11/12/2024
JUDE BELLINGHAM VS JAMAL MUSIALA KWAKO YUPI NAMBA 10 BORA MPAKA SASA.
TAKWIMU MSIMU 2024/2025
JUDE BELLINGHAM
1.MECHI 12 MAGOLI MATANO (5) ASSISTS NNE(4) DAKIKA ALIZOCHEZA 979.
JAMAL MUSIALA.
2. MECHI KUMI (10) ALIZO ANZA MAGOLI NANE (8) ASSIST MOJA (1) DAKIKA ALIZOCHEZA NI 839.
~ HIZO NI TAKWIMU KWENYE LIGI ZAO KWA MAANA LALIGA NA BUNDESLIGA , TWENDE SASA UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
JUDE BELLINGHAM.
~ MECHI SITA (6) GOLI MOJA (1) NA ASSIST MOJA (1) DAKIKA ALIZOCHEZA 510.
JAMAL MUSIALA.
~ MECHI SITA (6) ALIANZA MECHI NNE (4) PEKEE MAGOLI MAWILI (2) NA ASSISTS TATU (3) DAKIKA ALIZOCHEZA 399.
~ Msimu huu mpaka sasa Jamal Musiala ameonekana akiwa bora kwangu Mimi naenda na Jamal Musiala namba za takwimu zinambeba kutokea uwanjani, sijui Kwa upande wako wew utaenda na nan?
~ Jamal Musial ni Muingereza Kwa kuzaliwa ila anachezea timu ya taifa Ujerumani kutokana kufuata utaifa wa bimkubwa wake, miaka 21 tu kijana anazima Bayern Munich !.
~ Jude Bellingham ni mzaliwa WA Uingereza wazazi wake ni waingereza , Jude ana miaka 21 anakiwasha pale Real Madrid.
~ JUDE NI MZURI ILA TAKWIMU HAZIKO SAWA NA HUYU MUINGEREZA MPAKA SASA.
10/12/2024
SUNDOWNS THEY HAVE ANNOUNCED THEIR NEW COACH NAMED MIGUEL DE AZEVEDO CARDOSO.
~ Two hours ago, it was reported that Mamelodi Sundowns chairman Thlopie Motsepe announced the dismissal of coach Manqoba Mngqithi following a series of poor results on the pitch. His position will now be taken over by Miguel Cardozo, who will be assisted by Steve Komphela the fomour goal keeper of Zambia.
~ Be informed that Mamelodi Sundowns currently leads the South African PSL league with 21 points, having lost only one match out of eight. However, in the CAF Champions League, they have drawn both of their two matches and have two points, placing them second in their group maybe the results of CAF CHAMPIONS LEAGUE were bad thus why they decided to remove out their coach.
chilodavid14 ✍️
IN KISWAHILI
~ Mamelod Sundowns hii leo wametangaza kocha mpya ambaye ni Azevedo Cardoso, hii imeripotiwa Leo mwenyeti wa Mamelod Sundowns amemfukuza kocha Manqoba Mngqithi baada ya muendelezo mbaya WA matokeo uwanjani Kwa timu io.
~ Fahamu kuwa Mamelod Sundowns wapo nafasi ya kwanza kwenye ligi yao ya PSL ana alama 21 kwenye mechi 8 alizocheza kafungwa mechi Moja tu lakini pia kwenye michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE huku sasa ndipo Kuna tatizo, hawa Masandawana kwenye michezo miwili waliyocheza yote wamekwenda sare na kuwa na alama 2 pekee na kwenye msimamo wa kundi yupo nafasi ya pili.
10/12/2024
YANGA YANGA YANGA.
~ Sio kwamba sikuhizi upatikanaji wa magoli pale jangwani umekua mgumu sana aisee, embu tumpe mida kidogo kocha la boli tokea Ujerumani( Germany)
~ Mara nyingi huyu kocha kwenye makaratasi pale kabla ya mechi Yanga huwa wanakuja na mfumo wa 4-2-3-1 au siku nyingine 4-4-2, baada ya mechi kuanza game plays zake zinakua mbili tu ni either atumie mfumo wakwake mwenyewe uo sasa 4-6-0 yaani hakuna namba 9 kwenye eneo la ushambuliaji kwenye mechi ambayo itamuihitaji alinde, lakini pia 2-5-3 kwenye mechi ambayo itamuihitaji ashambulie.
~ Kwenye mfumo wa 2-5-3 apo sasa ndiyo Yanga huwa anafungwa Yale magoli ya counter attacks kutokana na idadi chache ya walinzi asa asa akiwa anacheza na timu ambayo Ina mawinga wenye kasi zaidi.
~Germany Mashine bado mpaka sasa ajapata mfumo sahihi wakuutumia pale Yanga na hii inamcost sana kutokana na Yanga Kwa sasa ana michezo migumu sana, ambayo anabidi atulie na kushinda , rekodi Bado mpaka sasa hatuwezi sema chochote Kwa maana mchezo mmoja pekee mpaka sasa.
08/12/2024
CS CONSTANTINE BS SIMBA SPORTS CLUB 🔥
~ Mechi ilianza kwa kila timu kupeleka mashmbulizi kwenye lango la mwenzie, lengo ni kupata goli la mapema kabisa na dakika ya 25' ni simba ndiyo walifanikiwa kwenye io mbinu ya kupata goli la mapema , goli bora kabisa liliofungwa na beki wao kitasa Zimbwe.
~ CS Constantine mpira wake ulionekana kuwa mchakamchaka kwenda kuchomoa bao ambao lilifungwa na simba madhambi mengi walifanyia pia hawa CS Constantine walikua na wachezaji ambao wanajua kupiga mizuriiliyokufa tatizo likikua kwa wamaliziajiwa wa io mipira.
~ Kipindi cha kwanza wanetu wa Simba sports club wamenaswa sana kwenye mtego wa kuotea (offside), ukiangalia na vile vituko vya Ateba ilikua poa sana kwenye harakati za kupoteza muda 😃.
HALF TIME CS CONSTANTINE 0 : 1 SIMBA SPORTS CLUB.
~ Kipindi cha pili kilianza kwa moto pia mwanzoni kabisa mwa kipindi cha pili Hamza Abdulazack alijiweka kamba mwenyewe na kufanya ubao usome moya moya, pia dakika ya 50' Brahim Did aliwaandikia CS Constantine bao la kuongoza na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
~ Brahim Did ni nyota ambae alikua wakuchungwa kwenye mchezo na ndiyo anaongoza kwa magoli kwenye timu yao yuko na magoli matano.
~ Simba wali settle, wakarudi kwenye utulivu na kuanza kucheza mpira na kuanza kufika kwenye lango la mpinzani wake CS Constantine.
~ Kibu Denis kafanya jitihada nyingi sana kapambana sana kwenye mchezo wa leo alikua na good game (mchezo mzuri), Fabrice Ngoma pia alikua na mchezo mzuri leo kapiga sana pasi mbele kuna zilizofika na zisizofika, Chamoua leo kaonyesha mchezo mzuri pia.
~ Mwalimu fadlu alifanya mabadiriko kumuingiza Mukwala na Nouma Valentine Lemgo ni kwenda kuongeza mashamulizi kupitia upande wa kushoto mwa mpinzani wake.
~ Yawezekana Brahim Did ndiye mchezaji ambae kafanyiwa mazambi mala nyingi kuliko mchezaji mwingine leo.
~ ila kipa wa CS Constantine bhana ana madoido sana raha ya kuongoza kwa waarabu bhana silaha kubwa yao ni kupoteza muda tu.
FT CS CONSTANTINE 2 : 1 SIMBA SPORTS CLUB 🔥
08/12/2024
DISEMBA 8 2024 CS CONSTANTINE VS SIMBA SPORTS CLUB.
~ Mchezo utapigwa huko Constantine mjini Algeria majira ya saa moja usiku Kwa saa za Africa Mashariki wenye uwezo wa kubeba mashabiki 22,968.
~ Huu ni mchezo wa pili wa hatua za makundi kwenye CAF Confederation Cup, ifahamike kuwa michezo yao ya kwanza timu hizi mbili ziliibuka na ushindi wa bao Moja moja Simba akimfunga Bravos na huku CS Constantine akimfunga CX Fraxien na timu hizi zina alama tatu zote kinachowatenganisha ni herufi tu za mwanzoni.
~ Pia hii timu haichezi mpira wa kiarabu sana huwa anacheza modern football Kwa maana mpira wa kisasa zaidi atalinda na kukushambulia Kwa ufasihi zaidi
~ CS Constantine Kuna wachezaji baadhi ni wakuchungwa wachezaji k**a Brahim Did, Achref Boundrama na Abdennor Belhoucini.
~ Simba ana nafasi kubwa ya kushinda ila asicheze k**a alivyocheza na Bravos nadhani fadlu aje na game play tofauti kabisa ya kuwachosha waarabu.
PRAY FOR SIMBA🦁❤️🇹🇿TANZANIA
08/12/2024
HAIJAISHA WANETU.
~ MSIMU ULIOPITA YANGA PIA ALIANZA VIBAYA KWENYE HATUA ZA MAKUNDI MECHI TATU MFULULIZO ALIKUSANYA ALAMA MOJA TU NA AKAFANIKIWA KUPITA KWENDA ROBO FAINALI KWA ILE KANUNI YA HEAD TO HEAD MONASTIL ALIKUFA BANGO NNE TAIFA PALE.
~ KUNA SEHEMU WANETU WAMEANDIKIWA TU NA INSHALLAH WANANCHI WATAENDA KUFURAHI SILAHA KUBWA KUWA NA SPIRIT YA KUKAZA UWANJANI SIKUHIZI WANETU WANAKABA SANA KWA MACHO ILA SIO KINYONGE KIIVYO.
~ MJERUMANI MASHINE WA GUSA ACHIA MALI AISEE ANAUFANYA MPIRA UONEKANE MBAYA SANA NADHANI HANA GAME PLAN KABISA NZURI KOCHA UZOEFU WAKE MDOGO MNO SEMA NDO HIVYO HAKUNA JINSI TENA WANANCHI NI KUPAMBANA TU.
~ KESHO ITAKUA POA SANA WANANCHI 👏YANGA 🔥 TUNAWAJUA MKO MOTO SANA SEMA BAHATI HAIKUA KWENU JANA SIKU NYINGINE ITAKUA KWENU .
~ TP MAZEMBE ANAFATA NI YANGA TENA ATAKUA UGENINI DECEMBER 14.
07/12/2024
MC ALGER VS YANGA.
~ Kipindi cha kwanza wanetu wa Yanga wamechezewa nusu uwanja aloo yanga waliwaacha sana MC Alger acheze mpira ni kitu ambacho hakikua kizuri kwenye game plan ya mwalimu Ramovic.
~ kipindi cha kwanza Pacome Zouazoua amepewa kadi ya njano ya kujitakia kabisa kwenye ile dakika ya 23'
~ Dakika 30 za mwanzo Yanga waliwaacha MC Alger wacheze wanavyotaka afu wao kazi yao ilikua kuzuia , baada ya dakika 30 za mwanzo Yanga wakafunguka na wao kuanza kucheza mpira
~ MC Alger walikua fasta sana kurudisha mali baada ya kupoteza mali ni wepesi sana kukaba na kurudisha mpira tena kwenye imaya yao.
~ Kuna mwamba anaitwa Delort anavaa jezi namba 9 ni alikua moto sana good game kwake, Kwa Yanga ibra bacca alooo ni moto sana kwenye lile eneo la ulinzi pale Yanga.
HT MC ALGER 0 : 0 YANGA
~ Nimependa ile fair play ya mtu mmoja kutoka benchi la ufundi kwa Yanga alikua akiongea na ball boys pape hii ndiyo maana halisi ya mchezo wa mpira wa miguu.
~ Kipindi cha pili kilivyo anza MC Algers walianza kwa moto sana, kuna mwamba anavaa jezi namba 11 alooo alikua moto sana ile winger machachali mno huyo Tayeb Meziani.
~ Poor marking kwa Yanga inawapa goli Mc Alger kulitia captain wao Ayoub Abdelloui mnamo dakika ya 64' piga goli flani hivi la kichwa baada ya mpira wa freekick.
~ Mabeki wa Yanga kuna muda walikua wamechoka walai mpaka Djigui alikua na kazi nyingine tena ya kufanya afanye marking yeye mwenyewe.
~ Wanetu ball boys walianza kuzingua kuanzka dakika ya 70' ya mchezo , na waarabu wakaanza kulala pale uwanjani kwenye izo dakika baada ya kupata bao lao la kuongoza .
~ Yanga hili tatizo la namba 9 asilia bado linawatesa sana pale mbele , nimeona mipira inayofika hakuna wamaliziaji pale mbele.
~ Dakika ya 78' aliingia Sofuine Bayazid na Kipre Junior sasa pale game plan ya mwalimu wa MC Alger ilikua kutumia mawinga ila apate matokeo kwenye dakika 10' za mwishoni, ila lengo lao halikufanikiwa yanga wakakaza
~ Poor marking ile ile Kipre Junior chupu chupu awaweke kamba pale, yanga mashambulizi tena.Chama chupu chupu awaweke kamba sio bahati kwao yanga.
~ Dakika za jioni Djigui Diara amepewa kadi ya Njano ni ya kujitakia kabisa angekausha , Chama pia amepewa kadi ya njano sahihi kabisa alifanya madhambi.
~ MC Algers wakapata bao la pili kupitia Sofuine Bayazid jezi namba 7 goli la kikatili kabisa na kumaliza mchezo.
~ Yanga haijaisha mpaka iishe sisi waTanzania tupo pamoja na nyinyi Yanga mpaka mwisho wa safari hii ya ligi ya mabingwa Africa 🌍, Yanga poleni kwa kupoteza mchezo wa pili kwenye hatua za makundi ya CAF CHAMPIONS LEAGUE bado kuna mechi 4 mbele tunaimani mtafanya vizuri zaidi na ziaid.
~ Yanga mpaka sasa hivi anadaiwa magoli manne atatoboa kweli?
FULL TIME MC ALGER 2 : 0 YANGA