Serie A wamewasiliana na West Ham kuhusu kumsajili beki wa England Kyle Walker-Peters (28) na kiungo wa Kifaransa Soungoutou Magassa (22) kutoka kwa The Hammers.

Chanzo: Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia

🚨 Bournemouth wako kwenye mazungumzo na Inter Milan kuhusu kumsajili winga Luis Henrique (24).

The Cherries wanapendekeza mkopo wenye kipengele cha kununua cha karibu pauni milioni 18 kwa Mbrazil huyo.

Chanzo: Talksport

🚨 Jesse Lingard (33) yuko kwenye mazungumzo na klabu za England na Italia. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United mwenye mechi 32 yuko huru baada ya kuondoka FC Seoul mwezi Desemba

Chanzo: Mail+

🚨 River Plate wamekubali dili kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea na Ecuador Kendry PÑez (18) ambaye alitumia nusu ya kwanza ya msimu huu Strasbourg kwa mkopo.

Chanzo: Fabrizio Romano

🚨 AC Milan wanatafuta beki na wanaweza kumlenga Radu Dragusin wa Tottenham. Mchezaji huyo wa Romania mwenye miaka 23 pia anafuatiliwa na Roma na Napoli.

Chanzo: Calciomercato

Jointy Johnson Jonathan John

26/01/2026

Goalkeeper BORA ni yupi kwako?
A..anayeanzisha mashambulizi nyuma lakini hadaki vizuri
B.. anayedaka lakini hana footwork nzuri..

KARIBU KATIKA MJADALA

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address

Namanga Tegeta
Dar Es Salaam