Pepeto Michezoni

Pepeto Michezoni

Share

Habari Motomoto za michezo,Gumzo na Dadisi michezoni ,Mashinani Kitaifa na hata Kimataifa.

22/02/2019

Chelsea imepigwa marufuku na FIFA kutosajili wachezaji kwa madirisha mawili yajayo ya uhamisho hii ni baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria na kanuni za kuwasajili wachezaji makinda.
Pia kilabu hiyo imepigwa rungu la faini ya pauni 460,000, nacho chama cha soka nchini Uingerezwa hakijaachwa salama kwani wamepigwa faini ya £390,000.
Kichocheo kikubwa kwa makosa haya nikutokana na jinsi walivyomsajili Bertrand Traore mwaka 2013.
Chelsea wana siku 90 kujitakasa kutoka kwa marufuku hiyo.
Picha kwa hisani.

17/02/2019

Mshambulizi wa Bandari Wyclife Ochomo anaendelea vizuri baada ya upasuaji wa eneo la kisukusuku (elbow) kufanyika kwa uzuri.
Ochomo alipata jeraha hilo kwenye ushindi mhimu wa Bandari dhidi ya Kariobangi sharks.
.

17/02/2019

Manchester United wanataka kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kupeleka ombi la pauni milioni 262 kwa PSG wakimtaka Neymar Jr huku ikiaminika kaimu mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer atachochea usajili huo endapo atateuliwa mkufunzi wa kudumu kilabuni hapo.

Photos from Pepeto Michezoni's post 23/12/2018

Kilabu ya Birikani Fc ya wadi ya Mwavumbo ndio mabingwa wa kipute cha Tayari super cup kwenye wadi hio hii ni baada ya kuicharaza Mwavumbo Fc kwa mabao 3-2 na imejishindia jezi pamoja na pesa taslimu.
Sasa Birikani itaiwakilisha wadi ya Mwavumbo kwenye fainali itakayofanyika Kinango ambako watapambana na wadi nyengine sita kutoka eneo bunge la Kinango.
Ligi inadhaminiwa na mbunge wa Kinango Benjamin Dalu Tayari.

Photos from Pepeto Michezoni's post 17/12/2018

Lions Fc ndio mabingwa wa kipute cha tayari super cup wadi ya Samburu Chengoni hii ni baada ya kuitandika Ghaibu Fc mabao 2-1.
Mshindi alijishindia jezi, mipira pamoja na pesa taslimu.
Tayari super cup ni ligi inayochezwa kwa lengo lakuunda timu ya Kinango na inachezwa katika wadi zote saba za eneo bunge la Kinango na inadhaminiwa na mheshimiwa
Benjamin Dalu Tayari mbunge wa Kinango.

23/11/2018

Tusker imekamilisha usajili wa kipa Emery Mvuyekure kutoka AS Kigali ya Rwanda na anachukua nafasi ya Patrick Matasi aliyejiunga na St. George ya Ethiopia.
Picha kwa hisani.

23/11/2018

Kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante amemwaga wino wa mkataba mpya wa miaka mitano kilabuni hapo na kuwapotezea Manchester United waliokua wakimtaka kwa sana.
Picha kwa hisani.

23/11/2018

Kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 11 Cristiano Ronaldo na Lionel Messi utawala wao wa tuzo za Ballon d’Or wafika kikomo baada ya jarida la Tuttosport kumwaga mtama kuwa hawako kwenye listi ya wagombea watatu bora wa tuzo hio mwaka huu.
Jarida hilo limewataja Luka Modric, Kylian Mbappe na Raphael Varane kuwa kwenye listi ya mwisho huku Modric akipewa nafasi kubwa yakushinda tuzo hio.
Picha kwa hisani.

14/11/2018

Timu ya taifa ya Harambee Stars ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 23 wataikaribisha timu ya taifa ya Mauritius katika uwanja wa kasaranii hii leo, kwenye mechi za mchujo wa kufuzu kwa mataifa ya Afrika yatakayoshiriki michezo ya Olympic huko Tokyo Japani mwaka 2020.

13/11/2018

Raia wa wingereza Daniel Sturridge anayechezea klabu ya Liverpool ameshtakiwa na Chama cha Soka wingereza FA kwa makosa ya ukiukwaji wa sheria za Ubashiri katika michezo
Inadaiwa kwamba alitoa habari zinazohusiana na mechi kwa ajili ya kusaidia ubashiri wa mechi kwa wawekezaji kwenye mitandao ya bet. Madai ambayo yamepingwa vikali na usimamizi wa klabu ya Liverpool.

13/11/2018

Kundi la mawakili wanaowakilisha shirikisho la kandanda humu nchini FKF lilielekea mjini Zurich Switzerland kuwasilisha kesi ya kulish*traki shirikisho la kandanda barani afrika CAF kwa kulirudisha taifa la Equatorial Guinea kushiriki dimba la soka la ubingwa wa taifa bora africa kwa upande wa kina dada (AWCON).

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mombasa?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Mombasa
80100