Korogwe District Football Association

Korogwe District Football Association

Share

Chama cha Soka Korogwe (KDFA) - Tunajenga vipaji na kuendeleza soka safi wilayani Korogwe.

Photos from Korogwe District Football Association's post 07/04/2026

Hongera wanamichezo wote kwa juhudi kubwa mlizoonyesha uwanjani! πŸ’ͺ⚽
Mchezo kati ya Magunga 0 dhidi ya Milani 1 umehitimishwa, na licha ya matokeo, bado mmeonesha moyo wa kupambana, nidhamu na uzalendo wa hali ya juu. Kumbukeni, ushindi sio mwisho wa safari bali ni hatua, na kushindwa sio mwisho bali ni funzo la kujijenga zaidi.
Kwa timu ya Magunga, pigeni moyo kondeβ€”kila changamoto ni nafasi ya kujirekebisha na kurudi imara zaidi. Kwa Milani, hongereni kwa ushindi, endeleeni kudumisha kiwango na nidhamu.
Twendeni tukazidi kushirikiana, kujifunza na kuendeleza vipaji vyetu kwa ajili ya maendeleo ya mpira wetu wa wilaya. πŸ”₯⚽
Mpira unaendelea, safari bado ndefu!

06/04/2026
04/04/2026

Matokeo ya mchezo uliochezwa katika uwanja wa TTC yamekamilika k**a ifuatavyo:
Rising Stars 1 – 3 Golden Generation
Kwa leo ikiwa ni siku ya ufunguzi, mchezo umehitimishwa rasmi.
Tunawakaribisha wadau wote wa michezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kesho kwa mchezo mwingine utakaoendelea.
Karibuni sana! ⚽πŸ”₯

18/05/2025

Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Korogwe (KDFA) kinapenda kuwataarifu wadau wote wa michezo na wapenda soka kuwa kutakuwa na Kozi ya Ukocha wa Mpira wa Miguu Ngazi ya Awali (Basic Coaching Course) itakayofanyika hivi karibuni.

Kozi hii inalenga kuwajengea uwezo watu wanaotamani kuwa makocha wa soka kwa ngazi za awali na kuanza safari yao ya ukocha kwa ufanisi

04/04/2025

Ndio, Manchester FC wameibuka kidedea baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Magoma FC katika uzinduzi wa ligi ya wilaya ya Korogwe.Ulikuwa mchezo wa kusisimua!

03/04/2025

πŸ“’ LIGI YA WILAYA YA KOROGWE KUZINDULIWA RASMI! ⚽πŸ”₯

Leo ni siku kubwa kwa soka la Korogwe! Tunafungua rasmi Ligi ya Wilaya ya Korogwe katika Kata ya Magoma, tukishuhudia vipaji vya mpira wa miguu kutoka wilaya yetu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huu ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mheshimiwa Mzava. Tunamkaribisha kwa heshima kubwa kushiriki nasi katika tukio hili muhimu kwa maendeleo ya soka letu.

Wananchi wote mnakaribishwa kuja kushuhudia mechi za kusisimua na kuunga mkono vijana wetu! πŸ™Œβš½

Photos from Korogwe District Football Association's post 03/04/2025

πŸ“’ LIGI YA WILAYA YA KOROGWE KUZINDULIWA RASMI! ⚽πŸ”₯

Leo ni siku kubwa kwa soka la Korogwe! Tunafungua rasmi Ligi ya Wilaya ya Korogwe katika Kata ya Magoma, tukishuhudia vipaji vya mpira wa miguu kutoka wilaya yetu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huu ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mheshimiwa Mzava. Tunamkaribisha kwa heshima kubwa kushiriki nasi katika tukio hili muhimu kwa maendeleo ya soka letu.

Wananchi wote mnakaribishwa kuja kushuhudia mechi za kusisimua na kuunga mkono vijana wetu! πŸ™Œβš½

23/12/2024

πŸ›‘ FULL TIME + PENALTY SHOOTOUT: MATOKEO YA FAINALI!

πŸ† KDFA Post Uchaguzi Cup

πŸ“ Uwanja wa Magereza Stadium, Korogwe
⚽ Mombo Mji 2️⃣ - 2️⃣ Manundu (Dakika 90)
⚽ Penati: Mombo Mji 3️⃣ - 2️⃣ Manundu

πŸŽ‰ Mombo Mji wameibuka mabingwa wa Korogwe Post Uchaguzi Cup baada ya ushindi wa mikwaju ya penati katika fainali ya kusisimua!

πŸ‘‘ Shukrani kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Athumani Nyamlani, Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, kwa heshima ya kuungana nasi kwenye tukio hili la kihistoria.

πŸ™Œ Tunawashukuru mashabiki wote, timu zilizoshiriki, na wadau wote waliowezesha ligi hii kufanikiwa. Korogwe imeonesha mshik**ano wa kweli kupitia soka!

πŸ’₯ Korogwe imechagua kwa amani, sasa tumeandika historia ya furaha ya soka!

22/12/2024

⚽ FAINALI YA KDFA POST UCHAGUZI CUP! πŸ†

πŸ“ Uwanja wa Magereza Stadium, Korogwe
πŸ“… Tarehe: Jumatatu, 23 Desemba 2024
⏰ Muda: Saa 9:30 Alasiri (15:30 EAT)

πŸ”₯ Ni vita ya mwisho! Mombo Mji πŸ†š Manundu katika pambano la kukata na shoka!

πŸ‘‘ Mgeni Rasmi: Ndg. Athumani Nyamlani, Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF

πŸ™Œ Mashabiki wa soka, usikose kushuhudia historia inavyoandikwa. Jitokezeni kwa wingi kuungana nasi kwenye fainali hii ya kusisimua!

πŸ’₯ Korogwe imechagua kwa amani, sasa tufurahi soka!

21/12/2024

πŸ›‘ FULL TIME: MATOKEO YA NUSU FAINALI!

πŸ† KDFA Post Uchaguzi Cup

πŸ“ Uwanja wa Sokoni Stadium
⚽ Manundu 2️⃣ - 1️⃣ Kilole

πŸ”₯ Manundu wamefuzu kwa fainali baada ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya bao moja la Kilole katika mechi ya kusisimua! πŸ‘

πŸ™Œ Shukrani kwa mashabiki wote waliokuja kushuhudia nusu fainali hii kali. Fainali sasa ni kati ya Manundu na Mombo Mji! Jiandae kwa burudani zaidi.

πŸ’₯ Korogwe imechagua kwa amani, sasa tufurahi soka!

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Korogwe?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address

Korogwe