Vimbwanga Vya Chuoni

Vimbwanga Vya Chuoni

Share

"Kutoka Lecture Room mpaka Hostel. Yale yote yanayofichwa chuo, hapa ndipo kijiwe chake. Simulizi, Visa, na Vituko vya Bumu. Karibu Kampasi! πŸŽ“πŸ”₯"

17/05/2026

Mwanza 101

17/04/2026
15/04/2026

Wakishua mmeelewa nini hapo???

14/04/2026

#​"Hivi 'Kuku wangu nimemchinja' kwa kingereza inakuwaje? πŸ˜‚ Maana huyu mshikaji kachanganyikiwa kabisa! πŸ‘‡"

25/03/2026

Sehemu ya 1: "SIRI YA CHUMBA NAMBA 302"
GPA VS PENZI LA SIRI
"NILIDHANI NIMEPAKIWA KWENYE BODABODA KWENDA 'HOSTEL' KUPUMZIKA BAADA YA MTUHAN WA UE, KUMBE NDIO NAANZA SAFARI YA KUIPOTEZA NDOA YA DEAN WETU WA WANAFUNZI..."
(The Story - Sehemu ya Kwanza):
Ilikuwa ni Jumanne ya saa 11 jioni, jua la Chuo Kikuu likiwa limeanza kuzama. Nilikuwa nimechoka vibaya baada ya pambano la saa tatu la mtihani wa Cost Accounting. Nilichokuwa nawaza ni kufika hostel, nile "Wali-Maharage" wangu, kisha nilale mpaka asubuhi.
Nikiwa nimesimama getini namsubiri bodaboda wangu wa kila siku, gari aina ya Range Rover nyeusi ilipaki mbele yangu. Kioo kikashuka taratibu. Alikuwa ni Dr. Malisa, Dean wetu wa Wanafunziβ€”mwanaume ambaye chuo kizima kinamheshimu kwa msimamo na ukali wake.
"Sophy, unapokwenda ni mbali na giza linaingia. Ingia nikutupe hostel," alisema kwa sauti yake ya mamlaka lakini safari hii ilikuwa na kaukaribu fulani.
Sikuwa na hiyana, nikaingia. Lakini tulipoingia barabara kuu, Dr. Malisa hakukata kona ya kuelekea hostel. Alinyoosha kuelekea upande wa mjini.
"Doctor, mbona tunapita huku?" nilimuuliza kwa sauti ya kutetemeka.
Alitabasamu kidogo, tabasamu ambalo sijawahi kuliona darasani. "Kuna mzigo wangu nataka niuchukue kule 'Apartments' za jirani, nisaidie kuubeba kisha nitakurudisha. Usijali."
Tulipofika kwenye jengo lile la kifahari, chumba namba 302, Dr. Malisa alifungua mlango na kuniambia niingie. Nilichokikuta ndani hakikuwa "mzigo" wa vitabu wala mafaili.
Kwenye kochi la sebuleni, alikuwa amekaa Sarah, rafiki yangu kipenzi (Roommate wangu) ambaye aliniambia anaumwa yuko hostel amelala. Alikuwa amevaa "Night dress" nyepesi, na kwenye meza kulikuwa na chupa ya Wine na glasi mbili.
Sarah alistuka kuniona, akasimama haraka. Lakini kabla hajasema lolote, Dr. Malisa alifunga mlango kwa 'lock' ya ndani, kisha akavua koti lake na kusema...
"Sophy, karibu kwenye familia. Sasa hivi siri ya Sarah ipo mikononi mwako, na siri yako inaanza sasa hivi..."
Moyo ulinitoka. Nilijua hapa si salama, lakini mlango ulikuwa umeshafungwa.
ITAENDELEA SEHEMU YA 2...Je, unahisi Dr. Malisa ana mpango gani na Sophy? Na kwa nini Sarah (Roommate) yuko pale?
K**a unataka nishushe SEHEMU YA 2 saa hivi, dondosha comment ya "NEXT" hapa chini! #

25/03/2026

"UNA ROOMMATE AU UNA 'GENERATOR' NDANI YA CHUMBA? πŸ˜‚πŸ”Š
Kuna kipindi unatamani kurudi hostel ukapumzike baada ya 'lecture' za saa tisa, unachochea mlango, unazima taa, unajifunika shuka... halafu ghafla unasikia: 'PRRRRRRRRRRR-KHAAA! PRRRRRRRRRRR-KHAAA!' πŸ€¦β€β™‚οΈ
Wakuu, maisha ya hostel yana mitihani mingi, lakini hakuna 'suplementary' ngumu k**a kupangiwa roommate anayekoroma utadhani anasaga kokoto kwa meno!
Yangu yalinikuta mwaka wa kwanza. Nilipangiwa jamaa mmoja anaitwa 'Chidi'. Mchana Chidi ni mpole, msafi, na anaongea kwa sauti ya chini k**a anaomba mkopo. Lakini akigusa tu mto... jamani!
Ile sauti inaanza k**a pikipiki inayopandisha mlima, halafu inabadilika inakuwa k**a sauti ya kikatakata miti (Chainsaw). Kuna muda unahisi kuta za hostel zinatetemeka na bati zinacheza! πŸ˜‚
Nilijaribu kila mbinu:
Mbinu ya Kukohoa: Nikawa nakohoa kwa nguvu k**a nimekwama mfupa ili ashtuke... jamaa anageuka upande wa pili halafu anaongeza 'volume' ya Turbo! 🏎️
Mbinu ya Kelele: Nikawa nagonga kitanda... anashtuka sekunde mbili halafu anaanza tena 'Remix' ya ajabu.
Mbinu ya Ushahidi: Siku moja nilikata tamaa, nikarekodi ile sauti yake, asubuhi namuekea asikie... akasema: 'Huyu sio mimi, huyo atakuwa ni mchawi anapita koridoni!' πŸ˜‚
Yaani roommate anashindwa kujitambua mpaka anasingizia wachawi wa kampasi!
JE, WEWE USHAWAHI KUPANGIWA 'GENERATOR' NDANI YA ROOM? πŸ˜‚ AU WEWE NDIO MTU WA KUKOROMA? πŸ‘‡ TAJA CHUO CHAKO NA MBINU ULIYOTUMIA ILI UPATE USINGIZI!
Institute of Accounting

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Mwanza
Mwanza