Faraja yetu ni kuona tunamipatia habari za michezo za Simba sc. Furahieni na tunamitakia siku njema ikiwemo Ijumaa,jumamosi n.k
Simba sc- Chama kubwa Tz
....
🙏ELIMIKENI NASI👉.Simba sc ni bora uwanjani na nje ya uwanja ila inadorora kiubora kwa sababu mbalimbali. Kauli za wachambuzi baadhi ni za kimaono. Ni ngumu kukubalika kwa waonao kwa macho mawili pekee bila jicho la tatu hadi la nne. Ukikosoa mtu mawazo yake,uweke na akiba ya maneno. Mwenyezi Mungu ana nafasi ya ukubwa zaidi katika kuwasimamia wanadamu kikauli na matendo. Watu kuna wakati wanatamka kauli ambazo ni za kiuchawi na anamroga nazo mwenzie au anajiroga kwazo ili ipatikane faida au hasara. Ila wanaotamka hizo kauli kuna wakati wanajitambua na kuna wakati hawajitambui. Katika matamshi na matendo ya kibinadamu kuna matamshi ya kibinadamu na ya Kimwenyezi Mungu na zote zipo katika kuleta faida au madhara kutokana na lengo la mhusika au wahusika. Mfano, twalaumu marefa ila katika maamuzi yao yana uhudiano kimaana na hayo maelezo yaliyotangulia. Simba sc niseme kuwa mfumo wa kocha kiuchezaji unawaathiri kwakuwa wachezaji wanautegemea zaidi kuliko kujiongeza kiakili ili visaidiane na mfumo wa kocha. Mfumo wa kocha wa kiuchezaji kumuongoza mchezaji namna ya kucheza ila mchezaji baada ya kujifunza kucheza kupitia mfumo,anatakiwa ausaidie mfumo kwa kujiongeza kiakili. Mifumo inasomwa na wapinzani maana ni rasmi lakini akili haisomwi kirahisi maana haionekani na hubadilika kutokana na mazingira na wakati. Mfumo unategemea akili ili ufanye kazi vizuri ila akili haitegemei mfumo. Wachezaji wa simba sc hawatumii akili vizuri katika nyakati nyingi ila wanategemea mfumo wa kocha uwabebe badala ya kuibeba pia ndio maana hawafungi magoli mengi k**a awali. Neno dozi imekuwa hadithi. Kufunga goli 4 hadi 5 imekuwa stori ya zamani. Simba sc ina kikosi kizuri ila mfumo wa ligi pia unaibeba
Young African na mfumo wa ligi serikali inautawala kimaamuzi muda wowote ikitaka kwa lengo matamshi yao yawe bila kujali haki na maumivu ya wakosa haki. Najua msema kweli hapendwi ili kulijua lazima uwe na jicho la 3 hadi la 4. (Niombe radhi kwa watakao kuwazika ili nilindwe maana imehusisha serikali na ina mkono mrefu wa sheria,katika kujielezea kuna kujisahau kujilinda). Simba sc wana majaribu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila yanapitia kwa viumbe duniani. Kila mtu ajiombee na aiombee ili kuishinda vita ila Mwenyezi Mungu ana maamuzi ya juu zaidi,kuomba inasaidia ila Mwenyezi Mungu akisimama imara na usiri wa makusudio yake huamua ambalo lipo nje ya upeo wa viumbe hata k**a viumbe hawana kosa. Mwenyezi Mungu ana sifa ya kiburi kikuu ili awe juu ya viumbe na sifa chache amewarithisha viumbe. Binadamu akilipata au akilikosa ajue Mwenyezi Mungu kataka. Kujiona umepata anakupa cheo tu ili ujione bora ila yeye ndio kila kitu. Tuwe wenye kushukuru kwa neema heri au shri ila kujilinda muhimu kwa msaada wake Mwenyezi Mungu. Simba sc kiuchezaji nyote ni wazuri ila mcheze kitimu zaidi na muwe tayari kumbeba mchezaji mmoja ili muwe bora kupitia yeye. Sio lazima kila mtu atake kufunga hata k**a mazingira hayaruhusu. Mpendane. Doumbia ana madhaifu ila mkimkusudia kweli anakuwa mfungaji bora atalipenda na atamitangaza nje na ndani ya Afrika. Mfungueni hata kwa goli la penati, atoe gundu. Anajibeba ila mbebeni zaidi kwa kumsoma mikimbio na uwezo wake mumpe mipira. Uongozi una madhaifu ambayo yanaigharimu timu. Wajitathmini watumbuane ikibidi kisheria. Twataka wawe wamoja kimaamuzi. K**a kuna changamoto zitatuliwe. Muache dharau na muone usajili wa wachezaji ni jambo nyeti lengo mpate wachezaji bora na sio kutokuwapata. Kutokuwa wamoja pesa hazitoki kirahisi na kwa wingi ili kuwapata wachezaji bora. Jitahidini Simba sc wote kusambaza kauli zangu hizi ili mtwae ubingwa na mfurahie wingi wa magoli na kumfunga mtani wenu kirahisi pia. Wachezaji mnajituma na kufunga magoli kwa tabu na mazuri,hivyo muwe na staili nzuri za ushangiliaji na pia kuwe na staili moja ya ushangiliaji wa timu naamini mkiifanyia mazoezi tutaipenda. Mchezaji ashangiliwe staili yake na staili ya kitimu ifuate, hakika mashabiki tupo nyuma yenu kumisapoti. Kwa sasa mna utoto mno katika kushangilia magori. Acheni mazoea. Aina ya ushangiliaji ni hamasa ya mchezoni kufanya vizuri zaidi. Simba nguvu moja daima. Wenu Mtaalamu Ibrahimu Ruhani Mtanga (mpenda michezo na Simba sc damu). Simu : +255714503377🤲🤍🩵❤️🖤
Amani itawale siku ya leo⭐🫶🤍🩵
08/08/2026
Akiitendea haki winga namba 11 Simba sc atakuwa na uwezo zaidi wa kuwa bingwa katika michuano ya ndani na ya nje msimu huu⭐🫶🤲🤍🩵❤️🖤
Kapteni zilipendwa wa Simba sc na Kocha wa timu ya vijana ya Simba sc wakati huu 2026, John Raphael Boko, akiwakaribisha wapenzi wa Simba sc. Sikilizeni👎
U*i mpya mwekundu wa Simba sc msimu ujao. Huyo mchezaji ni Nickson Kibabage . Beki namba tatu wa Simba sc. Hongereni viongozi.
07/08/2026
Amani itawale kwa wapenda Simba sc wote🫶🤲🤍🩵❤️🖤
Click here to claim your Sponsored Listing.