Gamba Buzness

Gamba Buzness

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Gamba Buzness, Dodoma.

12/08/2025

Bwana kaa nami siku zote.

Photos from Gamba Buzness's post 12/12/2018

It's all about breakfast you're welcome
@ Dodoma, Tanzania

Photos from Gamba Buzness's post 30/11/2018

Saladi on point

14/11/2018

Kuku tym

20/03/2018

MWANAUME MWENYE MALENGO NA WEWE UTAMTAMBUA KWA HAYA

Nimekuwekea hapa zisome Tabia za mwanaume mwenye malengo na wewe.

1. Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.

2. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu.

3. Anawapenda ndugu zako k**a ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!

4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi k**a kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu!

5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni bonge la bwana.

6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!

7. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.

Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina hii.

Hao wenye sixpack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa milegezo, wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, waume za watu, masupa staa, watoto wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.

Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hzo pesa zake, hivyo na wewe unajiongeza kwenye foleni!

Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto njema, mapenzi ya kweli ni vigumu sana kuyapata. Ila pesa na mali ni rahisi sana kuzipata k**a utajibidiisha.

Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! - Ukishikwa shik**ana, ukipendwa, pendeka!

Mwisho ndoa ni muhimu na Uzingatie mipaka ya Dini yako usijekuingia kwenye makosa.

17/11/2017

"Hua kuna muda MUNGU anamruhusu Huyo mtu uliempenda sana akuteme/akuache ili uweze kujikusanya vyema, ukaanza ku-focus upya na kufanya assesment ya maisha yako. Sio mahusiano yote lazima yaishie NDOA. Mengine ni kutufundisha ni namna gani tunatakiwa kuwa SMART linapokuja suala la kuwa na partner. SEPARATION IS NECESSARY FOR ELEVATION. You know am right!!!! 🔥🔥🔥🔥 🍹🍹🍹💯💯💯"

03/11/2017

Sio kila mwanamke mwenye utajiri au kipato kikubwa ni mchunaji. Baadhi ya wanawake ni Malikia wanaojitegemea. Wanapata pesa yao halali kwa kazi halali za mikono yao. Wanazichanga na wanatumia kwa uhuru zaidi, they earn it and slay it...Cheers kwa kila mwanamke afanyae kazi kwa bidii...msivunjike moyo sweethearts. Fire power...🔥🔥🔥💯💯 😍😍😍😍

23/10/2017

Y.O.LO: Hakuna kitu kinachoudhi na kuchanganya k**a kuwa katika ndoa au mahusiano na mtu ambae hana uhakika ni nini haswa anataka.

Unakuta kuna muda anaonesha kukupenda kweli, then baadae unakuta mtu huyohuyo anakufanya ujihisi hupendwi. Mtu anakuacha halafu baada ya kujitahidi kuendelea na maisha yako anarudi na kukuomba mrudiane.

Mtu anakwambia kabisa it's over, lakini baadae anakuita eti muyajenge. Mtu yuko na ndoa kabisa ila anajifanya yuko Single. Mtu kwa muda mfupi tu anabadilika kutoka "Nakupenda sana" kwenda "nakuchukia sana". Anakufanya unajisikia vizuri kidogo tu anakunadilikia..ni mbaya zaidi k**a umezaa na mtu wa aina hiyo ambae haeleweki.

Huu upuuzi wa kutokueleweka kwenye mahusiano ni utoto. Mtu ambae amekua kiakili anahitaji uhakika. Mtu aliyekua kiakili anaeleza wazi k**a mahusiano yapo au hayapo. Kuwa na uhakika na maamuzi yako kuliko kupotezeana muda.

Acha kumchezea michezo ya kitoto mwenzako. Chagua moja k**a upo kwenye uhusiano nae au laa. Usiwe mguu mmoja ndani mguu mmoja nje. Mapenzi sio moody. Mapenzi ni kitu ambacho kipo constant. Mapenzi yanatabirika na yanayotegemeana. Mapenzi ni facts sio theory. Mpe mtu clarity kuhusu mahusiano yenu.

Ndoa imara na Mahusiano imara hayajengwi kwa misingi ya mapenzi yasiyo na uhakika. Mtu uliyenae anaweza kabisa kukubaliana na matokeo. K**a haumtaki tena mweleze wazi ili afahamu amesimama wapi. Ni bora kukataliwa sasa hivi ukaendelea na maisha yako huku ukijitahidi kutibu moyo, kuliko kuendelea kusalitiwa na mtu ambae hafahamu ni nini anachokitaka.

09/10/2017

Pamoja kwa sasa ni mkeo ila ni mtoto wa familia nyingine na nidada wa watu wengine, hivyo jitahidi kumuheshimu na kumjali k**a ambavyo familia yao ilivyokuwa inafanya.. huna mamlaka ya kutokumuheshimu kwa sababu umemuoa....
🔊 Badala yake waoneshe unamjali na kumuheshimu mara dufu.

06/10/2017

Katika kizazi cha leo, ukiondoa S*x katika mahusiano utagundua kuwa asilimia kubwa ya wanaume hawana jambo lingine la maana la kuwepo katika mahusiano.

Vilevile ukiondoa pesa utagundua asilimia kubwa ya wanawake hawana jingine wanalohitaji katika mahusiano. Bila pesa Asilimia kubwa ya wanawake wataona haina haja ya kuwa katika mahusiano.

Na bila S*x, utagundua kua wanaume haoni haja ya mahusiano.

Namnukuu dada mmoja hivi, aliongea haya; "Sisi wanawake tunataka Boyfriends wetu watutunze, lakini hakuna cha thamani tunachokiongeza katika maisha yao zaidi ya kuwapa s*x tu...."

Wanawake nao wanalalamika kwamba wanaume wanapenda sana s*x basi, wakishapata s*x wanawakimbia na ule upendo waliokua wakiuonesha unapoa.

Ni wakati wetu sote kubadili mtazamo. Wanaume wengi siku hizi wanalalamika sana kwamba mnapenda pesa, sio wote ila baadhi yenu ni kweli mmeweka pesa kipaumbele. Na vile vile ni kweli asilimia kubwa ya wanaume wako after s*x.

Tujifunze kuongeza thamani katika mahusiano...mahusiano sio kupelekeana kula bata na Mafichoni Lodge bali ni kuombeana tunapokuwa down, kutiana moyo kuendelea kupambana na maisha..kusikilizana, na kupeana ushauri wenye tija, that's smart dating.

Inakua ni kazi bure pale ambapo mwanaume unajua jinsi ya kutengeneza pesa lakini unapata mwanamke ambae anajua kutumia tu. Ndio maana kwenye mahusiano ni vema nyote wawili mkawa na falsafa moja kuhusiana na pesa.

Vinginevyo utakua unacheza soccer safi la kushambulia, lakini defense ni dhaifu mno. Itakua ni ngumu kwa hiyo timu kushinda haitajalisha ni kwa kiasi gani inao washambuliaji makini wanaozifumania nyavu. Na mwanamke ni k**a safu ya ulinzi.

My wisdom; "As for you ladies, Be a Woman of virtue and purpose...Slay with sense and dignity..As for you Men, You gain more value as a man when you refuse to s*x with any woman just because she is available. The class you gain is invaluable. That's the Gentleman's Code."

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Dodoma