Zingo Sports

Zingo Sports

Share

A Digital Media Platform, Convey Trusted Sports News, Player's Journey and Life style & we Discover raw Talent.

04/04/2026

| Erling Haaland aliweka chuma mbili za haraka, Man City ikiwa inaongoza mabao matatu kwenye mchezo wa robo fainali ya FA Cup, dimba la Wembley.

Baada ya City kubeba taji la Carabao Cup mbele ya Arsenal, je anaweza kubeba na FA CUP kwa wapinzani waliopo?

Wapinzani waliopo robo fainali.

1. Kati ya ( Arsenal Vs Southapton )
2. Chelsea vs Port Vale
3. Westham

Kuna mpinzani anaeweza kumzuia Man City kutobeba taji la FA msimu huu? K**a Arsenal akifika fainali, anaweza kupoteza fainali mbili dhidi ya City?

Cc | .sports_

04/04/2026

| Mapambano ya wababe wa u*ito wa juu Duniani yanaendelea, leo kwenye ukumbi wa The 02, Uingereza, lnapigwa pambano kati ya Derick Chisora ( Worrior ) dhidi ya Bronze Bomber, Deontay Wilder, moja ya pambamo kali sana.

Wilder ataendeleza kuwachapa watu kwa KOs mbele ya Chisora ambaye anapenda sana vita akiwa ulingoni?

"Napigana nikiwa nyumbani ( Great britain ), nikiwa na watu wangu ( mashabiki ), hakuna kitakachonizuia kushinda". 𝐂𝐡𝐢𝐬𝐨𝐫𝐚.

𝐖𝐢𝐥𝐝𝐞

" Mimi ndiye Muhammad Ali wa kisasa".

Nani atachapika usiku wa leo, Wilder ni bondia mwenye ngumi nzito sana, akikupiga moja ikafika ( landed punch ), ni rahisi kukukalisha kwa KO, wakati Chisora ni Bondia anaependa kucheza kwa karibu ( Inside Fighter ), yani hata ukikimbia anakufuata ili akuchape. 😀

Nani anakalishwa mapema leo? Watamaliza round ngapi?

Follow us | .sports_

02/04/2026

| TFF imefuta shauri la Simba SC dhidi ya Mohamed Damaro kuhusu uhalali wa mchezaji huyo wa Yanga SC ambaye ilionekana k**a mchezaji wa kigeni na kuifanya klabu hiyo kuwa na wachezaji wengi wa kigeni.

"Shauri la Simba SC dhidi ya Damaro tumelitupilia mbali kwakua kanuni haimbani kuitumikia klabu hiyo". Sehemu ya Taarifa ya Shirikisho la soka, ilieleza.

Je, Simba SC walipaswa kwenda kuhoji mchezaji ambae alianza kucheza Singida BS k**a raia wa Tanzania?

Follow us | .sports_

31/03/2026

| Anaandika |

FT | SWEDEN 3-2 POLAND

Haya Teka la Arsenal, Viktor Gyokeres amefanikiwa kuipeleka timu yake ya Taifa ya Sweden fainali za kombe la Dunia, msumari wake dakika za mwisho wameilaza Poland ya Lewandowski.

NOTE.

Hii mechi Graham Potter ( Kocha wa Sweden ), amewafanyia umafia sana, ukiangalia matokeo pekee unaweza usiamini k**a Sweden kashinda. Very Strategic kushinda game.

1. Zieleski k**a angeshinda hii game, angefurahi sana, ameshinda mapambano mengi sana eneo la kati ( Decision, Energy ), mechi ya kiume sana.

2. Walichoamua kufanya Sweden ni kulinda goal lao lisiruhusu tena goal baada ya zile chuma mbili ( Defensive Transition & Offensive ), highline kwenye first phase yao (wasiweze kupasia vizuri ), wakishapita, rejesha nguvu nyuma kulinda.

Gyokeres ( Kwenye FIFA Qualifications )'

1. Mabao matatu ( Hat-trick ), dhidi ya Ukraine, yameipeleka Sweden fainali ya Play-offs, anaenda kufunga bao muhimu vs Poland.

2. Kwenye michezo mitato akiwa na u*i wa Swden, ameweka wavuni kamba nne na kuivusha timu yake hatua muhimu. Good guy.

NB. Teka limejipata? Linarudi EPL sasa.

31/03/2026

| DRC watacheza mechi yao ya Play-offs dhidi ya Jamaica usiku wa leo, March 31,2026 ili kujihakikishia kushiriki fainali za kombe la Dunia, mchezo ambao utafanyika majira ya saa tano usiku kwa Tanzania.

"Tunaenda kucheza mchezo wa mwisho, ni mechi ngumu sana ambayo tunapaswa kushinda, hii sio mechi ya benchi la ufundi pekee, tunatakiwa kuicheza wacongo wote".

DR Congo, unampa stake yako?

Writer |

Chanzo [ ]

31/03/2026

Its AJ to be Undisputed?

Oleksandr Usykaa alivyochora na kuhusisha bondia mwenzake, Anthony Joshua anavyoweza kuwa bingwa wa Dunia 2027.

𝐀𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐮 𝐤𝐢𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐞𝐤𝐚𝐧𝐚.

Video by Jts AJ to be Undisputed?

Oleksandr Usykaa alivyochora na kuhusisha bondia mwenzake, Anthony Joshua anavyoweza kuwa bingwa wa Dunia 2027.

𝐀𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐮 𝐤𝐢𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐞𝐤𝐚𝐧𝐚.

Video by

31/03/2026

| Bingwa wa Dunia u*ito wa juu, Oleksandr Usykaa kupitia chapisho lake la video, anaamini Bondia, Anthony Joshua atakua Bingwa wa Dunia asiekifani ( Unified Undisputed Heavyeeight World Champions ), Mwaka 2027.

Ikumbukwe, AJ amekua akifanya mazoezi kwenye kambi ya Usykaa kabla na baada ya fight yake na Jake Paul, hivyo huenda ameona ubora wa AJ na aina ya mabondia waliopo kwasasa.

Je, AJ anaweza kuwa Undisputed? Kumbuka kuna madogo k**a Daniel Dubois, Wardley hata Itauma, ambao wanakuja kwa kasi.

Writter |

Chanzo | [ ]

31/03/2026

| "Zaidi ya watu milioni 60 wa Tanzania ni either Simba SC au Yanga SC, mwanzoni nilivyoanza kutafutwa na Yanga SC niligoma kutokana na haya ( ukosoaji ), lakini baadae nilifanya maamu*i kwakua k**a unataka kukua lazima ukubali changamoto.

Sikuile licha ya kelele nilisababisha goli pia, lakini yote nimejifunza na naamini halitajirudia tena ( baada ya kelele za mashabiki kuhusu kukosa nafasi za wazi ).

Emmanuel Mwanengo - Mshambuliaji wa Yanga SC.

Writter |

Chanzo |

31/03/2026

| "Timu ilianza kusajili wachezaji wachanga, Tulijua Enzo Maresca kipi anahitaji kutoka kwetu, Kushinda Ubingwa wa Dunia ngazi ya klabu, kusberehekea pamoja na kutuma imani na kujiamini, ilikua kitu bora sana.

Kuondoka kwa kocha ambaye kwetu alitujenga ( Impact on us ), ilikua suala la Taasisi lakini kwangu nisingeweza kulikubali, ukitaka kuendeleza project ya baadae, huwezi kupambania mataji makubwa k**a EPL au Uefa, lazima usubiri".

Baadhi ya maneno ya beki wa Chelsea, Marc Cucurrela akizungumza kuhusu klabu hiyo.

Unaamini Chelsea ilikosea?

Writer |

Chanzo | |

30/03/2026

| Dauka Somba, ambaye ni Afisa Habari wa TPBCA akielezea fursa zinazopatikana wakati wa Media Day, ikiwemo kuwapatia vifaa tiba kwa Mabondia wakike wakati wa kujifungua.

30/03/2026

| Chama cha makocha wa ngumi za kulipwa nchini ( TPBCA ) kupitia kwa mwenyekiti wake, Jaffary Ndame wamezindua mradi wa siku maalum ya Taarifa ( Media Day ) ambayo itafanyika kila mwezi na itaanza rasmi April, 2026.

Malengo ya Chama hicho ni kuongeza uwezo wa makocha kwa kuwatambua kupitia usajili ambao unafanyika ili kuzalisha mabondia wenye uwezo ili kuleta ushindani Ulingoni.

Chama kimewaomba makocha ambao sio wanachama, kujiunga kuanzia sasa, ili kuleta hamasa ya mchezo kwa kuinua mabondia wenye uju*i na ushindani.

Writer |

Cc | |

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Tanga?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Tanga