17/11/2022
FRANCK RIBERY KUREJEA TENA FC BAYERN MUNICH
✅Nyota wa zamani wa Bayern Munich na Ufaransa, Frank Ribéry anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo ya Bundesliga chini ya jukumu jipya.
✅Ribery (39) anatarajiwa kuwa balozi wa klabu, mazungumzo ya awali tayari yamefanyika kati ya pande zote mbili na yanaendelea vizuri.
✅Ribéry atachukua majukumu ya uwakilishi (Balozi) wa Bayern katika siku zijazo, si mchezaji wa kwanza wa zamani kuchukua nafasi hii huku wachezaji k**a vile Giovane Elber (50) na Claudio Pizarro (44) wakiwa tayari wamechukua kazi sawa na klabu.
✅Tangu alipostaafu mwezi Oktoba kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya goti, Ribéry amekuwa akifanya kazi k**a kocha msaidizi katika klabu ya Serie A, Salernitana ambaye kwa sasa ipo nafasi ya 12.
17/11/2022
ASH*TAKIWA KWA MAKOSA 232 KISA KAMARI TU.
✅Mshambulizi wa Brentford raia wa Uingereza Ivan Toney mwenye umri wa miaka 26 amesh*takiwa na Chama cha Soka nchini Uingereza kwa makosa 232 ya ukiukaji wa sheria yalitendeka kuanzia 25 Februari 2017 hadi 23 Januari 2021.
✅Sheria ya FA nchini Uingereza inawazuia wachezaji wote wakiwemo wanaoshiriki ligi kuu Uingereza , Ligi ya wanawake Uingereza, Ligi daraja la kwanza pamoja na michuano mingine ya mpira wa miguu iliyo chini ya chama Cha soko nchini Uingereza kujihususha na KAMARI.
✅Katika muda uliotajwa Toney amewahi kuvitumikua v vilabu vinne tofauti ambavyo ni Scunthorpe United, Wigan Athletic, Peterborough United na Brentford.
Hadi hivi Sasa nyota huyo amefunga magoli 10 ndani ya EPL akiwa na Brentford lakini hakujumuishwa ndani ya kikosi cha Uingereza kuelekea Qatar kombe la Dunia lakini Toney anapaswa kulijibia hilo ifikapo 24 November 2022.