29/08/2022
: Wak**atwa na polisi kwa madai ya kutaka kumpindua Mwenyekiti wa shirikisho la Soka kambini
Baadhi ya viongozi kwenye k**ati ya Wenyeviti wa vilabu wamek**atwa Jumatatu hii Agosti 29, 2022 kwa tuhuma za kupanga njama za kutaka kumpindua Mwenyekiti wa shirikisho la soka, Bwana Abbé MAYELE KINOIS; kambini hapa mkoani Kigoma.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wa karibu na viongozi wa jamii wahusikao na michezo zimethibitisha hilo kwa kusema kuwa k**ata k**ata hiyo imefanyika mida ya saa saba mchana ambapo zaidi ya watu wawili ndio wamepelekwa kituo cha polisi A ili kwenda kujibu shtaka linalowakabili la kufanya kikao cha kupanga mapinduzi ya kumuondoa Bwana Kinois bila kupata kibali toka Ofisi ya Mkuu wa kambi.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakupenda kutaja jina lake amesema; "Hawa viongozi wenu wanacheza na serikali. Tuliwasambaza hiyo jana pale kwenye ukumbi wa vijana walipokutana bila barua ya ruhusa toka serikalini. Nimesikia eti ni zaidi ya vikao viwili wamefanya bila kuwa na kibali."
Kuk**atwa kwa viongozi hao wa k**ati ya Wenyeviti wa vilabu kunakuja wakati huu ambapo zaidi ya asilimia 95 ya Wenyeviti wa vilabu vyote vya daraja la kwanza na la pili kambini hapa wamekuwa wakimpinga bwana Kinois kutokana na uongozi wake mbaya ambapo Wenyeviti hao wa vilabu waliwayi kukutana Agosti 9, 2022 kwenye kikao cha kuamua kuomba Mwenyekiti wa shirikisho pesa walizochangiza kwa ajili ya washindi wa ligi ya Nyarugusu Cup daraja la kwanza na la pili ili washindi hao wapate haki yao na kuhamua kumkataa bwana Abbé MAYELE KINOIS.
Vigogo hao waliwayi kuandikia bodi ya michezo barua wakionyesha kuwa Kinois hafai kuwa Kiongozi wa shirikisho kambini kutokana na makosa mengi anayoyafanya ikiwemo kula rushwa pande zote na kujikopa hela ya kuendesha ligi bila kuzirejesha. Majibu ya barua hiyo ya Wenyeviti wa vilabu yalionekana kuchelewa ndipo wakaamua kuandaa kikao hicho ambacho kimepelekea baadhi ya waandaaji wacho ambao majina hayajajulikana kuonja maabusu.
26/08/2022
HIVI KWA HII DERBY KATI YA AB3 ABEILLES NA S2 SPORTS CLUB NI UPI UTABIRI WAKO KUHUSIANA NA MECHI HIYO YA HAO WATANI WA JADI WAWILI WA MIAKA MINGI AMBAO PIA NI MAJIRANI SANA?
07/08/2022
: DOUÉ NOUMANDIEZ ATEULIWA KUWA BOSS MPYA WA KAMISHENI YA MAREFA WA CAF
Doué Noumandiez Désiré ameteuliwa na Mwenyekiti mpya wa CAF, Bwana Patrice Motsepe, kuiongoza Kamisheni ya marefa kwenye ngazi ya soka barani Afrika.
Doué Noumandiez Désiré amekuwa bosi mpya wa marefa wa mpira wa miguu Afrika. Mwenyekiti huyo ambaye ni raia wa Ivory Coast aliteuliwa na Motsepe mwanzoni mwa wiki hii kuchukuwa wazifa huo. Baaba ya kufanya ziara nchini Algeria, Raïs wa soka barani Afrika aliamua kumfukuza bwana Eddy Maillet kutokana na matukio mengi katika uamuzi kwenye soka la barani Afrika. Doué Noumandiez aliyeteuliwa atakuwa na jukumu nzito la kuboresha soka kwenye uamuzi barani.
Akiwa famasia aliyefunzwa na mwenye taaluma, Doué Noumandiez aliyeichukuwa mikoba ya Eddy Maillet amewahi kusimamia michezo mikubwa ya soka ikiwa ni pamoja na CHAN 2009, CAN 2020, CAN U17 2011, Ligi ya mabingwa ya CAF 2011, Kombe la dunia Monde 2014 na kombe la dunia la vilabu 2014.
06/08/2022
LIGI YA UFARANSA: PSG YAANZA MAUAJI KWA KUWATANDIKA CLERMONT FC 5 - 0
⏱ MUDA KAMILI WA MECHI !
CLERMONT 0 - 5 PARIS
Hawa ndio waliofunga magoli kwenye mechi hiyo:
⚽️ Neymar
⚽️ Hakimi
⚽️ Marquinhos
⚽️ Messi
⚽️ Messi
🔴 Hili limekuwa onyesho la kwanza la PSG kuanza Ligue 1 msimu huu!
06/08/2022
: UONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI TANZANIA, TFF WATANGAZA KUWASILI KWA RAÏS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU BARANI AFRIKA, CAF DOKTA PATRICE MOTSEPE AMBAYE ANATARAJIWA KUPOKELEWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KILIMANJARO HIYO JUMAPILI AGOSTI 7, 2022 MIDA YA SAA KUMI NA MBILI JIONI
02/08/2022
: S2 Sports Club yaibutua Fundisho 1 - 0 kwenye Umoja wa madereva Cup
• 🏟️ Arena stadium/ Makere*
• ⚽ S2 Sport 1️⃣-0️⃣ Fundisho FC
28/07/2022
: CAF YATANGAZA TOP 20 YA VILABU BORA BARANI AFRIKA
Hii hapa orodha ya vilabu 20 bora kwa mujibu wa CAF:
1. Al Ahly 🇪🇬
2. Wydad Casablanca 🇲🇦
3. Petro de Luanda 🇦🇴
4. CR Belouizdad 🇩🇿
5. Raja de Casablanca 🇲🇦
6. Mamelodi Sundowns 🇿🇦
7. Pyramids FC 🇪🇬
8. ES Setif 🇹🇳
9. Zamalek SC 🇪🇬
10. JS Saoura 🇩🇿
11. RSB Berkane 🇲🇦
12. Simba SC 🇹🇿
13. Orlando Pirates 🇿🇦
14. Al Hilal 🇸🇩
15. Esperance 🇹🇳
16. TP Mazembe 🇨🇩
17. JS Kabyile 🇩🇿
18. Rivers United FC 🇳🇬
19. Al Ahli Tripoli 🇱🇾
20. Al Merreikh 🇸🇩
K**a ulivyosoma kwenye orodha, Simba Sports Club ya Tanzania ipo kwenye nafasi ya 12 ikiwa imeipiku TP Mazembe ya DRC ambayo iko nafasi ya 16. Hivi Wakongomani mumefeli wapi jamani ao munaonaje mubaki zenu kwenye muziki tu?
28/07/2022
: Baraza la Nidhamu lamfungia Mwamuzi Alexis miezi 3 kwa kosa la kutomudu mchezo kwenye mechi mbili za Nyarugusu Cup
Baraza la Nidhamu kwenye Shirikisho la mpira wa miguu kambi ya Nyarugusu, AFRN limemfungia mwamuzi Bizimana Alexis kutojihisisha na maswalwa ya soka kambini kwa kosa alilorudia la kutomudu mchezo kwenye mechi mbili za ligi ya Nyarugusu daraja la kwanza na la pili iliyotamatika hivi majuzi kambini hapa, mkoani Kigoma.
Barua ambayo wanasheria hao wa soka kambini waliyomwandikia Bizimana Alexis hiyo Jumatano Julai 27, 2022 inataja kuwa Mwamuzi huyo amepumzishwa kwa kipindi cha miezi 3 baada ya kupatikana na makosa ya kutosimamia sheria 17 za soka hali iliyompeleke ashindwe kumudu michezo miwili wakati alipokuwa mwamuzi wa kati. Hii ni pamoja na mechi ya nusu fainali daraja la kwanza iliyopigwa Julai 08, 2022 wakati REGIDESO ilikuwa ikitwangana na GHI1 Bilombe na mchezo wa fainali daraja la pili kati Lion du camp walioonyeshana ubabe na Club United, kandanda iliyosakatwa Julai 21, 2022 kwenye Nyarugusu Cup na kupelekea washika bendera kuanza kubadilishwa k**a mboga mbichi zilizokosa soko.
Hivyo, kwa mujibu wa vitabu vya sheria za soka kwenye kanuni ya (6) ibara ya (a), Baraza la Nidhamu la Shirikisho limeamua kumfungia kimichezo mwamuzi Bizimana Alexis kwa muda wa miezi mitatu tangu hiyo Julai 27, 2022 hadi ifikapo Oktoba 27, 2022 ndipo atarejea kifungoni kuendelea na maswala ya soka.
22/07/2022
: Uongozi wa shirikisho la mpira wa miguu waahirisha siku ya sherehe za kutoa zawadi kwa washindi wa Nyarugusu Cup, Kulikoni? Zama hapa
Uongozi wa shirikisho la mpira wa miguu kambini Nyarugusu, AFRN kwa ufupi; umeamua Ijumaa hii Julai 22, 2022 kuhairisha siku ya sherehe za kutoa zawadi kwa washindi wa ligi ya Nyarugusu Cup iliyotamatika hivi majuzi kambini hapa, Wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa chazo chetu kilicho karibu sana na Uongozi wa kandanda kambini hapa, maamuzi hayo yametolewa kutokana na rufaa ambayo klabu ya AB1 SIMBA imekata kwenda Bodi kuu ya mpira wa miguu kambini baada ya klabu hiyo kupinga majibu yaliyotolewa kwao na baraza la nidhamu.
Hivyo, kwa maamuzi hayo ya Uongozi wa shirikisho la kandanda kambini hapa, sherehe ya utoaji zawadi kwa washindi wa Nyarugusu Cup ambazo zingefanyika hiyo Jumamosi Julai 23, 2022 kwenye ukumbi wa vijana D1, zone ya 1 imehairishwa hadi pale majibu ya rufaa hiyo ya AB1 SIMBA kulalamika kuwa klabu ya GHI1 BILOMBE walimchezesha mchezaji wao BARAKA swala ambalo limetupiliwa mbali na Baraza la sheria za soka kambini Nyarugusu.
Ikumbukwe kuwa klabu ya AB1 SIMBA walikuwa wameliandikia Baraza la nidhamu barua ya lalamiko kwamba GHI1 BILOMBE walimchezesha mchezaji wao BARAKA ambaye hao SIMBA wanataja kuwa hakutakiwa kuichezea BILOMBE ila kwa majibu ya wanasheria wa AFRN, lalamiko la AB1 SIMBA liko nje ya fensi kisheria za soka na matokeo yanabaki yale yale huku BILOMBE wakionekana kushinda kesi k**a isemavyo barua ya Uongozi wa nidhamu.
20/05/2022
NYARUGUSU_CUP: UONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU KAMBINI WATOA BARUA ZA TAARIFA ZA MIPANGO YA MECHI ZA VIPORO NA KUHAIRISHWA KWA MECHI AMBAZO ZINGEPIGWA WEEKEND HII.
07/05/2022
MICHEZO: MECHI ZA MTOANO ZA NYARUGUSU CUP KUANZA KURUSHA VUMBI WEEKEND HII
05/03/2022
?? : ABBE M. KINOIS AKUTANA NA WENYEVITI WA VILABU VYA DARAJA LA KWANZA NA LA PILI
Mwenyekiti wa shirikisho la soka katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (AFRN) Bw. Abbé Mayele Kinois amekutana na wenyeviti wa vilabu vya daraja la kwanza na la pili katika mkutano wa Baraza kuu kambini hapa, mkoani Kigoma.
Mada kuu zilizojadiliwa katika mkutano huo ulioanza tangu saa tatu na dakika 45 na kutamatika saa nane na dakika 40 ni pamoja na swala la wachezaji wageni, usajili wa wachezaji, mafunzo ya kuhusu Uongozi kwa viongozi wa vilabu na maandalizi ya ligi mpya inayotarajia kuanza kurusha vumbi wiki ijayo.
Wakati mada hizo zikifafanuliwa mkutanoni, washiriki wamekubaliana kuwa wachezaji wageni ni wale watakaoanza kuonekana kwenye vilabu kuanzia sasa wakiwa bado kusajiliwa na kilabu chochote kambini hapa ambao imesemekana kuwa kwenye vitambulisho vyao kusiwe kunajazwa namba yoyote ya kitambulisho, jambo ambalo wote waliosh*tiki walihafiki.
Na, kuhusu swala la usajili; mwenyekiti wa AFRN amesema kuwa kuna fomu za makubaliano ambazo wachezaji 33 wa kila kilabu watatakiwa kujaza. Hii itahusu kila mchezaji na uongozi wa klabu husika ambayo mchezaji husika atataka kuichezea; 'tofauti na hapo timu itasubiri Oktoba 2022 ili kumsajili mchezaji huyo'; Kinois amekazia.
Ama kuhusu swala la mafunzo kwa Viongozi wa vilabu, timu zote zimekubaliana kwamba mafunzo hayo yafanyike wiki ijayo kwa muda wa simu mbili ambazo ni Ijumaa na Jumamosi. Kwenye siku hizo mbili, washiriki watafaifi mafunzo ya jinsi ya kuviongoza vilabu vyao kwa misingi sahihi na imara wakitia ndani kupata maelezo ya jinsi ya kuandaa katiba za vilabu vyao ambao ndio ukingo pekee wa viongozi na wachezaji pamoja na mashabiki.
Na kuhusu maandalizi ya ligi nyingine, kura imepigwa ya kujadili kuhusu kiwango cha pesa ambacho kila kilabu kitajisajili. Walioshinda kwenye kupiga kura hiyo ni wale walioenda upande wa timu za daraja la kwanza kutoa shilingi 80.000 na zile za daraja la pili kutoa 55.000/=
✍🏽