25/06/2025
Ubaya ubwela
Sports bar ๐ช๐ช๐
25/06/2025
Ubaya ubwela
08/03/2025
07/03/2025
Kuna Nyakati tofauti tofauti iliyopita kwenye Ardhi ya soka Tanzania Uwezo na vipaji vya washambuliaji mbali mbali wamepita ligi kuu Tanzania bara na baadhi bado wapo Mfano John Bocco, Fiston Mayele, Meddy Kagere yupi kwako alikuwa Mshambuliaji wako pendwa..?
07/03/2025
Hilo ndio kikosi cha wachezaji wanao pewa sifa azistahili mpaka sasa ligikuuu katika tim tatu simba yanga azam
1. Mohammed mustard
2.kelvin kijiri
3chadrack boka
4.abdul razak Hamza
5.yoro
6.fabrice ngoma
7.kibu
8.Jean charles
9.ateba
10 nassor saadun
11.prince dube
Naona awa watu wapewa sifa zisizo stahili mfano kibu na chasambi mukwala na ateba dube na mzize yani akuna usawa Ndo ivo kila mtu ana nyota yake
15/01/2025
Nyota wa Yanga wanatakiwa kuongeza umakini wakati wakipambania ushindi, Jumamosi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger kutokana na rekodi ya ajabu ya mwamuzi, Patrice Milazare kutoka Mauritius ๐ฒ๐บ ambaye anatarajiwa kuamua mchezo huo.
Katika michezo mitatu aliyoamua msimu huu, rekodi ya Milazare ni ya kutisha, hakuna timu yoyote iliyofunga bao, hivyo kocha wa Yanga, Sead Ramovic na vijana wake wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanabadilisha rekodi hiyo kwani uhitaji wao wa kushinda ni mkubwa kulinganisha na wapinzani wao MC Alger hata sare inawabeba.
Katika michezo aliyochezesha msimu huu, Milazare aliongoza mechi mbili muhimu za kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, Oktoba 10, 2024, Ghana walikuwa wenyeji wa Sudan matokeo yalikuwa 0-0.. Mwezi mmoja baadaye, Milazare alichezesha mechi nyingine kati ya Libya na Benin matokeo 0-0.
Mchezo wa tatu wa msimu huu kwa Milazare ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, na MC Alger walicheza ugenini dhidi ya TP Mazembe huko DR Congo. Katika mechi hiyo, hakuna timu iliyofunga bao na mechi hiyo ilimalizika 0-0.
Kulingana na rekodi za mwamuzi huyo, kila hatua itahitaji umakini wa ziada ili kupambana na si tu wapinzani wao MC Alger, bali pia na mwamuzi huyu ambaye ni k**a vile โmfalme wa suluhu
14/01/2025
Kwenye viwango vya timu bora barani Afrika chini ya CAF, Yanga wana alama 34 mpaka sasa na ikitokea Yanga wamefuzu kwenda robo fainali watafikisha alama 39 na kuzishusha timu 2 kwenye top 10 ya CAF. Na ikitokea Yanga wamefika nusu basi wataingia 5 bora ya CAF. Misimu 3 ya KIBABE.
06/01/2025
Kimahesabu Ya Yanga ni kushinda mechi mbili zilizobaki ila Kuna Ugumu mkubwa Sana nauona,,,,na Huenda yakajirudia Yale ya CR BELOUZIDAD,,,,Maana Yangu ni Hii,,,,,,
MC Algeria ana Point 5 endapo atashinda Mechi ijayo na Mazembe atakuwa na Point 8,,,,,,,,,,,
Yanga Akicheza na Al Hilal ikitokea Yanga kapata Sare Atakuwa na Point 5,,,,,
Mechi ya Mwisho itakuwa Benjamin Mkapa,,,,ambapo Yanga ataingia Uwanjan akiwa na Point 5 hivyo atatakiwa Kumfunga MC Algeria Goli 3_0 atakuwa ikitokea Hivyo Yanga Kafuzu ila Kikubwa ni Mechi ya Al hilal tusipoteze Tupate Point la Sio Tatu Bas Moja Alaf mechi ya mwisho,,,,,,Iwe Afe kipa Afe Beki MC Algeria Afungwe Chuma 3-0
Wengi mnasema Al Hilal anafungika kwake ila sio Rahisi k**a wengi mnavyofikiria,,,,,Jamaa Wapo vzr sana nadhan mpka hapo Kuna watu wamenielewa k**a Sio point Tatu bas tupate Moja ๐
Huenda yakajirudia Yale Yale ya CR BELOUZIDAD,,,,,kwamba Head to Head itaamua
๐๏ธSpSports extra large
04/01/2025
๐๐ฅ๐๐๐๐๐ก๐ ๐ก๐๐ช๐ฆ: ๐๐๐๐ ๐๐ก๐ง ๐ ๐ญ๐๐ญ๐ ๐๐จ๐ฉ๐๐ ๐๐ช๐ ๐ก๐ ๐ ๐๐ฆ๐๐๐๐๐๐ ๐ช๐ ๐ฌ๐๐ก๐๐ ๐ฆ๐
Mashabiki na Wanachama wa Yanga waishio Jijini Dar ea Salaam, wamekubaliana kuwa siku ya kesho wanaenda kuvamia Duka la Mchezaji wao Clement Mzize lililopo Sinza ili Kununua Mzigo wote uliopo Dukani na kuacha Duka likiwa Tupu.
29/12/2024
Shida nyingine imewasili hapa mjini,timu nyingi zimenza kunyanyasika zikikutana na Yanga.
Chini ya makocha wawili waliopita (Nabi & Gamond) Yanga walicheza mpira wa pasi nyingi,Yanga walikuwa na utaratibu wa kuwatongoza wapinzani kwa pasi nyingi kabla ya kufunga magoli (TIP TAP FOOTBALL) ila chini ya Ramovic tunashuhudia pira โGegen-Pressingโ au kwa kizungu tunasema โCounter-pressing).
-Yanga ya Ramovic haitaki pasi 10 kufika kwenye lango la mpinzani,badala yake inahitaji pasi tatu hadi nne kufika kwako na kukufungaโ๏ธ
-Yanga ya Ramovic haitaki back-pass wala Sideway pass,mchezaji akiiba mpira ni kwenda mbele Yanga wako direct sanaโ๏ธ
-Yanga ya Ramovic haipigi cross nyingi za juu,badala yake mashambulizi mengi yanatokea pembeni kwa fullbacks na wingers kisha zinapigwa V-pass kwenye 12 na viungo washambuliaji wanafungaโฆ..rejea magoli mawili ya Pacome leoโ๏ธ
JINSI GANI YANGA WANAWEKA MTEGO KABLA YA KUFANYA PRESSING?
Mara nyingi tumezoea kuona mstari wa kwanza wa namba 9 na 10 ukianzisha pressing kwa walinzi wa timu pinzani,ila Yanga ya Ramovic,inasubiri wapinzani wafike kati kati ya uwanja kisha viungo wazuiaji (Aucho na Muda) wanaweka pressure kwa mchezaji mwenye mpira huku walinzi wa kati (Job na Bacca) wakisogea kati kati ya uwanja kukata passing optionโฆ..baada ya kuiba mpira unapigwa pembeni kwa mawinga na fullbacks kisha shambulizi linaanzia hapoโ๏ธ
Ndugu zangu huu mpira wa Yanga una magoli mengi ya โTurnoversโ wapinzani wanafanyishwa makosa mengi na kuhadhibiwa.
25/12/2024
Nimeanza kuelewa kwanini Yanga waliwakomalia Widad Casablanca.
Ukweli ni kwamba Mzize ni mchezaji mwenye thamani kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Mzize anacheza K**a right-winger,Left-winger na number 9.
Mzize anakupa kasi,mashuti,pressing,magoli na nguvu ya kukimbia k**a kichaa uwanjaniโฆ..siyo kila mchezaji ana mapafu k**a Mzize.
Leo kaweka goli la 5 la NBC Premier League.
Ni basi Watanzania tumeamua kuwasifia akina Dube,Ateba na Mukwala Ila Mzize ni mshambuliaji bora mzawa kwa sasa.
Msimu huu ametulia sana mbele ya goliโฆ.na tukumbuke huyu bado ni kijana Wa miaka 20
Anaandika Mchambuzi wa Michezo kutoka Crown FM, Hans Rafael.โ๏ธ
25/12/2024
๐จโ ๏ธHaitochukua muda Wananchi wataanza tena kurejea ule mpira wao na mabao yao, haitochukua muda kabla Clement Mzize aanze kupokea ofa nyingi huko nje, haitochukua muda kuanza kutenganisha maji na mafuta, haichukui muda kugundua Prince Dube kamba zote hajafunga penati, haitochukua muda timu zitaanza kuitwa Matawi.
K**a hii hali itaendelea haitochukua muda jina la GSM na udhamini kuanza kuwa kiitikio kwenye ule wimbo maarufu, haitochukua muda kusikia Marefa na TFF wote ni Wananchi, haitochukua muda sana๐