SOKA TZ

SOKA TZ

Share

Ukurasa Wa Habari Za Michezo Na Burudani Dhamira Ya Ukurusa Huu Ni Kutoa Habari Za Kimichezo Ndani Na Nje Ya Tanzania Ratiba Za Michezo Na Mashindano mbalimbali

30/05/2024

🌟 Join Us for the AYLF Mega Community Outreach! 🌟

We're excited to celebrate International African Child Day with a special event at Tumaini la Maisha, Muhimbili National Hospital on 16th June 2024.

Let's come together to make a positive impact on the lives of children across Tanzania. Save the date and be part of something extraordinary!

*Support our cause by donating via TIGO PESA:*
Lipa Number: 18665273
Name: AYLF TZ


Photos from SOKA TZ's post 28/04/2024

AYLF-UDSM Chapter, leo tumekutana katika Small meeting gathering ya mwisho kwa mwezi April na tulikuwa na Theme(mada) inayoitwa "RELATIONSHIPS AND RECONCILIATION". Mwl wetu wa leo alikuwa anaitwa WITNESSRUSSIA.

Alitukumbusha kuwa kiongozi mzuri ni yule anayejua na kutambua uhusiano wake yeye na MUNGU,familia na watu wengine wanao mzunguka.

Pia alitukumbusha kuyatambua maeneo muhumu katika maisha yetu yanayoitaji upatanisho kati yetu na MUNGU,familia na watu wanao tuzunguka.

Lakini aligusia njia na hatua muhimu zinazoweza kutumia kujenga uhusiano na upatanisho katika maisha yetu.

Alisisitiza jambo la muhimu zaidi kwetu sisi k**a vijana na viongozi wajao tunatakiwa kufwata na kuiga mfano na maisha ya YESU WA NAZARETH ambaye alifundsha upendo/mahusiano mazuri pamoja na kufanya upatanisho.hivyo njia pekee ya kuiponya jamii ni kujifunza KUSAMEHE. Alisema msamaha na kufanya upatanisho ndiyo itakuthibitishi kutokufanya au kulipa kisasi.

Aligusia aina mbili za msamaha
1.Unilateral forgiveness,huu ni msamaha unao toa pasina kuitaji chochote kutoka kwa yule aliyekutendea jambo.

2.Bilateral forgiveness,huu ni msamaha unaotolewa kwa kuhusisha pande mbil za watu au makundi na kwa lengo la kupata malipo au fidia.

alitufundsha njia muhimu za kuweza kusamehe kwa urahis,mduara wa kusamehe Vs kutokusamehe.

Alihitimisha kwa kutufundsha njia sahihi za kujenga urafiki wa muda mrefu ambazo ni,
1.intentionality(kuwa na watu wachache mnaoendana kifikra)
2.long term commitment
3.self-sacrifice(kujinyima)
4.trust-worthiness(ukweli na uaminifu)
5.able to forgive (kuwa tayari kusamehe)
6.take time (wape muda unao wapenda)
7.be present (uwepo wako kila wanapo kuhitaji)
8.express appreciation(eleza kushukuru kwako kwa mambo muhimu wanayokufanyia au kufanya)
9.listen(sikiliza zaidi)
10.learn to communicate

"Tumejifunza kupaa k**a ndege, tumejifunza kuogelea k**a samaki ila tumeshindwa kujifunza kitu kidogo tu. Kuishi k**a ndugu."(Martin Luther King Jr)

Godson Kitomary,
Ass Cordinator,
AYLF-UDSM Chapter,
April 28,2024.

14/04/2024

What is your identity?

Do you have posses self awareness??

Ni moja ya maswali ambayo wana AYLF-UDSM Chapter siku ya leo wameweza kuyajibu wao binafsi.

Self awareness(utambuzi binafsi) ni hali ya mtu kujifahamu yeye binafsi ni nani? na watu wanazungumzaje kuhusu yeye na je anaendana na mitazamo ya watu hao au kwenye mitazamo ya watu hao wanamchukuliaje.

Self-awareness imegawanyika katika sehemu mbili
a)internal awareness(wewe binafsi unajitazamaje?)
b)External awareness(Watu wengine wanakutazamaje?)

Namna unavyoonekana kwa watu ndiyo huonyesha furaha yako. Ukiwa na utambuzi binafsi kwa mujibu wa tafiti za kisayansi unakuwa;
1)Utafanya maamuzi mazuri.
2)Utakuwa na mahusiano mazuri na watu.
3)Utakuwa mbunifu na mzuri wa kuwasiliana na watu.
4)Utataengeneza watoto wanao jitambua.
5.Utakuwa kiongozi mzuri utakayezungukwa na wafanyakazi wazuri kupitia ule uwezo uliokuwa nao ndani yako.

Mambo yanayoonyesha kwamba hauna utambuzi binafsi;
1)Kujiamini kupita kiasi.
2)Kukosa usahihi kwenye jambo.
3)Changamoto zako binafsi kwenye maswala mbalimbali.

Nguzo saba za kujenga ufahamu mzuri na utambuzi binafsi
1.Values
2.Passion
3.Aspiration
4.Fit
5.Patterns
6.Reaction
7.Impact

Karibu AYLF-UDSM CHAPTER Main Campus,
GODSON KITOMARY,
Ass Cordinator.
April 14, 2024.

Photos from SOKA TZ's post 04/04/2024

Sehemu ya Pili....

Mwana simba,siku moja aliondoka yeye Mwenyewe na kwenda kisimani kunywa Maji na alipofika na kuanza kunywa maji aliona Picha yake kwenye maji na kugundua kuwa yupo tofauti na Kondoo aliokuwa akiishi nao. Mara ghafla akaja Simba mkubwa huku yule Mwana simba akiwa anaendelea kunywa maji akaona picha mbili ndani ya maji na alipogeuka alimwona Simba mkubwa akinywa maji na alipomaliza aliunguruma kwa nguvu jambo ambalo lilimfanya akaogopa lakini aliendelea kujishangaa mbona alifanana kila kitu na yule simba lakini yeye alikuwa na tabia k**a za wale kondoo wa mwindaji?.

Jambo lililompa Mashaka sana na akaamua kuondoka zake. Siku iliyofwata alirudi tena mtoni na alipoangalia alimwona yule Simba akitokea kwenye msitu mkubwa na akaendelea kushangaa zaidi lakini moyoni mwake aliazimia atakuwa na kufanya k**a yule Simba mkubwa na alipokunywa maji akajaribu kuunguruma na sauti ikaanza kutoka kidogokidogo k**a yule Simba. Baada ya hapo alimfwata yule simba kule msituni alipoelekea na aliona maisha ya tofauti kabisa na aliyokuwa akiishi na hii ilimfanya kuona uhalisia wake kuwa yeye ni Simba na sio Kondoo na Mwishowe aliamua kufanya maamuzi ya kubaki msituni na kuwa simba kamili na sio kondoo tena.

Niandikie ulichojifunza katika story hii.
Godson Kitomary,
(AYLF-UDSM CHAPTER ASS CORDINATOR).
04/04/2024.

Photos from SOKA TZ's post 04/04/2024

Mayles Monrue anahadithia katika Kitabu chake cha "Spirit of Leadership" hadithi aliyojifunza kutoka kwa Chifi wa kijiji kimoja Nchini Zimbabwe na Hadithi hii inamhusu Mwindaji na Mwana wa Simba(Simba Mtoto)....

Anaanza kwa kusema siku moja Mwindaji alikwenda msituni kuwinda k**a kawaida yake,katika safari yake ya kuwinda siku hiyo ilikuwa tofauti na siku zote sababu alipofika porini alikutana na Mwana simba akiwa hana uwelekeo wowote na hii ikampelekea yeye kujificha sehemu fulani ili aangalie kitakachoendelea. Baada ya kukaa kwa muda mrefu aliona hakuna simba yoyote anayekuja kumfwata huyo mwana simba,hivyo aliona huruma na kuamua kumchukua mwanasimba huyo mdogo na kwenda naye nyumbani amfuge katikakati ya Kundi lake la Kondoo.

Miaka ileanda na Mwana simba akakua katikati ya kundi la Kondoo na akiwa ameiga na kuwa na tabia zote alizonazo Kondoo. Alimfuga na kwenda naye malishoni k**a ilivyokuwa Kondoo zake na baadae aliwapeleka Mtoni kunywa Maji. Walienda mara kwa mara na siku moja walipofika mtoni waliona simba mmoja Mkubwa akija na Kondoo wote walikimbia na hata yule Mwana wa Simba kwakuwa alishakuwa na tabia za Kondoo alikimbia pia.....

Itaendelea Post ya Pili.

19/02/2024
29/01/2024

Season shift

13/01/2024

Ujana ni bongo na siha njema,ili kukamilisha kile tulichoitiwa duniani haina budi kuhakikisha kuwa yale maarifa tuliyoyapata yanatumika kwa manufaa ya jamii yote. Mwaka 1970 wakati mwalimu Nyerere anakipandisha hadhi chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM) kutoka kuwa College campus ya Makerere alisema hivi "Wale wapatao upendeleo huu wa kipekee wanao wajibu mkubwa wa kulipa fadhila maaana ni k**a kijiji kilichokuwa na njaa kilichouza chakula chote na kumpa mmoja ale ashibe aendee akalete chakula kingi zaidi,hivyo Vijana wakike na wakiume waliopewa elimu na jamhuri hii na wakashindwa kuitumia kwa manufaa ya jamii basi watakuwa wasaliti wa Jamhuri yao wenyewe".

02/01/2024

𝐂𝐇𝐈𝐍𝐔𝐀 𝐀𝐂𝐇𝐄𝐁𝐄 𝐀𝐌𝐄𝐀𝐍𝐃𝐈𝐊𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐑𝐈𝐖𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀𝐊𝐄 𝐘𝐀 "𝐓𝐇𝐈𝐍𝐆𝐒 𝐅𝐀𝐋𝐋 𝐀𝐏𝐀𝐑𝐓" 𝐊𝐖𝐀𝐌𝐁𝐀.
𝐌𝐭𝐮 𝐚𝐧𝐚𝐲𝐞𝐰𝐚𝐚𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐉𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐳𝐚𝐤𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐬𝐡𝐞𝐫𝐞𝐡𝐞 𝐡𝐚𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢 𝐡𝐢𝐯𝐲𝐨 𝐤𝐰𝐚 𝐚𝐣𝐢𝐥𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚𝐨𝐤𝐨𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐲𝐚 𝐧𝐣𝐚𝐚. 𝐖𝐚𝐚𝐥𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐰𝐨𝐭𝐞 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐯𝐲𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐦𝐚𝐣𝐮𝐦𝐛𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐰𝐚𝐨.
𝐓𝐮𝐧𝐚𝐩𝐨𝐤𝐮𝐬𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐚 𝐮𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐰𝐚 𝐦𝐛𝐚𝐥𝐚𝐦𝐰𝐞𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐚𝐫𝐝𝐡𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐣𝐢𝐣𝐢 𝐜𝐡𝐞𝐭𝐮, 𝐬𝐢𝐲𝐨 𝐤𝐰𝐚 𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐲𝐚 𝐌𝐛𝐚𝐥𝐚𝐦𝐰𝐞𝐳𝐢.
𝐊𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐚𝐧𝐠𝐞𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐢𝐨𝐧𝐚 𝐦𝐛𝐚𝐥𝐚𝐦𝐰𝐞𝐳𝐢 𝐚𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐲𝐮𝐦𝐛𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐰𝐚𝐤𝐞.
𝐓𝐮𝐧𝐚𝐤𝐮𝐬𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐧𝐢 𝐣𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐳𝐮𝐫𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐉𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐤𝐮𝐤𝐮𝐬𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐚 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚.

𝐊𝐰𝐚 𝐡𝐢𝐲𝐨 𝐭𝐮𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐞 𝐧𝐚 𝐮𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐰𝐞𝐭𝐮 𝐢𝐥𝐢 𝐭𝐮𝐟𝐮𝐫𝐚𝐡𝐢𝐞 𝐧𝐠𝐮𝐯𝐮 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚.
𝐓𝐮𝐤𝐢𝐭𝐚𝐛𝐚𝐬𝐚𝐦𝐮 𝐡𝐚𝐢𝐦𝐚𝐚𝐧𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐢𝐬𝐢𝐩𝐨𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐧𝐠𝐮𝐯𝐮 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐲𝐚𝐬𝐡𝐢𝐧𝐝𝐚 𝐦𝐚𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨.

𝐏𝐞𝐤𝐞 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐮𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐚𝐛𝐚𝐬𝐚𝐦𝐮 𝐥𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐦𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐦𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐞𝐤𝐚.
𝐔𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐩𝐞𝐤𝐞 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐮𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐟𝐮𝐫𝐚𝐡𝐢 𝐥𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐦𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐦𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐡𝐞𝐫𝐞𝐡𝐞𝐤𝐞𝐚.
𝐔𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐩𝐞𝐤𝐞 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐮𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐚𝐦𝐤𝐚 𝐥𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐦𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐦𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐨𝐧𝐠𝐞𝐚.

𝐓𝐮𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐳𝐞 𝐦𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐲𝐚𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐮𝐮𝐧𝐠𝐚𝐧𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐦𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐲𝐚𝐭𝐚𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐞𝐧𝐠𝐚𝐧𝐚🙏🏽.

Nikutakie 2024 yenye kheri na fanaka tele!!

11/11/2023

Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi kusema "Taifa lolote litakalowasahau vijana lihesabu maumivu".

Vijana Ndiyo nguvu kazi ya Taifa na katika Afrika asilimia 75 ni Vijana.Hata maandiko matakatifu yanasema "nimewaandikieni Ninyi vijana kwakua mnazo nguvu za kumshinda yule muovu".Lengo Letu kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na Kizazi Cha vijana watakaorejea katika misingi ya maadili na uadilifu Ili tupate tena Viongozi shupavu k**a Mwalimu,Kwame Nkrumah,Nelson Mandela na Thomas Sankara wengine.

Tunahitaji kupata vijanawatakao Kuwa na uchungu na Taifa lao,wenye suluhisho la matatizo na migogoro katika jamii,wenye kuwajibika na pia wana hofu ya Mungu ndani Yao.Tunatazamia wakombozi wa bara hili watakuwa vijana wenye maarifa na tabia za kiungu.

VIVA AFRICA!

Photos from SOKA TZ's post 03/10/2022
03/10/2022

RATIBA YA LEO JUMATATU YA OCTOBER 03

NBCPL- 16:00 Coatal Union Vs Kagera Sugar

NBCPL- 18:15 Ruvu Shooting Vs. Yanga SC

NBCPL - 20:15 Azam FC Vs. Singida Big Stars

SERIE A - 21:45 Hellas Verona Vs. Udinese

EPL - 22:00 Leicester City Vs. Nottingham Forest

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Greater Manchester?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Mlapakolo
Greater Manchester