Swahili MEDIA

Swahili MEDIA

Share

🔴 HABARI, MATUKIO NA MICHEZO
🟢 MAWASILIANO PIGA:0713114698
🔵

03/09/2026

Arusha Septemba 3 2026 Hali ya taharuki imeibuka majira ya mchana katika maeneo ya Viwandani Kata ya Themi jijini Arusha baada ya gari kuwagonga watoto wawili waliokuwa wakitoka shuleni

Inaelezwa kuwa watoto hao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Olorien ambapo mtoto mmoja amefariki dunia papo hapo katika eneo la tukio

Mtoto wa pili ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo alifariki dunia akiwa anapelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu

Baada ya ajali hiyo wananchi wenye hasira kali waliichoma moto gari hilo lililohusika katika ajali hiyo na kuteketea kabisa

Inaelezwa kuwa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo alikimbia eneo la tukio baada ya ajali hiyo ili kuepuka hasira za wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo

Tukio hilo limesababisha taharuki katika eneo hilo huku vyombo vya ulinzi na usalama vikifika na kuanza kufuatilia tukio hilo

03/09/2026

Mtoto mwenye ulemavu, anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano na ambaye hadi sasa hajatambulika, amekutwa akiwa ametelekezwa katika kichaka kilichopo Mtaa wa Negamsi, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.

Mtoto huyo ameokolewa leo, Septemba 2, 2026, na wasamaria wema waliomkuta akiwa katika mazingira hayo na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Hadija Muhango, amesema mtoto huyo atafanyiwa uchunguzi wa afya ili kubaini hali yake kiafya huku taratibu za kumtafuta mzazi, mlezi au ndugu wa mtoto huyo zikiendelea,

02/09/2026

KWA HASIRA LISSU AHOJI "WAKINA NANI WANASEMA HECHE ANANIZUIA KUTOKA GEREZANI

02/09/2026
02/09/2026

Zoezi ya kushinda kuandika dotto magari na chid benz

02/09/2026

Wasanii wote walioitwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Patrobas Katambi wameitikia wito isipokuwa Dudubaya, Niffer na Anko T ambao hawajafika mpaka sasa!

02/09/2026
02/09/2026

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dkt. Lameck Karanga, leo Septemba 1, 2026, amejionea zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa wananchi wa Kijiji cha Qaru, Tarafa ya Endabash, Wilaya ya Karatu.

Akiwa katika kituo cha uandikishaji, Mhe. Dkt. Karanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na uongozi wa NIDA kwa kuwezesha watumishi kuwafikia wananchi vijijini na kutoa huduma hiyo bila malipo.

Aidha, Mhe. Dkt. Karanga amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia nyaraka halali na sahihi wakati wa kuwasilisha taarifa zao, hatua ambayo itasaidia kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza katika usajili na utoaji wa vitambulisho pamoja na namba za NIDA.

Zoezi hilo limefanyika katika Kijiji cha Qaru kwa takribani siku mbili, huku leo, Septemba 1, likiwa siku ya hitimisho.

Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Qaru, timu ya NIDA inatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika maeneo mengine yenye changamoto, hususan kuwafikia wananchi ambao bado hawana namba au Vitambulisho vya Taifa.

01/09/2026

Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Loreto, Stellah Shilingi (15) amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka juu ya ghorofa ya kwanza hadi chini katika Mtaa wa Majengo Mapya, Kata ya Nyakato, Wilaya ya Ilemela.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa iliyotolewa leo Jumanne, Septemba Mosi, 2026 imesema tukio hilo lilitokea Agosti 31, 2026 saa 11:00 asubuhi, wakati mwanafunzi huyo akiwa na wanafunzi wenzake wakielekea kufanya usafi shuleni hapo.

Mutafungwa amesema baada ya kujirusha, mwanafunzi huyo alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na kuchukuliwa haraka kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kwa ajili ya matibabu, lakini baada ya kufikishwa hospitalini hapo ilibainika kuwa tayari amefariki dunia.

"Baada ya tukio hilo, alipata msaada wa haraka kwa kuchukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kwa ajili ya matibabu, lakini baada ya kufikishwa hospitalini hapo ilibainika kuwa tayari amesha fariki dunia," amesema Mutafungwa.

01/09/2026

Mwili wa kijana wa kiume ambaye hadi sasa utambulisho wake haujafahamika umeokotwa katika eneo la Daraja lililopo kwenye barabara ya Mbuyu wa Mjerumani-Mbulu, Kijiji cha Kazaroho, Kata ya Kisangaji, Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Mwili huo umeokotwa ukiwa katika eneo hilo, huku wananchi wakieleza kushtushwa na tukio hilo ambalo limeibua maswali kuhusu mazingira yaliyopelekea kijana huyo kufariki na mwili wake kutupwa katika eneo hilo.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi limechukua mwili huo na kuuhifadhi kwa ajili ya uchunguzi, wakati jitihada zikiendelea kubaini utambulisho wa marehemu pamoja na chanzo na mazingira ya kifo chake.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, amefika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini utambulisho wa kijana huyo na sababu za kifo chake.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Arusha