26/03/2026
PESA NGUMU SANA WAZEE,SIO MASIHARA.
Siku moja way back 2018 iyo mwanzoni mwanzoni! Jua kali kinoma noma Dar es Salaam,maeneo ya Tegeta kwa Ndevu pale upande wa kushoto k**a unaenda town kwa maana ya Kariakoo!
Mzee unaambiwa nime tandika mezani sendo za kina dada za spesho,nasubiri kupiga hela.ππ
Unaambiwa nilikaa kuanzia saa3 asubuhi,nikaagiza chai na mchana ilivofika nikaagiza nikala..kimbembe kwenye kulipa sasa. Nakwambia sikuuza hata pisi moja. Nimekaa mpaka saa1 jioni wateja wanaleta dharau tuπ kila wakipita mezani kwangu wanazigusa tu bila kuongea ata kuulizia bei k**a wanaaga maiti vileπ€¦.
Oyaa nilipata mawazo kinyama yani,nikicheck uko home mama mtu ana kitumbo ndiiii wa leo wa kesho alaf uku mzee baba nanga ina paa!π₯²π₯²
Stori za hapa na pale sasa washkaji kujipa moyo hili life mpaka lini?? Badae nikakaa pembeni kidogo,yaani akili imeganda k**a sielewi ninacho taka kufanya. Nikampigia mwanangu mmoja ivi familia yangu kabisa yupo hapa town ila mwenyeji wa Iringaπ.
Nikamuuliza ivi magari ya Njombe saiv napata?? Akaniambia oooh fresh saiv yana kesha Mjomba Magu karuhusu. Uyooooo mzee nikafunga chap chap roba langu nikaweka Stoo na Masai nikampanga natafuta chenji nimletee jero lake la kulindia mizigo mie uyoooo kwenye daladala la Ubungo Terminal enzi izo!! π€¦π€¦
Nimefika ivi k**a upepo mzee konda kanipa tiketi yangu kwenda Njombe. Imefika saa2 na nusu iv Usiku ndinga linakata upepo tu,miti inarudi nyuma kwa spidi kali na sisi tuna yeya mbele tu! Nililia sana iyo siku zile za kimya kimya ila machozi tu ndo yana tiririka, nimekaa dirishani na pisi moja ivi mpaka ikawa inaniuliza una shida gani kaka??πββοΈπββοΈ
Basi uongo uongo mwingi nikamwambia nimepata msiba nimefiwa na pacha angu uko Njombeπ€¦π€¦ Daaah pole nyingi ila kiukweli nilikua na mawazo sana. Nikamtumia sms Mama mtu nikampanga bhn kuna mfanyabiashara mwenzetu apa kakata moto tunampeleka kwao Iringa alaf nikazima simu.
Unaambiwa saa10 Alfajr mzee ndo tunaingia Iringa mjini. Baridi inagusa kinoma noma,kila mtu kavaa Sweta ama Koti zito mie uyo sikujiandaa kwa lolote mzee nina jezi ya Simba nyepesi kinoma baridi linapiga mpaka mifupa inagoma kutoa ushirikiano mzuri unavotembea. Lile Bus bana kumbe linaishia Iringa tu ikabidi tufaulishwe kwenye chuma ya Mbeya ili tushuke njiani watu wa Njombe. Ndinga lilikua linaondoka saa12 asubuhi...bas nikaanza kutafta msosi pale uku tunasubiri muda ufike tuondoke zetu Njombe. Chakula cha Iringa Stendi pale hasa usiku ni wali maharage na chai tuπππ
Bas bana,saa12 na Nusu ivi asubuhi walee Bus likaanza kukata upepo. Kutoka Iringa hadi Njombe ni k**a masaa 3 hadi 4 kwaiyo kwenye saa3 na Nusu ivi kutokana na ramani niliyokua nayo nikashuka nshwaaa Njombe iyo mwanzoni mwanzoni tu mie sikuenda hadi mjini uko.π₯±π₯±
Jua limeshatoka ila baridi bado ile ile mzee. Oyaa niliteseka kinoma iyo siku. Muda wote huo sijawasha simu,nahofia sms za mama mtu zikianza kutiririka unaweza kugeuza safari bila kufika mwishoππ
Basi nikaanza kwenda natembea mdogo mdogo kwenda SEHEMU husika kufuata PESA zangu.ππ
OYAAAAA Weee...nilikuta watu wengi vibaya mno. Unaambiwa kwanza k**a umefika hospitali vile wagonjwa wa kila aina wapo. Wasaka UTAJIRI k**a mimi tupooo...walioenda kuwaroga wapenzi wao watulie kwenye ndoa wapoo...walio enda kuwarudisha wapenzi wao walio achana wakati bado wanapendana wapo kibaooo.
Wenye kesi za mauaji wanafuta ushahidi wapoooo. Wenye Ngoma wanao amini wamerogwa na jirani wapo kibaoooo mpaka unawaza huyu si awahi tu hospitali jamani?? π€¦π€¦π€¦
Mzee ile foleni niliyo ikuta nilikaa siku3 kavu bila kumuona mhusika. Unaambiwa ngome ni kubwa mpaka kuna wodi kabisa na guest za kulala humo k**a hautaki kulala kwenye trubai au kulala kwenye "kimunya" sababu ya baridi kali ππ
Siku ya 4 mzee ndio zamu yangu ikafika ya kuonana na yule Mzee...Oyaaaa Mmmmh NGOJA KWANZA NARUDI KUMALIZIA....π€¦π€¦π€¦