13/10/2026
Leo nimemsikiliza David Molinga, nyota wa zamani wa Yanga SC, na nimejifunza jambo moja: kipaji ni kitu kimoja, kupambana ni kitu kingine.
Unaweza kuwa na kipaji kikubwa, lakini ukikosa juhudi, ukaigharimu timu kwenye nyakati muhimu. Alimtolea mfano Albert Kangwanda.
Ninaamini wachezaji wengi kutoka DR Congo 🇨🇩 wana hulka ya kupambana na kuvumilia. Young Africans Sports Club imekuwa na bahati nzuri na wachezaji kutoka nchini humo.
Itapendeza kuona msimu ujao wakirejesha nguvu huko kusaka vipaji.