Lwangwa,Busokelo Mbeya 🇹🇿
Tanzania Travel Show
History|Culture|Tourism &Lifestyles
Mbugani Tenende 🛣️
Barabara ya Kikusya kwenda Ipinda hadi Matema,ukipita wakati huu utaona shughuli za Kilimo cha Mpunga zikiendelea katika mbuga hii maarufu wilayani Kyela.
Daraja la Tapio/Tapio Bridge
Daraja Hili lipo kata ya Kisegese,Halmashuri ya Busokelo linawaunganisha wananchi wa Busokelo na wananchi wa Kyela.
Salamu toka Tukuyu,Mbeya 🇹🇿
Green City
Ukisikia Mji wa Kijani,huku ndiko Kijani yenyewe iliko Hii ni Mitaa ya Lwambi kata ya Itete Halmashauri ya Busokelo,Wilaya ya Rungwe,Mkoa wa Mbeya 🇹🇿
Ngoma ya Asili
Hii ni ngoma ya asili inaitwa Kitwika kutoka Nchi jirani ya Malawi mpakani kabisa na wilaya ya Kyela,muundo wake ni unafanana kabisa na ngoma za Kinyakyusa.
Sababu ya ngoma za asili za Kinyakyusa kufanana au kuingiliana na ngoma za Malawi ni mchanganyiko wa historia, jiografia na utamaduni wa watu wa eneo hilo. Kwa ufupi, ni kwa sababu watu ni wale wale, mipaka imewatenganisha baadaye.
📍Busokelo,Mbeya 🇹🇿
Hali ya mvua na ukungu,kuanzia kituo cha mafuta lwangwa hadi Njiapanda ya Itete Hospital k**a ilivyochukuliwa leo Jioni tar 26/22/2025.
Salamu kuelekea siku ya Xmass
Tupo mitaa ya Sokoni Kuu Kyela/Market Square harakati za manunuzi ya sikukuu zinaendelea hapa Mjini.
Kityeputyepu cha Ngana
Hili ni daraja la kamba maarufu k**a kityeputyepu linalounganisha Wakazi wa Kata ya Ibanda na Kata ya Ngana (Kasumulu) Wilayani Kyela.
Kwa wale watumiaji wa barabara kuu ya kwenda Malawi ukishukia kituo cha Njiapanda Kasumulu ndipo unaenda moja kwa moja kilipo hiki Kityeputyepu.
Click here to claim your Sponsored Listing.