William Benedicto

William Benedicto

Share

W***y tactics

09/04/2026

Madrid vs Bayern analysis (1st leg)

Tuanze na idea ya Bayern kwenye ujenzi wa mashambulizi (build up) kutokea chini. Bayern wamekuwa wanawasogeza juu baadhi ya wachezaji (full backs) ambao wataenda kucheza kwenye maeneo ambayo yatampa maswali magumu mpinzani wake.

Mfano: Stanisic na Laimer wanasogea juu kwenye half spaces halafu Olise na Diaz wanatanua mapana ya uwanja. Bayern walikuwa wanafaidika vipi na muundo huu wa kusogeza walinzi wake wote wawili juu?

Kwakuwa Madrid kipindi cha kwanza walikuwa wanazuia na 4-4-2 ilikuwa na madhaifu kwa Mbape na Vin ambae kazi yao ilikuwa kusubiri mipira ya counter na kushindwa kuisaidia Madrid OOP. Turudi kwenye mada

Laimer na Stanisic wakisogea juu inawafanya Valverde na Guler wafuate mikimbio ya hao wachezaji wa Bayern, kwakuwa Laimer na Stanisic walikuwa wanaingia ndani maana yake Diaz na Olise wanaachwa kwenye situation za 1v1 dhidi ya Trent na Carreras.

Na hapo ndio tatizo kubwa lilikuwa linaanzia kwa upande wa Madrid hata ukiangalia upande wa Olise alikuwa anapita sana sababu ya 1v1 dhidi ya Carreras ambae hakuwa na game nzuri dhidi ya Bayern.

Nini walifanya Madrid kuzuia uhatari huu?

Madrid waliona njia salama ni kurudi kwenye low block ya 4-4-2 kuwaacha Vin na Mbape juu hawafu wachezaji wengine nane wazuie kwa ukaribu sana na kufunga nafasi yoyote ile katikati ya mstari. Hii ilisaidia kwa kiasi chake maana wachezaji k**a Olise na Diaz wanahitaji sana soace ili wakufunge.

Hapa wakawaacha Bayern wazunguke na mpira juu ya combact block yao ambayo waliweka huku wakisubiri nyakati za kufanya counter attacks. Kuna walikuwa wanafanikiwa kuishinda rest defense ya Bayern Munich. How?

Rest defense ya Bayern ilikuwa 2+1 (Upamecano na Tah halafu juu yao anakuwepo Kimmich) Kimmich kazi yake ilikuwa ni kuvunja aina yoyote ya pasi ambayo itatupwa kwa Mbape na Vin, k**a ikitokea akawa nyuma ya mchezo maana yake hakuna mchezaji wa kuwaokoa dhidi ya Vin na Mbape.

Mbape na Vin waliona kuna ugumu kupitia katikati mwa kiwanja maana Kimmich angekuwa rahisi kwenda kuziba mapengo ya Tah au Upamecano, sasa wao wakaamua kwenda wide ili hata Kimmich akienda kuziba nafasi speed yake ni ndogo kulinganisha na Mbape au Vin.

Licha ya hayo yote ila Vincent alikuja na moja kati ya muundo bora sana wa kufanya counter pressing.

Hii aina ya pressing hawakuwa wanafanya tu sehemu moja ila kila mchezajikwenye kila eneo alikuwa anaenda kupress pale anapopoteza mpira. Najua ni hatari sana ila risk ambayo alichukua ndio imewafanya kuwa hapa walipo.

Kuanzia namna ambavyo Madrid walipokuwa wafanya build up Kimmich unamuona amesogea juu kabisa lengo likiwa ni kuweka presha ila kuna muda kutoka kwa Kimmich kwenye kungo kulileta shida kwa Pavlovic ambae alikuwa anabaki k**a single 6 dhidi ya wachezaji wawili wa Madrid.

Bado tena unawaona Madrid ili kuua kabisa uchezaji wa Bayern ule wa wachezaji kuzunguka uwanja mzima walikuwa wanashuka hadi kwenye muundo wa 5-3-2 ili Valverde amsaide Trent kuzuia. Mambo yalikuwa mengi ila acha tusubiri tuone second leg.

06/04/2026

CHOBWEDO โžก๏ธ YANGA deal done โœ…๏ธ

Baadhi ya vyanzo vinaripoti kwamba mchezaji Raia wa Tanzania Ramadhani Chobwedo amekamilisha uhamisho wake akitokea TRA yenye makazi yake Mkoani Arusha kuelekea Yanga.

Nani atoke Chobwedo aingie? ๐Ÿ˜€

Photos from William Benedicto's post 03/04/2026

Nipo nawaza hapa labda tusaidiane mawazo kidogo.

Kilichopungua Yanga ni risk kwenye nyakati muhimu uwanjani kuanzia wakiwa wanashambulia, wanajilinda na kujenga mashambulizi.

Picha hizi hapa chini nimejaribu kuwaza suluhisho la matatizo yao.

A. PRESSING HIGH (kuzuia shambulizi kuanzia juu ya uwanja)

B. BUILD UP PHASE (ujenzi wa shambulizi 3-1)

C. ROTATIONAL PLAY (kubadilishana nafasi kwa wachezaji)

Nikisema nianze kuelezea moja moja nadhani hatutomaliza ila picha hizo zinajieleza kwani nimezipanga kulingana na hicho ambacho nimeandika. Wewe unawazaje?

Photos from William Benedicto's post 02/04/2026

OURA MAGICIAN

Hii ni mechi ya Simba dhidi ya Coastal Union na hili ni goli la Mwalimu ambae alipokea pasi kutoka kwa Chama.

Moja kati ya madhaifu ya hizi timu za madaraja ya kati ni k**a wakiamua kwenda aggressive na kufanya highline (kuzuia kuanzia juu) k**a ambavyo wamefanya kwenye hii picha, lazima kuwepo n space eneo au kuna mmoja ambae atamfanya mpinzani kuwa free k**a ambavyo imetokea hapa.

Nadhani idea yao ilikuwa nzuri ila kutimiza idea ndio shida ilipoanzia, Chama kushuka chini ilimfanya Kibabage kudumisha rest defense. Na kitendo hiki kinasababisha overload upande wao mmoja zaidi ya wachezaji wanne wa Simba upande huo Kibabage, Chama, Rushine, Oura, .

Kwakuwa Coastal walikuwa tayari wameshaamua kusogea juu hakukuwa na namna ya kurudi chini, ukiwaangalia wachezaji wa Coastal walikuwa idadi sawa na Simba ila sehemu moja ambapo nadhani walikosea Coastal ni kumuacha mchezaji mmoja free ambae ndio kwangu naweza kusema alikuwa key player kwa Simba (OURA)

Anapokea mpira wakati anafanya zile touch maana yake anampa muda Chama wa kusogea tena juu, mfano k**a Oura angepokea mpira na kuutupa kwa Chama Je Chama angepata ile nafasi ambayo amepata? Jibu ni hapana so hapa ndio pale unasimama na kumpigia makofi OURA ambacho amekifanya.

Baada ya hapo ilikuwa ni nani ataenda kumalizia pasi kali ya Chama na eneo hilo alikuwepo Gomez Mwalimu akatulia na kumuandikia mnyama goli.

Je wangefanyaje kwenye moment k**a hii?

Chama baada ya kumuwin mchezaji wa kwanza wa Coastal wale wawili ambao walianza kwenda kupress wangerudi nyuma ili kumuacha Chama apate muda sana na mpira bila madhara ili wao warudi kwenye muundo mzuri kwa kuwa na idadi nzuri ya kuzuia.

Mawazo yako ni yapi kwa Coastal Union?

31/03/2026

Je ni sahihi Cherki kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Ufaransa?

Nani ampishe Cherki ๐Ÿ˜€

31/03/2026

Simba wamefanyaje kuwafunga TRA goli la tatu?

20/03/2026

Msimu huu ni mgumu sana ila tunaamini top ni yetu. GGM

Photos from William Benedicto's post 20/03/2026

Swali. Je tutegemee Simba ambayo itapiga sana cross licha ya kutoanza na mshambuliaji?

Nimeweka picha mbili hapo chini, Picha ya mchezo wa Madrid vs Man City na Simba vs Pamba. Kwa haraka bila kusoma maelezo nadhani umeshaelewa ni nini natamani kuzungumza hapa.

Ukiangalia nafasi ambayo alikuwepo Vin wakati Tchouamen anatoa cross kutokea upande wao wa kulia ni same idea ambayo mchezaji wa Pamba alikaa wakati anasubiri cross kutoka upande wao wa kulia.

Ni eneo ambalo huwa limejaa tricks nyingi sana maana mara kadhaa walinzi huwa wanafocus zaidi na sehemu ambapo mpira upo kuliko wachezaji ambao wanakimbia nyuma ya migongo yao.

Ila pia ni eneo ambalo sio kila mchezaji (mshambuliaji) anaweza kugundua na kwenda katikati ya walinzi wawili. Maana ukimuangalia Rushine ni k**a anaamini kwamba yeye ndio wa mwisho ila kumbe Toure yupo nyuma yake.

Ni nafasi ambayo kipa wa Simba aliweza kusave ila isingekuwa uhodari wa kipa huenda tungeamka na mjadala mwingine leo.

Mwisho kabisa naomba nisikie maoni yako, Simba ilianza kucheza bila mshambuliaji kiongozi na sio mara ya kwanza wala ya pili, Ila nadhani kwenye mechi za wiki hii imekuwa timu namba moja kwa kupiga cross nyingi ndani ya box la mpinzani wao.

Swali. Je tutegemee Simba ambayo itapiga sana cross licha ya kutoanza na mshambuliaji?

Photos from William Benedicto's post 17/03/2026

Nimejaribu kwa uchache tuu kukuonesha namna hizi timu (PSG vs CHELSEA) zilikuwa na aina moja ya uchezaji hasa pembeni mwa kiwanja na k**a wote waliamua kutumua risk methood kushambulia.

Photos from William Benedicto's post 11/03/2026

Uchambuzi na W***y Tactics ๐Ÿงต

Bayern Munich walikuwa wageni wa Atalanta mchezo ambao ulimalizika kwa Bayern kushinda magoli 6 kwa moja na Olise kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.

Ila kiufundi nadhani Bayern walifanya zaidi ya tulivyowazoea, Atalanta walikuja na man to man pressing tena walikuwa very aggrresive so solution kwa Bayern ilikuwa ni total rotational play (wachezaji kuuzunguka uwanja mzima bila kujali nafasi na namba unayo cheza)

Jukumu la kujenga mashambulizi halikuwa la Upamecano na Tah tu k**a ambavyo tumezoea ila wachezaji k**a Gnabbry, Jackson, Palv na Kimich walikuwa wanashuka chini kupandisha shambulizi,hata Upamecano akapewa uhuru wa kupokea mpira nyuma ya mstari wa kiungo wa Atalanta.

Pia Tah akapewa uhuru wa kupiga cross akitokea pembeni k**a winga au mlinzi wa pembeni, ila Stanisic alipewa uhuru wa kuuweka mpira ndani ya nyavu k**a mshambuliaji. Nadhani huu ndio msimu bora zaidi kwa Bayern Munich chini ya kocha Vincent Komapony.

10/03/2026

Makosa ya Polisi Tanzania dhidi ya Yanga.

07/03/2026

Mashabiki wa Barcelona soogeeni hapa kidogo tuzungumze hii detail ndogo kwenye hii mechi ya Barcelona vs Atletico.

Balde yupo na mpira alioupokea kutoka kwa Gerald Martin ila hakuna sehemu ya kupeleka mpira sababu Atletico wapo watatu (Lloente x Simeone x Koke)

Najaribu kujiuliza wangefanya hivi ingekuwa rahisi kuwawin hasa upande huu wa kushoto wa Barcelona na kulia kwa Atletico.

Gerald alipo ni mbali k**a angesogea karibu maana yake angemlazimisha Griezman kusogea ili kuweka presha kwa Gerlad na kufanya hivyo atamuacha Pedri kuwa huru nyuma yake na kufanya mikimbio kwenda karibu na goli.

Halafu Lloente na Coke wangekuwa eneo hilo hilo ili kutomruhusu Raphina kuleta madhara sasa kufanya hiyo movement tayari Balde anaweza kupokea mpira nyuma ya Simeone na kuangalia kati ya Torres ambae atakuwa ndani ya box au Pedri ambae atakuwa njee nani atampa mpira.

Vipi wewe ukiangalia picha hii unawazaje?

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Arusha