21/08/2023
ek
Msanii wa zamani wa Konde Music Worldwide, Killy amemlipua Harmonize.
"Kwanza kabisa usingeweza kutulipisha hata sumni kwasababu wewe ndiye uliyevunja mkataba hiyo ingekuwa vichekesho na kali ya mwaka zaidi na zaidi wewe ndio tulitakiwa tukulipishe yani utulipe, mfano tungesema twende Mahakamani alafu sheria ifatwe, bro ivi unafikiri ungechomoka, ila sisi watoto wa mjini tukasema tufunike kombe mwanaharamu apite kila mtu aendelee kufanya michongo yake"
"Alafu pia siyo Killy na Cheed tu, hakuna msanii aliyewahi kuwa hapo akarudisha pesa kwasababu hapo hakujawahi kuwa na mifumo wala misingi ya urudishwaji pesa zaidi ya wewe mwenyewe tu ndio uliyekuwa ukiingiza pesa, mlishawahi kunikatalia kufanya show ya milioni 10 na mpaka advansi milioni 5 ilishaingizwa kwenye account ya ofisi na huyo mtu nilimleta mpaka kwako masikini ya Mungu sikuwa hata na mia, mama yangu mzazi anaumwa nyumbani"
"Wadogo zangu wamerudishwa nyumbani ada hakuna nikasema na mimi nipate Rizki ila show mliikataa nakumbuka hiyo siku nilivyorudi nyumbani nililia sana sababu mpaka leo sijawahi kujiua Mungu alivyokuwa fundi sasa toka nimeanza kujitegemea mwenyewe nimeshaingiza zaidi ya milioni 40 na imetokana na muziki wangu huu huu, nimenunua gari yangu kwa pesa yangu mwenyewe mpaka nimeanza na ujenzi wa nyumba kitu ambacho sikuwahi kukitegemea kabisa kulingana na hali ilivyokuwa huko"- Killy, Msanii wa muziki Tanzania.
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
Toa maoni yako
28/01/2023
11/07/2022
14/04/2018