03/09/2026
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema dunia inaingia katika “eneo hatarishi” la hali ya hewa kutokana na kuimarika kwa El Niño, inayotarajiwa kufikia kiwango cha juu mwishoni mwa mwaka huu. Guterres amesema ongezeko la joto la bahari na kupanda kwa joto duniani vinaashiria hatari ya kuongezeka kwa matukio ya hali mbaya ya hewa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema El Niño imeimarika na inatarajiwa kuwa na nguvu kubwa katika miezi ijayo, huku hali hiyo ikitarajiwa kuendelea hadi Februari. Shirika hilo limeonya kuwa athari zake katika mifumo ya joto na mvua zinaweza kuendelea hadi mwaka 2027.
Kwa mujibu wa WMO, kuimarika kwa El Niño kunaweza kuongeza hatari ya mafuriko, ukame na joto kali katika maeneo mbalimbali duniani. Ingawa El Niño ni hali ya asili ya tabianchi na haisababishwi na mabadiliko ya tabianchi, wataalamu wanasema inaweza kuchochea zaidi joto na matukio ya hali mbaya ya hewa katika sayari ambayo tayari inapata joto kutokana na uchomaji wa nishati za mafuta.
Guterres amesema dunia iko katika mazingira ambayo hayajawahi kushuhudiwa, akitaka mataifa kuongeza kasi ya kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda jamii dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza. Amesema ushindani uliopo sasa ni kati ya kuongezeka kwa hatari za hali ya hewa na kasi ya hatua zinazochukuliwa kuwalinda watu.
football clubs
01/09/2026
79’
Singida BS (3)- (2) Namungo FC
⚽️Benjamin Tanim 18’
⚽️Mohamed Damaro 38’
⚽️Roger’s Gabriel 50’
⚽️Sagasse Nzaou 55’
⚽️Marcel Canadi 73’
football clubs
31/08/2026
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa taarifa kuhusu kifo cha askari namba. H.1796 Koplo Mwita, aliyekuwa akishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi katika kituo cha Polisi Wilaya ya Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya leo Agosti 31, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, askari huyo alikutwa akiwa amefariki Dunia ndani ya chumba cha mahabusu katika kituo hicho mnamo tarehe 27 Agosti 2026 majira ya saa moja na dakika tatu usiku.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kabla ya kifo chake, marehemu, pamoja na Afisa mmoja na Askari watano wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali, walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai.
Kufuatia kifo cha askari huyo, uchunguzi wa kisayansi uliofanyika na ndugu zake kushuhudia ulibaini chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga ambapo mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa rai kwa baadhi ya Wananchi, baadhi ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuandaa na kusambaza taarifa zisizothibitishwa au kutoa hitimisho lisilotokana na matokeo rasmi ya kiuchunguzi, kwani kwa kufanya hivyo ni upotoshaji ambao ni kinyume cha sheria.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kuwa uchunguzi wa tukio hili unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia taratibu zote za kiuchunguzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.” imeeleza taarifa hiyo.
football clubs.
31/08/2026
BREAKING NEWS!
Mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu nchini Godlisten Malisa anadaiwa kuk**atwa Leo Namanga alipokuwa safarini kutoka Marekani.Akitoa taarifa hiyo wakili Matata ameeleza kuwa Gj amekuwa nchini Marekani kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha Tanzania k**a mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana k**a ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.
Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini k**a utaratibu unavyotaka.
Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.
Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.
Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.
Hadi sasa hakuna taarifa kamili za aliko Malisa na nini ni sababu ya kuk**atwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga".Ameeleza Dickson Matata (Wakili)
football clubs.
31/08/2026
Mudathiriiii!,dakika ya 76' Yanga wanaandika goli la 2
fountain gate 0-2 Yanga
football clubs
31/08/2026
Shalulileee!,dakika ya 25' Yanga wanaandika goli la kuongoza
Fountain gate 0-1 Yanga
football clubs
31/08/2026
Kikosi cha Young Africans Sports Club dhidi ya Fountain Gate Ligi Kuu Tanzania Bara
Azizi Ki ameanza Leo
football clubs
29/08/2026
Breaking news:Nchimbi aonekana kwenye uapisho wa Ndejembi.
Hatimae makamu wa Rais aliyejiuzulu wadhifa huo Dr. Emmanuel Nchimbi ameonekana katika hafla ya kumuapisha makamu wa Rais aliyeteuliwa karibuni bwana Deogratius Ndejembi.Ikumbukwe kumekuwepo na minong'ono mingi ya juu aliko balozi Emmanuel Nchimbi baada ya barua ya kujiuzulu aliyoitoa.
football clubs
28/08/2026
Full time //nbc pl
Yanga 2-0 Pamba fc
⚽️ Maxi 17'
⚽️ Toure 23'
football clubs
28/08/2026
Toureeee!,dakika ya 22' Yanga wanaandika goli la 2
Yanga 2-0 Pamba fc
football clubs