Michezo Online News

Michezo Online News

Share

Timely updates on Sports News and events happening in Kenya and world at large

Photos from Michezo Online News's post 05/06/2026



Andoni Iraola ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa Liverpool FC.

Kocha huyo wa zamani wa AFC Bournemouth amesaini mkataba wa miaka miwili katika uwanja wa Anfield.

Photos from Michezo Online News's post 28/05/2026



Crystal Palace wameibuka kidedea na kulishinda Kombe la Mashirikisho (Conference) la UEFA.

Bao la pekee lake Jean Philippe Mateta ndilo lilishindia Palace ushindi huo muhimu

Photos from Michezo Online News's post 24/05/2026



Baada ya raundi 38, hatimaye Ligi Kuu Uingereza, EPL msimu wa 2025/26 imefika tamati hii leo.

Arsenal ndio wametawazwa mabingwa msimu huu huku nao Westham, Burnley na Wolves wakishuka daraja.

Arsenal walimaliza msimu alama saba, mbele ya nambari mbili Man City.

19/05/2026



Sasa ni rasmi! Baada ya kusubiri kwa miaka 22, Arsenal wameibuka mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza, EPL msimu 2025/26.

Hii ni baada ya nambari mbili Man City kutoka sare ya 1-1 na Bournemouth mapema leo.

18/05/2026

Arsenal wamesogea karibu kutwaa Kombe la EPL baada ya kuwatandika Burnley kwa bao 1-0 ugani Emirates.

Iwapo Man City watatoka sare au kushindwa na Bournemouth baadaye leo usiku, Arsenal watakuwa mabingwa wa msimu 2025/26.

Photos from Michezo Online News's post 17/05/2026



Haya ndio matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa hii leo.

17/05/2026



Chelsea wamemteua na kumtangaza rasmi Xabi Alonso kuwa Meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne.

Mhispania huyo ataanza rasmi majukumu yake ugani Stamford Bridge mnamo tarehe 1 Julai 2026.

16/05/2026



Manchester City ndio mabingwa rasmi wa Kombe la FA msimu huu baada kuwatandika Chelsea kwa bao moja sufuri ugani Wembley.

Hili ni kombe la pili City wametia kibindoni baada ya kushinda Kombe la Carabao mapema.

15/05/2026



Aston Villa wamewapepeta Liverpool kwa mabao 4-2 ugani Villa Park.

Kufuatia ushindi huo, Villa wamejikatia tiketi ya moja kwa moja kucheza katika mechi za Klabu Bingwa Ulaya, UCL msimu ujao.

Hii ilikuwa mechi ya raundi ya 37/38 ya EPL.

Photos from Michezo Online News's post 10/05/2026



Arsenal wamefungua mwanya juu ya jedwali la EPL hadi alama tano baada ya kuwafinya Westham United kwa bao 1-0 ugani London Stadium.

Arsenal sasa inahitaji kushinda mechi mbili zilizosalia ili kutawazwa mabingwa wa EPL msimu 2025/26.

Kwingineko, mechi zingine zilizochezwa hii leo za EPL, zilitamatika kwa sare ya kufungana.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Nairobi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Nairobi
00100