12/05/2026
Hii hapa nyingine kubwa kutoka Msimbazi kuja kwako Mwanasimba kindakindaki.
Sasa unaweza kuwapa burudani wakupigiao kwa kufanya goli la Chama dhidi ya mtani kuwa muito wa simu yako. Nani kwenye simu yako unatamani awe wa kwanza kukutana na goli lile la mwaka wa mbele? 😄
11/05/2026
Clean sheet ya 10 kwa Djibrilla Kassali kwenye Ligi Kuu.
*Djibrilla Kassali "Mahamadou Tanja"* - Golikipa wa Simba SC 🇳🇪
*AMECHEZEA TIMU 2 KUBWA MPAKA LEO 2026:*
1. *AS FAN* 🇳🇪 - _Association Sportive des Forces Armées Nigériennes_
*Msimu:* 2024/2025
*Namba:* 16
*Ligi:* Niger Premier League - Niamey
2. *Simba SC* 🇹🇿
*Amejiunga:* 20/01/2026
*Namba:* 39
*Mkataba:* Bado haujafahamika
*Umri:* Miaka 29, alizaliwa 05/07/1996 8256
---
*MUHTASARI WA KAZI YAKE:*
**Timu** **Mwaka** **Maelezo**
**AS FAN** 2024/2025 Timu ya Jeshi la Niger. Alicheza k**a golikipa namba 1
**Simba SC** 20/01/2026 - Sasa Usajili wa dirisha dogo 2026. Anashindana na Moussa Camara
fb29e573
*Timu ya Taifa:* Niger - Mechi 28, Clean sheets 11 8256
*Angalizo:* Wapo wachezaji 2 wenye jina k**a hilo. _I. Djibrilla_ wa *Zira FK* Azerbaijan ni mtu tofauti. Wa Simba ni *Djibrilla Kassali Djibo* au *Mahamadou Tanja*. e1f1e573
*Sasa anapambana na CAF Champions League* - Alicheza dakika 360 mechi 4 msimu wa 2025/2026. e12f
*Swali kwa mashabiki Geita:* Mnamuona anafaa kuwa namba 1 Simba au Moussa Camara abaki?
* *
11/05/2026
*Simba Sports Club ilianzishwa rasmi *MWAKA 1936* 🦁📅*
*HISTORIA FUPII YA MAJINA:*
1. *1936:* Ilianzishwa ikiitwa *Queens* - na vijana wa Kidato cha Pili *Dar es Salaam Secondary School*
2. *1940s:* Ikabadilika jina kuwa *Sunderland* - kwa heshima ya timu ya Sunderland ya England
3. *1971:* Ikabadilishwa rasmi kuwa *Simba Sports Club* - jina tunalolitumia hadi leo 2026
*MAANA YAKE:* Simba ina *miaka 90* mwaka huu 2026. Ni moja ya klabu kongwe zaidi Tanzania baada ya Yanga 1935.
*WALIOANZISHA QUEENS 1936:*
- *Sheikh Thabit Rage* - Kocha/Mchezaji wa kwanza
- *Mzee Ali Said Chweya*
- *Mzee Salum Nassor*
- Vijana wa shule ya sekondari Dar
*Sababu ya kuanzishwa:* Kulikuwa na ubaguzi kwenye timu za wakoloni, hivyo vijana wazalendo wakaamua kuanzisha timu yao.
*Swali la ziada kwa mashabiki wa Geita:*
Je, mnajua *Simba ilicheza mechi yake ya kwanza wapi mwaka 1936*?
* *
11/05/2026
🏆 CAF imetangaza rasmi nchi 12 zitakazopata nafasi nne za uwakilishi katika mashindano ya vilabu Afrika msimu ujao. Mataifa hayo yatakuwa na timu mbili kwenye CAF Champions League pamoja na timu mbili kwenye CAF Confederation Cup.
🇹🇿 Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopata nafasi hizo kutokana na ubora wa vilabu vyake kwenye mashindano ya CAF katika misimu ya hivi karibuni.
📋 NCHI 12 ZILIZOPATA NAFASI YA TIMU 4 CAF NI:-
1️⃣ 🇩🇿 Algeria
2️⃣ 🇦🇴 Angola
3️⃣ 🇨🇮 Côte d’Ivoire
4️⃣ 🇨🇩 DR Congo
5️⃣ 🇪🇬 Egypt
6️⃣ 🇲🇱 Mali
7️⃣ 🇲🇦 Morocco
8️⃣ 🇳🇬 Nigeria
9️⃣ 🇿🇦 South Africa
🔟 🇸🇩 Sudan
1️⃣1️⃣ 🇹🇿 Tanzania
1️⃣2️⃣ 🇹🇳 Tunisia
⚽ Hatua hiyo inaendelea kuonyesha ukuaji mkubwa wa ushindani wa soka la vilabu katika bara la Afrika.
🤔 Je, unaamini vilabu vya Tanzania vitaweza kutumia vizuri nafasi hizi nne za CAF na kuifikisha nchi mbali zaidi Afrika msimu ujao? 🇹🇿⚽
Follow:jamesalexsports
11/05/2026
Kuhusu tuzo ya Simba Sc Katibu Mtendaji wa BMT ambao ni watoa tuzo Bi Neema Msitha amesema haya:
“Nadhani tuna kazi kubwa sana ya kutoa elimu baada ya Mashabiki wa Yanga kulalamikia tuzo kubeba Simba, vigezo vyetu sisi BMT ni michuano ya Kimataifa kwa maana hata ubebe vikombe 200 ndani tunataka kujua Kimataifa umefanya nini, hakuna timu tuliyoipima pale kwa vigezo vya ndani bali Kimataifa”
Neema Msita, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa akijibia kwanini Yanga hajashinda mbele ya Simba tuzo ya Klabu bora.
#
10/05/2026
*🔥 UTABIRI WA MECHI - KIPINDI CHA PILI 🔥*
_IDARA YA HABARI SIMBA MKOA WA GEITA_ 🦁
Wana Simba, mapumziko yameisha. Tunawapa nafasi ya kushinda zawadi sasa hivi!
*JIBU MASWALI HAYA 3 KUHUSU KIPINDI CHA PILI:*
1. *Goli la kwanza kipindi cha pili atafunga nani?* Taja jina la mchezaji wa Simba
2. *Kipindi cha pili kitaisha Simba mangapi?* Mfano: 1-0, 2-1
3. *Goli hilo litafungwa dakika ya ngapi?* Dk 46 hadi Dk 90
*ZAWADI:* Washindi *3 wa kwanza* wenye majibu sahihi watapata *vocha ya Tsh 2,000*
*SHERIA ZA KUSHIRIKI:*
1. Jibu mara moja tu. Ukihariri, ume-disqualify.
2. Utabiri unafungwa *Dk 50* ya mechi. Baada ya hapo hatupokei.
3. Atashinda aliyejibu sahihi yote 3. K**a hakuna, tunachukua aliyekaribia zaidi.
*MFANO WA KUJIBU:*
`1. Kibu 2. 1-0 3. Dk 67`
Weka utabiri wako SASA 👇🏽
Mechi imeshaanza!
*
10/05/2026
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi nchi 12 zitakazopata nafasi nne za uwakilishi katika mashindano ya vilabu Afrika kwa msimu ujao, hatua inayodhihirisha kuongezeka kwa ushindani wa soka la vilabu barani Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kila taifa lililochaguliwa litapeleka timu mbili katika michuano ya CAF Champions League pamoja na timu mbili kwenye CAF Confederation Cup. Tanzania imefanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo kutokana na mwenendo mzuri wa vilabu vyake katika mashindano ya CAF katika misimu ya hivi karibuni.
Mataifa mengine yaliyopata nafasi hizo ni Algeria, Angola, Côte d’Ivoire, DR Congo, Egypt, Mali, Morocco, Nigeria, South Africa, Sudan na Tunisia.
Mafanikio hayo yanaonyesha namna soka la Tanzania linavyoendelea kukua na kupata heshima kubwa katika anga la kimataifa, huku vilabu vya nchi hiyo vikiongeza ushindani dhidi ya mataifa yenye historia kubwa ya soka Afrika. Hatua hiyo pia inatarajiwa kuongeza ari kwa vilabu vya Tanzania kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa
#
10/05/2026
Nimapumziko mafupi baada ya kimaliza kusimamia chaguzi zote mkoa mzima
wa geita kuwapata viongozi wawilaya viongozi wampito.
wakati kati ndio mwenyekiti simba mkoa
wapembeni kushoto ni mjumbe wak**ati tendaji mkoa na namwenyekit k**ati ya ushindi simba mkoa geita kulia ni msemaji Simba mkoa geita
#
10/05/2026
🦁 M A T C H D A Y 🦁
🏆NBC Premier League
®️ RD 22
🆚️ Tanzania Prisons
🏟 KMC Complex
🗓 10.05.2026
⏰️ 19:00(01:00 jioni)
📺 Azam Sports 1HD
Yakoub anazidi kuimarika anaendelea na mazoezi binafisi
Simba SC imetwaa tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume wa mwaka katika Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) 2025 zilizofanyika Jijini Dar es salaam huku mafanikio hayo yakidhihirisha mwendelezo wa ubora wa Klabu hiyo katika mashindano mbalimbali ya ndani na Kimataifa kwa mwaka 2025.
Tuzo hiyo imetolewa Mei 9, 2026 katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es salaam ambapo imekabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, na kupokewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Zubeda Sakuru mbele ya Wadau mbalimbali wa michezo Nchini.
Katika tuzo za Wanamichezo binafsi, Mwanariadha Alphonce Simbu ametwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kiume wa mwaka huku Stumai Abdallah wa JKT Queens na Timu ya Taifa ya Wanawake akitwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa K**e wa mwaka kutokana na mafanikio yao katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Kwa upande wa Vijana, Raymond Francis ametangazwa kuwa Mwanamichezo Bora Kijana wa Kiume wa mwaka huku Rose Kataboy akitwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Kijana wa K**e baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo yao kwa mwaka 2025.
Mbali na Wanamichezo, tuzo nyingine zilizotolewa ni pamoja na Kocha Bora wa Kiume aliyekwenda kwa Anthony Mwingereza, Kocha Bora wa K**e aliyotwaliwa na Esther Chabruma, Mwamuzi Bora wa Kiume aliyeshinda Shabani Mahobonya, Mwamuzi Bora wa K**e aliyokwenda kwa Dariso Mwidadi pamoja na tuzo za Wanahabari wa michezo zilizotwaliwa na Fatma Chikawe na Khalid Msabaha.
https://whatsapp.com/channel/0029Vb5KkB2KLaHr2jPM7N19
09/05/2026
SELEMAN MATOLA🎙️
Kocha Matola akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons.
"Tumehama Isamuyo kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ambapo kwa sasa mvua zimekua nyingi na za mara kwa mara, hivyo tumehamia KMC ili kuweza kucheza katika mazingira mazuri muda wowote" Seleman Matola
MPANZU TUZO INAITA🔥🦁
Elie Mpanzu mpaka sasa ana Assist 7 nyuma ya Feisal mwenye 8 lakini ni mchezaji amecheza mechi chache lakini mchango mkubwa wa mbao
K**a kakikaza zaidi akaenda n mwendo huu kwenye kuchagua M.V.P wajipange kwa sababu anakuja kwa kasi saaana, Combination yake na Chama ni ya 🔥
Bado zipo mechi nyingi lolote litatokea kuhusu tuzo na ataendelea kuwatesa Gongowazi 🐸 kwenye mioyo yao.
Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amepongeza kiwango na muunganiko wa viungo Clatous Chama na Elie Mpanzu baada ya wawili hao kuendelea kuwa tishio katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Barker amesema uzoefu na ubunifu wa Chama umeongeza tofauti kubwa ndani ya kikosi hicho huku Mpanzu naye akiendelea kuimarika kadri msimu unavyoendelea.
“Chama ana utulivu mkubwa na ubunifu wa hali ya juu. Mpanzu naye ameendelea kukua na sasa wanasaidiana vizuri kutengeneza mashambulizi hatari,” alisema Barker.
Katika michezo ya karibuni, wawili hao wamehusika moja kwa moja kwenye mabao muhimu dhidi ya Singida Black Stars, Young Africans SC na JKT Tanzania.
https://whatsapp.com/channel/0029Vb5KkB2KLaHr2jPM7N19