11/02/2024
Kitaalamu hii imekaaje
All football news
11/02/2024
Kitaalamu hii imekaaje
03/09/2022
Zoran Maki kocha Mwenye misimamo mingi Sana huwa anafanya jambo analo litaka yeye tuuu hataki kupangiwa .
Siku zote makocha WA aina hii huwa hawadumu katika Soka letu kwa sababu Viongozi wengi wa soka LETU huwa hawapendi KUAMBIWA Ukweli .
Soka la Tanzania Ili lipige hatua kubwa linahitaji makocha WA aina hii Ili Viongozi wa timu wabaki katika kazi zao za msingi waache kuingilia benchi la Ufundi.
Nasredine Nabi pale maamuzi yake yanaheshimiwa na haingiliwi kamwe tunaona na Zoran Maki pia hata Pablo Franco hakuingiliwa na mtu yoyote nzuri Sana HIII .
Siku zote kocha ni mtu WA mwisho katika maamuzi kwa sababu yeye mda mwingi yupo karibu na wachezaji.
👉Maneno ya mmoja kati ya wadau wa soka Tanzania
02/09/2022
🇨🇩Takwimu za Tuisla Kisinda akiwa RS Barkene
🏟️Game- 36
⚽Goal- 1
🅰️Assists - 4
Man of the match mara- 0
Tukiachana na zile mbio zake Uwanjani hakuna kingine alichonacho .
🇿🇲CHAMA JR akiwa RS Barkene
🏟️Game- 3
⚽Goal- 1
🅰️Assists - 2
Man of the match Mara -1
Chama Jr aliondoka kisa mifumo mibovu ya ulipaji wa Pesa Kisinda ameondoka kisa kiwango kibovu na kukosa mchango kwenye klabu Yao wanasema waarabu kazi yake ilikua kula na kwenda uwani tu😂😂 maana mkataba wake ulikua wa Miaka minne 4 ila wameona wakatishe akaendelee kujichubua Kule Jangwani 🟢🟠
👉unazungumziaje swala hilii
02/09/2022
Unafikiri nani kakalia kuti kavu
02/09/2022
Dirisha la usajili la Epl limefungwa rasmi tarehe 2 September. Shukrani za dhati ziwaendee hawa watu wameupiga mwingi sana kutuhabarisha yanayojiri kwenye usajili. Ni wakati sasa wa kuyaona matunda ya sajili zetu japokuwa Kuna Mengine tayari yamesha Anza kuonekana. All the best🙌
31/08/2022
HAKIKA ILIKUWA SIKU YA HUZUNI KWA WAPENDA SOKA.
Siku ambayo kikosi kizima cha timu ya taifa ya Zambia kiliangamia.
Ilikuwa ni tarehe 27/4/1993 jioni ambapo ndege ya Zambia air Force ilipopata ajali ikiyokea Libreville, Ambapo ilikuwa imebeba wachezaji waliokuwa wanaenda kucheza mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Senegal huko Dakar.
Abiria 25 na baadhi ya wahudumu wa ndege walipoteza maisha.
Watu wafuatao walipoteza maisha.
Wahudumu wa ndege.
➡️Colonel Fenton Mone (pilot)
➡️ Colonel Victor Mubanga (pilot)
➡️ Colonel James Sachika (pilot)
➡️Edward Nhamboteh (Injinia)
Wachezaji.
➡️Efford Chabala (golikipa)
➡️John Soko (beki)
➡️Whiteson Changwe (beki)
➡️Robert Watiyakeni (beki)
➡️Eston Mulenga (beki)
➡️Derby Makinka (kiungo)
➡️Moses Chikwalakwala (kiungo)
➡️Wisdom Mumba Chansa (kiungo)
➡️Kelvin "Malaza" Mutale (mshambuliaji)
➡️Timothy Mwitwa (mshambuliaji)
➡️Numba Mwila (mshambuliaji)
➡️Richard Mwanza (golikipa)
➡️Samuel Chomba (beki)
➡️Moses Masuwa (mshambuliaji)
➡️Kenan Simambe (mshambuliaji)
➡️Godfrey Kangwa (kiungo)
➡️Winter Mumba (beki)
➡️Patrick "Bomber" Banda (mshambuliaji)
Makocha
➡️Godfrey "Ucar" Chitalu (kocha mkuu)
➡️Alex Chola (kocha msaidizi)
Wachezaji wawili
Charlie Musonda na Kalusha Bwalya (nahodha wa timu). Wao walinusurika na ajali hii kwakuwa wao walikuwa Ulaya (kwenye majukumu ya vilabu vyao) hivyo walitakiwa kuungana na wachezaji wenzao moja kwa moja kwa bahati mbaya wenzao wanapata ajali,kwahiyo kwenye jumla ya wachezaji walioitwa na kocha wao kwaajili kushiriki kwenye mashindano hayo ni wachezaji wawili tu walibaki hai.
Pumzikeni kwa amani,walikufa kishujaa na watabaki kuwa maahujaa,siku zote mtabaki kuwa katika fikra zetu.
Hasa kwa sisi Waafrika.
Usisahau ku like page kwa taarifa zaidi za michezo
31/08/2022
Mchambuzi mimi nimebaki mdomo wazi, sielewi nini kimetokea!
Ni kweli siwajui sana wachezaji kumshinda Thomas Tuchel, anashinda nao mazoezini na amejiandaa na mechi ya leo kwa zaidi ya siku mbili, kwahiyo mbinu za leo alishazifanyia kazi kuanzia kwenye uwanja wa mazoezi.
Lakini ningepata nafasi ya kumhoji leo, kwa hizi dakika 45' za kipindi cha kwanza, ningemuuliza kwanini amechagua kwenda na mfumo wa mabeki wanne?
Azpilicueta kucheza upande mmoja na Hakim Ziyech, binafsi sikulitegemea na nililiona ni k**a tatizo, Tuchel anajua Azpi sio bora tena, ndiyo maana mara kadhaa amekubali kumpanga k**a RWB na nyuma yake anamweka Reece James ili akafanye makosa mbele kuliko kufanya makosa nyuma.
Sisemi k**a Azpi ameshaishiwa kabisa, lakini sio bora tena kucheza tena upande ambao Hakim Ziyech yupo, mfumo wa 4-3-3 kwa kikosi alichokuwa nacho leo naona k**a haikufaa, binafsi yangu na uchambuzi wangu wa hovyo, ningeona ingekuwa sawa Cheek akacheza k**a RWB kisha nyuma yake akae Azpi, kwenye mfumo wa mabeki watatu, au k**a akitaka aendelee na mfumo wa mabeki watatu, basi Chalobah awe nyuma, Azpi au Cheek akae juu yake.
Ziyech na Azpi wote sio bora kwenye kuzuia....Mount pia anashindwa kutengeneza umoja mzuri kwenye safu ya kiungo!
Imekuwaje Tuchel kachagua kwenda na mfumo wa mabeki 4? Nipo hapa nawaza bila majibu!
Mchambuzi nimechambua soka au karanga?😂
31/08/2022
Burna Boy🇳🇬 : Haya Ndio mambo waandaji wa tamasha wanapaswa kukamilisha ili Burna Boy akubali kutumbwiza kwenye tamasha 😱😱😱😱
Kwa mujibu wa gazeti la The Nation: yafuatayo Ndio mambo ambayo Burna Boy anahitaji ili atoe burudani kwenye tamasha
Burna Boy ili atumbwize huwa analipwa dola laki 5 ( 500,000$) kabla kwanza yakutumbwiza
Lakini sasa lazima wakamilishe haya yafuatayo 👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Lazima waandaaji wa tamasha hilo walipe tiketi ya ndege binafsi( private jet) yenye sit 13 ili kukamilisha usafiri wake
Baada ya hapo, lazima kutakuwepo msafara wa gari 5, bus kubwa ambalo litafanyakazi siku nzima .
Burna boy anapaswa kulala kwenye Hotel ya kifahari yenye gorofa kuanzia 4,5 Na hapo sasa lazima Apewe kile chumba cha kifahari kuliko vingine lazima pawepo chumba maalumu cha kuvutia ( sigara....) Na vyumba vingine viwili ambavyo Bado hawajataja kazi yake maalumu Na vyumba vingine Sita vilivyomo vioo vikubwa Kwa ajili ya Watu wake Yaani hapo kwa jumla anahitaji vyumba 10 .
Kunahitajika pia sebule kubwa ambayo yeye Na watu wake watapiga story Na liwe eneo la kuvuta ( sigara,...) .
🔴Kuhusu Chakula
Vyumba vyote 10 kunapaswa kuwepo chakula ambapo lazima wahudumiwe chakula Asubuhi mchana Na jioni lakini pia chakula lazima kiwe cha kifahari ”.
Bado hatujamaliza mdau wetu wa Tujuze, tukiendelea Na Gazeti hilo linataja kua lazima kuwepo chupa 12 za maji , Ginger ales 8, Sprites 6, chupa kubwa 6 za Pepsi Soda, mzabibu , chupa tatu za Champagne 🍾 , chips la Hennessy XO, Whisky Jack Daniels Na vingine ambavyo hawakutaka kuweka wazi lakini pia lazima kuwepo aina yote ya matunda 🍌, 🍉 , 🥭, 🍍,......
Lazima vitamba vyote viwe Na rangi nyeusi. Lazima pawepo towel (vitamba) 6 vyenye rangi nyeusi Kwa kuvutia jasho usoni mwake, Na 4 vyakutumia chooni lazima hivyo viwepo kabisa Kwa ajili ya Staaa mkubwa Burna Boy
👉Je Unafikiri yupo sahihi?
31/08/2022
FULL TIME:
🏟️ St Mary's Stadium
SOUTHAMPTON 2-1 CHELSEA
⚽ Lavia 28'
⚽ Armstrong 45+1'
⚽ Sterling 23'
Shughuli imemalizika katika dimba la St Mary's, the Blues wamepokea kipigo cha pili cha ugenini msimu huu mikononi mwa Watakatifu, Southampton.
30/08/2022
Kupitia ukurasa wa unaandika kuwa Klabu ya Manchester city ipo karibu kufikia makubaliano na Klabu ya Borussia Dortmund kumsajili beki wao . Man city hawaja muuza beki yeyote wa kati msimu huu lakini wanataka kuongeza ili kuunda safu bora zaidi ya ulinzi.
🔵Name: Manuel Akanji
🔵Uraia: Swiss
🔵Umri: 27yrs
🔵Nafasi: Beki wa kati
🔵Urefu: 1.88m(futi 6 na inchi 2)
=Like Page Yetu uwe wakwanza kuhabarika..
[/]✓
30/08/2022
▪︎Idrissa Gana Gueye atasafiri hadi Uingereza usiku wa leo kusaini Everton kwa ada ya kawaida. Atafanyiwa vipimo vya afya kesho na kusaini mkataba wa miaka miwili, pamoja na chaguo la mwaka mmoja mwengini. 🚨✅
Source: David Ornstein