20/02/2026
MTAKUJA GETO AU HAMJI MAMBO MENGI HATUTAKI ๐คฃ๐คฃ
๐ค Habari | ๐ฎ Michezo | ๐ Burudani
Tunakuletea habari motomoto, michezo na burudani kali kila siku!
๐ฒ Jiunge nasi kwa updates zisizoachwa nyuma!
20/02/2026
MTAKUJA GETO AU HAMJI MAMBO MENGI HATUTAKI ๐คฃ๐คฃ
18/01/2026
UKICHEKA UNAPATA DHAMBI ๐ฅบ
01/10/2025
๐ข๐ก Mashabiki wenzangu wa Yanga ๐ก๐ข
Yale yaliyotokea Mbeya k**a ni kweli, basi baadhi ya mashabiki wamelewa na ushindi wa Yanga mpaka wakajisahau. Tujue mpira una matokeo matatu: kushinda, sare au kufungwa. Sasa k**a nyie mnaona sare haikubaliki, basi labda mnapaswa kuanzisha mchezo wenu wenye matokeo moja tu ya ushindi. ๐
Elimu ya ukocha sio lelemama โ ni ngumu sana, ndiyo maana kesho mtu anaajiriwa na keshokutwa anaondolewa. K**a unaona ni rahisi, basi jaribu wewe mwenyewe ukawe kocha wa Yanga ndipo utajue shughuli yake. Mpira sio maneno ya vijiweni, ni taaluma na kazi kubwa. โฝ๐ฅ
Tukumbuke tumetoka mbali โ kutoka kwenye bakuli hadi tulipo leo. Kuna watu wamefanya kazi kubwa, jasho na kujitoa kwa hali na mali. Tuwaheshimu, tusije tukawadhalilisha kwa sare moja tu. Ni aibu kuona mashabiki wanapiga kelele "hatumtaki kocha" wakati hata dakika 90 haziwezi kuwasomesha juu ya mpira. ๐คฆโโ๏ธ
Wale waliopiga kelele Mbeya, mimi nahisi si mashabiki wa kweli bali mamluki wenye njaa za tumboni. Uongozi wa Yanga ndio unajua nini kifanyike, sio nyie mnaokurupuka baada ya sare moja. Mpira sio kileo cha kila siku, ni safari ya damu, jasho na maarifa.
๐ข Yanga ni taasisi kubwa, si ya kuamuliwa na jazba za dakika chache. ๐ก
27/09/2025
Kocha Folz ameonyesha kwa vitendo kuwa ni mwalimu wa kiwango cha juu. Ushindi wa leo ni mwendelezo wa uthibitisho kwamba waliokuwa wakimsema walikosea. Yanga chini yake si timu ya majaribio โ ni timu yenye ubora, falsafa, na matokeo.
26/09/2025
๐ฆโฝ Wanasema Simba ni tajiri Afrika, kumbe tajiri wao ni bakuli la kuchangisha ๐. CAF imewapiga faini $85,000 (milioni 208) tu, tayari timu nzima imeishiwa power wanapiga hesabu za michango ya harusi ili kulipa deni.
Mdhamini wao sijui yuko wapi? Au naye kageuka k**a mdhamini wa kikopo cha mchele โ akiona mambo magumu anajificha chini ya meza. Hivi kweli klabu kubwa eti inaomba omba mitaani? Hii sio Simba SC, hii ni โSimba Social Club ya Tandale.โ ๐คฃ
Wamepewa adhabu ya kucheza bila mashabiki na bado wana hasira, kumbe kosa ni la mashabiki wao wenyewe. Yaani mnachoma moto nyumba halafu mnawaambia majirani waje kulipa mabati! ๐
Kwa hiyo msichanganywe na porojo zao, Simba ya sasa ni maskini wa hela, matajiri wa maneno matupu. Wacha Yanga ibaki ikiwapa somo la uhalisia.
25/09/2025
UJUMBE KWA WANAOJARIBU KUMSEMA KOCHA FOLZ
Wapo watu wanajiita wachambuzi wa mpira lakini ukiwasikiliza, unagundua hawajui chochote zaidi ya kuropoka. Wengine wamejipachika vyeo vya โmchambuziโ kumbe kazi yao kubwa ni kutafuta kiki kwa kuongea vibaya kuhusu kocha wa mafanikio wa Yanga, Folz.
---
๐น Folz Ni Kocha wa Kipekee
Tangu afike Yanga hajafungwa hata mechi moja. Ameweka nidhamu ya kimbinu, ameleta direct football โ pasi za mbele, runs za kasi, movement sahihi, na mwisho mpira unakuwa kambani. Sasa mtu akisimama hadharani na kusema kocha k**a huyu hafai, si bora akiri tu hajui mpira?
---
๐น Wachambuzi Wanaopinga
Hawa wanaomkosoa ni watu wa ajabu kweli:
Wanataka mpira wa manjonjo bila matokeo.
Wanataka kuongea ili wapate views, si kutoa uchambuzi wa kweli.
Ukweli ni kuwa wengi wao ni wakala wa Msimbazi waliotumwa kumchafua kocha wa mafanikio wa Yanga.
Kwa lugha rahisi: mtu akisema Folz hafai, basi huyo si mchambuzi โ huyo ni keyboard warrior mwenye ajenda.
---
๐น Hatari ya Kutojali Mafanikio Haya
Kocha huyu ni hazina. Dunia inamuona. Waarabu hawalali, wakisikia sisi wenyewe tunamchafua, si ajabu kesho wakaleta mamilioni na kumchukua. Tukibaki tunajuta huku tukijifariji kwa โtulikuwa tunamkosoa kwa sababu hakutoa speed dakika zoteโ. Huu utakuwa ujinga wa karne.
---
๐น Wajibu Wetu K**a Mashabiki
Mashabiki wa Yanga lazima tuamke. Tumupe heshima kocha wetu. Tuwasome vizuri hao wanaojiita wachambuzi. Wanaposema vibaya Folz, wajiangalie kwanza โ Yanga imekuwa timu isiyoshindwa chini yake.
Hawa watu wanaopiga makelele, k**a kweli wangepewa timu ya ligi ya vitongoji, wangetimuliwa kabla ya mwezi kuisha.
24/09/2025
๐น Falsafa ya Kocha
Kocha Folz ni muumini wa direct football. Hachukui muda kwenye pasi nyingi zisizo na matokeo. Falsafa yake inajengwa juu ya:
Pasi za kwenda mbele kwa haraka,
Harakati sahihi za wachezaji (runs) katika nafasi,
Movements za haraka ndani ya eneo la mpinzani,
Nia ya moja kwa moja ya kumalizia mpira kwa goli.
---
๐น Kipindi cha Kwanza
Mara nyingi Yanga huonekana kucheza kwa mtindo wa tahadhari, ikitumia muda mwingi kusoma mchezo. Hali hii huwapa mashabiki taswira ya kuanza vibaya, lakini kiufundi ni sehemu ya mbinu za kocha โ kufanya scanning na kusubiri muda sahihi wa kushambulia.
---
๐น Kipindi cha Pili
Hapo ndipo mabadiliko yake ya kimkakati huonekana. Anapoongeza kasi kupitia wachezaji wapya, timu hubadilika na kushambulia kwa vertical runs na kasi kubwa kwenye transitions. Ndipo magoli hupatikana kwa wingi.
Mfano ni mechi dhidi ya Pampa Jiji, ambapo kipindi cha pili kilileta matokeo ya 3โ0.
---
๐น Rotation na Kuficha Mbinu
Folz hapendi kikosi cha kudumu. Hutumia mchanganyiko tofauti kila mechi, jambo linalowafanya wapinzani washindwe kuandaa mbinu za moja kwa moja dhidi ya Yanga. Mfumo huu pia unawaweka wachezaji wote kwenye hali ya ushindani na utimamu wa mechi.
---
๐น Matokeo
Mpaka sasa hajafungwa tangu afike.
Wachezaji wote wanahisi ni sehemu ya kikosi.
Yanga inabaki kuwa timu isiyotabirika, yenye ubora wa kiufundi na kimkakati.
---
๐น Hitimisho
Folz si kocha wa mpira wa kupendeza macho kwa kasi ya mwanzo hadi mwisho. Ni kocha wa nidhamu ya kimbinu na matokeo. Mfumo wake unalenga kasi ya maamuzi, direct pe*******on, na mabadiliko ya kimkakati ambayo huleta matokeo chanya.
Kwa hivyo, hata pale mashabiki wanaposema โhawamuelewiโ, ukweli ni kwamba wanashuhudia Yanga yenye falsafa mpya ya soka la kimkakati na lenye tija.
19/09/2025
Watu wanasema kocha Folz hawamuelewi, eti anawachanganya ๐ค. Lakini sasa fikiria โ k**a hata mashabiki wa Yanga wenyewe wanachanganyikiwa, je wapinzani wataishije? ๐
Folz sio kocha wa kukalilika, na huo ndio mfumo wake! โก
๐ Mchezo wa kwanza akacheza tofauti
๐ Mchezo wa pili akabadilisha tena
๐ Ndani ya mechi moja, kipindi cha kwanza anakuja na kitu kipya, kipindi cha pili anakupa sura nyingine kabisa
Tazameni mechi na Simba โ alianza namna yake, akihitaji goli akaswitch mfumo aliocheza na timu ya Kenya kipindi cha kwanza, akapata bao ๐ฅ
, kisha akarudi kubadilisha tena. Huyu jamaa ni k**a โchameleon,โ kila dakika anatupa rangi mpya.
Hata wachezaji wake anaweka tofauti tofauti, hakuna anayeweza kusema ameshaelewa mfumo wake. Hii ni akili ya kipekee ya kocha wa kisasa. ๐ฅ
Kumbukeni msimu uliopita kocha wa Al Ahly naye alikuwa na mfumo k**a huu โ anaweza kukaa kulinda kimya kimya, ukimfunga anarudisha papo hapo, halafu anarudi tena kulinda. Hivi ndio makocha wa akili wanavyocheza, wanakuchanganya mpaka unakosa mwelekeo.
โ
Kwa kifupi, Folz si kocha wa kawaida. Yanga yake ni timu inayobadilika kila dakika, na ukidhani umemuelewa tayari kashakubadilishia mchezo. Wapinzani wanabaki kwenye sintofahamu, na hapo ndipo nguvu ya Yanga ilipo ๐๐.
18/08/2025
SIMBA SC WAMEGEUZA MISRI KUWA KABURI LA MAZOEZI YAO ๐โฝ
Mechi ya kwanza walipigwa 7-1, ya pili tena wakafungwa 4-3 na ENPPI ๐ณ. Jumla michezo miwili tu wamevuna mabao 11 kwenye nyavu zao.
Hii sio pre-season tena, ni tour ya vipigo ๐คฃ. Halafu wanaanza kuficha matokeo eti mashabiki wasijue, kumbe hii ni zama za mitandao kila kitu kinavuja ๐ฅ.
Kwa hali hii safu ya ulinzi ni k**a wavu uliotoboka, washambuliaji nao hawana makali ya kuokoa. Hakuna mbinu, hakuna ubora โ Simba wamebaki majina tu, uwanjani ni Chui wa Karatasi ๐๐.
Msimu mpya unakuja, lakini dalili zinaonyesha ni safari ya machozi
17/08/2025
Wapo baadhi ya wana Simba ambao wameamua kuvaa joho la uongo la โUyangaโ wakijifanya ni sehemu ya familia kubwa ya Yanga SC. Wanafanya hivyo kwa hila moja tu โ kujaribu kuipandikiza chuki, kugombanisha viongozi, na kuichafua sura ya timu ya wananchi. Wanamsak**a hata Injinia Hersi wakidhani watavuruga mshikimano wetu, kumbe nia yao ni fitna tupu.
Lakini nawahakikishia, Wanayanga tumesha watambua! Hakuna vazi la kijani na njano linaloweza kuficha mioyo yao ya wekundu. Hata wakijidai ni sisi, roho zao zinaonyesha wazi kuwa ni maadui wa ndani.
Wanayanga tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikikano wetu na tusikubali hila za โSimba waliovaa ngozi ya Yanga.โ Historia imeonyesha, yeyote anayejaribu kuivuruga Yanga huishia aibu. Yanga ni taasisi, ni familia, na ni nguvu ya pamoja โ haitabomolewa na mbinu za kifitini