24/06/2025
: “Nimefanya Rotation katika michezo iliyopita, k**a tutashinda kesho tutakuwa Mabingwa bora sana, naona watu wengi wapo kinyume na sisi kwanini tupo hapa, na k**a tutashinda hili kombe tutakuwa mabingwa wazuri Mno” Miloud Hamdi – Kocha wa Yanga
spt
23/06/2025
Maofisa wa mchezo namba 184 wa ya (Young Africans vs Simba SC).
23/06/2025
BODI ya Ligi kuu ya soka Tanzania bara TPLB imetangaza maofisa wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kwenye Ligi Kuu bara kati ya wenyeji Young Africans Sc dhidi ya Simba Sc ambapo mchezo huo namba 184 utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar kutoka Misri akisaidiwa na Mahmoud Ahmed Abo El Regal k**a Mwamuzi msaidizi namba 1 na Samir Gamal Saad Mohamed ambaye atakuwa msaidizi namba 2.
Ahmed Mahrous naye kutoka Misri atakuwa ‘4th Official’ naye kutoka Misri huku Kamishna wa mchezo huo utakaopigwa Juni 25, 2025 saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa akitarajiwa kuwa Salim Omary Singano.
spt🦂