Ila Gen Z jamani..
Dar Digital
Karibu kwa habari za Michezo
02/06/2026
🚨Golikipa wa Senegal Assane Sarr amechaguliwa kuwa Golikipa bora wa Mashindano ya AFCON U17 2026.
➡️Kiungo wa Tanzania Issa Chole amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mshindano ya AFCON U17 2016.
🚨Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka (17) Serengeti Boys imepoteza mchezo wa fainali ya AFCON U-17 mbele ya Senegal kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-2) baada ya mchezo huo kutamatika kwa sare ya bao (1-1) ndani ya dakika 90'.
➡️Hivyo Senegal ndio Mabingwa wa Michuano hiyo ya AFCON U-17 iliyofanyika nchini Morocco huku ubingwa huo ukiwa wa pili kwa Senegal kwani mnamo mwaka 2023 walitwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza.
➡️Serengeti Boys wamemaliza nafasi ya pili huku Misri wakishika nafasi ya tatu.
NB:Hongereni Serengeti Boys kwa kulipambania taifa na kuipeperusha vyema bendera ya nchi...
Hili ni goli la Serengeti Boys..
Ila content jamani......
02/06/2026
🚨 Mshambuliaji wa Brazil, Yan Sasse ameondoka Espérance Sportive de Tunis baada ya kudumu kwa miaka mitatu yenye mafanikio.
➡️Sasse anamaliza mkataba wake na kuagana na miamba hiyo ya soka la Tunisia na Afrika, huku akiacha alama kubwa ikiwemo kutwaa mataji ya Ligi Kuu na kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
➡️Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa yupo huru kutafuta changamoto mpya baada ya kuandika ujumbe wa dhati wa kuwashukuru viongozi, mashabiki na benchi la ufundi la klabu hiyo.
✅Takwimu za winga huyo wa Kibrazil:
🏟️ Mechi - 95
⚽ Mabao - 24
👟 Assists -11
🏆 2 Tunisian League titles
🏆 2 Tunisian Cups
🏆 1 Tunisian Super Cup
Obrigado, Yan. ❤️💛
02/06/2026
🚨Klabu ya Chelsea imeweka thamani ya hadi pauni milioni 120 kwa kiungo wake nyota, Enzo Fernández.
➡️ Taarifa zinaeleza kuwa Real Madrid wanaendelea kufuatilia uwezekano wa kumsajili nyota huyo wa Argentina, huku ikielezwa kuwa wanaweza kujumuisha baadhi ya wachezaji wao katika dili hilo ili kupunguza gharama ya uhamisho.
➡️ Hata hivyo, bado hakuna mazungumzo rasmi yaliyokamilika kati ya pande hizo mbili, na Chelsea inaonekana kutokuwa tayari kumuachia Enzo kwa bei ya chini ya thamani waliyoipanga.
Via: Mail Sport.
02/06/2026
🚨Dili la kocha wa Azam Fc Florent Ibenge kuifundisha timu ya Taifa ya Mali limekufa rasmi.
➡️ Ibenge alipitishwa kwenye mchujo mkubwa lakini wameshindwa kufikia makubaliano ya pande zote mbili.
➡️ Azam Fc imeendelea na mchakato wa kuhakikisha anabaki klabu hapo.
02/06/2026
🚨Klabu ya Simba SC inatarajia kuingia kwenye mfumo mpya wa usafiri wa kifahari baada ya basi lao jipya la kisasa aina ya IRIZAR kuwasili rasmi katika Bandari ya Dar es Salaam, likiwa katika hatua za mwisho za kutolewa bandarini hapo. Pamoja na usafiri huo wa timu, gari jipya la mfanyabiashara na mdau maarufu Jayrutty ambalo atalitumia kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara za kuuza jezi rasmi za klabu nako kumewasili sambamba na basi hilo, hatua inayokwenda kuongeza chapa na hadhi ya klabu hiyo ya msimbazi kibiashara na kiutendaji.
➡️Muktadha wa kuchelewa kwa basi hilo nchini umefafanuliwa kuwa ulitokana na changamoto za kiusalama na usafirishaji wa kimataifa, kwani gari hilo lilinunuliwa miezi minne iliyopita lakini likakwama njiani kutokana na janga la vita vinavyoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Taarifa hiyo imeweka wazi kuwa muonekano wa basi hilo ndio ule ule wa uhalisia tangu liliponunuliwa kule lilipoundwa, ikipinga uvumi wowote unaoweza kusambazwa na kubeza muonekano wake, kwani gari hilo lilikaa kwenye meli kwa miezi yote hiyo minne likiwa njiani kuelekea Tanzania.
➡️Basi hilo jipya limeundwa maalum (custom-designed) kwa kufuata maelekezo na mahitaji yote mahususi ya klabu ya Simba Sports Club, kuanzia muonekano wa nje hadi mpangilio wa ndani ili kuwapa wachezaji faraja ya kiwango cha juu wanapokuwa safarini. Mashabiki na wanachama wa Simba SC wametakiwa kutulia na kuwa na subira katika kipindi hiki cha lala salama cha mchakato wa ushuru bandarini, kwani muda si mrefu chombo hicho kipya kitazinduliwa rasmi na kuanza kazi ya kubeba miamba hiyo ya msimbazi.
Kumbe ndo ukweli ......
Duh kumbe....