Brotherhood Fitness Club

Brotherhood Fitness Club

Share

We are located at Jacaranda street near Uhuru primary school.

11/06/2022

11/12/2020


・・・
JE UNAFANYA SANA MAZOEZI YA TUMBO LAKINI KITAMBI HAKIONDOKI? JIFUNZE SABABU HAPA.

# Sehemu ya kwanza #

Kuna mazoezi yanajulikana kwa jina maarufu k**a “mazoezi ya tumbo” na watu wengi hukazana sana kuyafanya kwa matumaini kwamba wataondoa kitambi ama kutengeneza “six-pack”.
Watu wengi hujisikia kukata tamaa wanapoona wamefanya mazoezi haya kwa miezi kadhaa lakini kitambi hakiondoki na six-packs hazitokezi!

Ukweli wa mambo
Kila mtu ana six-packs! K**a unavyoona pichani, kuna msuli mkubwa unaofunika tumbo kwa mbele unaoitwa “rectus abdominis” na kila mtu ana msuli huo. Kuna tishu zinazopita kati ya msuli huo na kuufanya utengeneze packs. Juu ya msuli huo kuna mafuta yaliyohifadhiwa na mwili k**a unavyoona kwenye picha ya kushoto kwako. Misuli hii inaweza kuonekana kwa nje kirahisi endapo mtu ana mafuta kidogo mwilini. Kikawaida kwa watu wengi zinaonekana six-packs lakini wapo baadhi ambao zinaweza kuonekana eight-packs mpaka ten-packs.

Ukweli ni kwamba hakuna mazoezi ya tumbo yatakayoondoa mafuta hayo! Pengine watu huhisi kwamba mazoezi haya yatachoma mafuta ya tumbo kwa sababu husikia hali ya kuungua/kuumia sana wanapofanya mazoezi haya. Mazoezi haya yanasaidia sana kufanya eneo lako la tumbo na mgongo kuwa imara na misuli yako kuwa mikubwa zaidi lakini haitaonekana kwa nje k**a bado kuna rundo la mafuta yaliyoifunika.

Mafuta hayo yataondokaje?
Mwili utatumia mafuta endapo utakuwa na mahitaji makubwa ya nishati kuliko nishati uliyoipata kupitia chakula ulichokula! Hii inaitwa “caloric deficit” ikitokea hali hii mwili utalazimika kutumia hifadhi ya nishati zake ambazo ni mafuta! Hiki ndicho kitafanya mwili wako upungue! Hivyo KITAKACHOFANYA SIX-PACKS ZIONEKANE SIO MAZOEZI BALI NAMNA UNAVYOKULA!

post inayofuata kwa sehemu ya pili #

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Brotherhood Fitness Club, Jacaranda Street
Arusha

Opening Hours

Monday 06:00 - 21:00
Tuesday 06:00 - 21:00
Wednesday 06:00 - 21:00
Thursday 06:00 - 21:00
Friday 06:00 - 21:00
Saturday 06:00 - 21:00
Sunday 10:00 - 18:00